Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Watanzania tuamke, Katiba ya mwak 1977 ina-limit mihula miwili ya miaka mitanomitano, ndiyo maana kabla ya hiyo katiba muda wao ulikuwa unabadilika.

Heb tupitie historia kidogo.
View attachment 1252969
View attachment 1252970
Yaani prof. Assad anavyochukiwa, hadi picha yake kwenye website (National Audit Office of Tanzania » The CAG) walishafuta kwenye orodha ya ma-CAG.

-Je, kafikisha miaka 60? (Mussa Juma ASSAD Born : 6 October 1961)
-Je, sheria ilibadilishwa lini kustaafishwa kabla ya miaka 60? (Mandatory retirement also known as enforced retirement or compulsory retirement)
-Je, anaumwa ama ametiwa hatiani na tume ya maadili?
-Je, Rais amefuata katiba inavyosema?

View attachment 1252957
View attachment 1252749
Hivi ni nini kisichoeleweka hapo?

....Even the president shall hold the office for a fixed term of five years and is elegible for re-election for one term only..

Ufìpa translation is JPM is not eligible for re-election..
 
Pamoja na kuwa sio mwanasheria hapa najua unapotosha, kinachozingatiwa hapa sio umri tu bali ni kuwa pale CAG akiteuliwa kwanza atamaliza miaka yote ya kipindi alichoteuliwa yaani miaka mitano ya mwanzo ,baada ya hapo anaweza kuteuliwa tena (angalizo na sio lazima kama vilaza walivyoshupalia neno (eligible) nadhani hawajui tafsri ya neno eligible ,neno eligible halilazimishi ni sawa tu na kusema ''anastahili'' )kwa miaka mingine mitano ambayo hataongezewa tena,hapa kiliwekwa kwanza kipindi cha miaka mitano,na maana yake ni kuwa anaweza kutoteuliwa tena kinapokuja kipindi cha pili cha miaka mitano,mnaolilia na ukihiyo wenu wa sheria mngejiuliza kwanini haikuwekwa miaka kumi moja kwa moja na ikawekwa miaka mitano mitano? maana yake yule aliyemteua anaweza tu kumyoa kwa kutomuongezea miaka mingine mitano,hiyo ndio kinga ya CAG. Kule Marekani Trump anatoa na kuingiza pale anapoona hufai tena yeye anatwit tu,hata ungekuwa kwenye ziara ,mnakumbuka yule aliyekwa waziri wa mambo ya nje alipokuwa ziarani Kenya kibarua kikaota mbaya,pamoja na hizo kanuni sijui katiba mwisho wa yote anayeteua ndio mwenye mamlaka ya kutengua,kama alivoteua kwa raha zake pia atatengua kwa raha yake.

Kaka utashupaza mishipa yote ya shingo weeee...
Lakini unatetea ubeberu na ukandamizaji wa haki za watumishi!
Labda huko serikalini ndo mambo hayo ya kuviziana yanafanyika..!
Private sector uteuzi wa kibabe kiasi hiki ukitokea dhidi yako then wahi CMA kachukue siti za mbele make Kuna dalili nyingi sana za "Un-Fair Termination"
Watakuwa wamekurahisishia kustaafu kwa Neema!
 
Kishamaliza miaka yake mitano. Boss kaona haina haja ya kuongezea mhula mwingine. Hakuna katiba iliyovunjwa.
Kwa hiyo na magufuli akimaliza miaka mitano tusimwongezee mitano mingine? Mmeset precedence tayari, 2020 tutampiga chini magufuli msilalamike
 
Shall be eligible doesn’t mean shall be reappointed.

Sijui tatizo ni lugha..????
Kiingereza nintatizo.Wengi wanaopiga yowe hawajasoma English Medium schools wasamehe bure

Cheo Cha kuteuliwa hakiendani na umri wa kustaafu waweza teuliwa hata ukiwa na miaka sabini ukitokea popote hata sekta binafsi kwa CAG..Mfano Raisi kana akimteua CAG kutoka kampuni binafsi ya ukaguzi Mfano PwC akiwa na miaka 30 unataka akimaliza muda amfanye Nini? Ananpa mafao yake Case inaishia hapo.Cheo Cha CAG aweza pewa hata kikongwe wa miaka 80 katiba haitamki umri wa CAG .Aweza kuwa hata na miaka 20.Mkataba wake ukiisha kwa heri ya kuonana.

