Sasa hatumii katiba bali anaongoza kwa mawazo yake binafsi na ushauri wa Daud Bashite tu
Magufuli anavunja katiba sana.
Mfano, amevunja katiba kwenye marufuku ya mikutano ya kisiasa.
Mara nyingi nimesema amevunja katiba katika hilo.
Lakini, kwenye kuto renew mkataba wa CAG Assad, hakuna alipovunja katiba.
Dalili zinaonesha kwamba haku renew mkataba wa CAG Assad kwa sababu Assad ni mtu wa msimamo. Na ukifuatiliwa ATCL inavyooelekwa, na ilivyokingiwa kifua ili isikaguliwe vitabu vyake na CAG, utaona Magufuli hana imani kwamba Assad anaweza kuficha madudu. Kwa hiyo inaonekana kamtoa u CAG, ili aweke mtu wake ambaye ana imani naye.
Lakini hajamtoa kwa kuvunja katiba.
Ni muhimu tutenganishe nia mbaya na kuvunja katiba. Na ni muhimu tujue kwamba mambo ya nia ni vigumu kuyathibutisha kisheria.
Magufuli amefanya Technical Knock Out.
Kama una kifungu cha katiba unachosema kavunja, kiweke hapa tukijadili.
Tumseme kuhusu kuvunja katiba anapovunja katiba kweli.
Tukimsema kuhusu kuvunja katiba, katika jambo ambalo hajavunja katiba kama hili la kuto renew mkataba wa CAG, hata anapovunja katiba kweli, kama kwenye kukataza mikutano ya kisiasa, tukisema kavunja katiba, tutaonekana walalmishi tu.
There is such a thing as crying wolf.