Tatizo wengi humu ni vibarua serikalini au wakereketwa wa vyama ambao hawajawaha ajiriwa sekta binafsi kwa mkataba.Mfano unaajiriwa kuwa meneja mkuu wa kiwanda Cha Coca-Cola kwa mkataba wa miaka mitano ukiwa na miaka 30.Ukimaliza hiyo miaka mitano Wana Uhuru wa kukupa Chako na kuachana na wewe au kukuongezea mkataba hakuna Cha kusema ooh umri wa kustaafu wa serikali na sekta binafsi ni miaka 60.Huwezi dai uongezewe muda au upewe kazi nyingine ilii ufikishe miaka 60!!!

Nadhani humu nafikiri wengi hawajui nafasi za uteuzi maana yake wanafikiri ni ajira ya kudumu
 
CAG sio sawa na waziri au internal auditor.

Ni taasisi muhimu kikatiba katika kusimamia misingi ya utawala bora, na mipaka ya madaraka/mamlaka ya Serikali kupitia nguzo zake 3 za dola (separation of powers and checks and balances).

Kupitia Katiba rais amepewa mamlaka ya kumteua CAG yasiyo na masharti kama ilivyo kwa mawaziri.

Lakini Katiba imempa ulinzi CAG dhidi ya watawala kupitia masharti (ingawa ni dhaifu) ya kusitishwa kwa ajira yake kikatiba.

Kwakuwa rais wa TZ ana mamlaka kama ya Malkia wa Uingereza, "ulinzi" wa CAG kikatiba unategemea busara za aliyepo madarakani.
Vinginevyo ulinzi dhaifu wa CAG utasababishwa na udhaifu wa Bunge.

Kwasababu kazi ya Bunge kwa mujibu wa Katiba ni kuisimamia na kuidhibiti Serikali.

Sasa changanya na "the hallmarks of bad governance (ambiguousness, arbitrariness and capriciousness) ulinzi wa CAG hapo ni SIFURI!
 
Refarii anaposema mpira kati basi goli limeshahesabika. Haijalishi kama ni goli la mkono, la offside, au mfungaji alicheza rafu kabda ya kufunga!

Kinachobakia ni mijadala ya mashabiki kuhusu goli hilo kitu ambacho hakiwezi kubadili maamuzi ya refa. Na tugange yajayo
 
Profesa Asad siji msahau na uchochezi wake kipindi Cha UKUTA wa CHADEMA bapo alienda press na kutoa madhaifu ya serikali yakiyo kwenye ripoti ya ukaguzi ya CAG kabla hajakabidhi ripoti kwa Raisi kitu ambacho ni kinyume kabisa Cha maadiili ya ukaguzi.

Kitu kilichochochea zaidi watu kuwa against na serikali. Na aliifanya kusudi Sijui kwa Nini siku zile hakukamatwa kushughulikiwa

Ukishakagua ripoti unatakiwa ukabidhi kwanza kwa aliyekupa kazi ya ukaguzi yeye akakurupuka. Mimi ni mmoja wa waliopiga yowe kuwa afungishwe virago na NBAA wamfutie usajili kwa kukiuka maadiili ya ukaguzi.

Profesa Assad hakuwa na maadiili ya ukaguzi Bora kafungishwa virago akalee wake zake wanne
 
Kwani yeye Asadi au Mke na watoto wake wanasemaje? Asadi alishawahi kukuomba hela ya kula?
Du sijawahi kusikia jibu ka kipuuzi kama hili? Kumbe Prof Assad alikuwa akifanya kazi kwa manufaa yake binafsi sio kwa manufaa ya nchi kwa ujumla??? Mkuu una mawazo mgando sana.
 
Mi ninachofurahi ni kuwa neno "shall be eligible" tutalitumia tena kwenye vikao vyetu kumchinja yule malaika mkuu,

wanasemaga "mkuki kwa nguruwe kwa binadamu chungu"

Mzee Membe jiandae 2020, wembe uliomyoa CAG ndo tutautumia kumyolea malaika mkuu
 
Watanzania tuamke, Katiba ya mwak 1977 ina-limit mihula miwili ya miaka mitanomitano, ndiyo maana kabla ya hiyo katiba muda wao ulikuwa unabadilika.

Heb tupitie historia kidogo.
View attachment 1252969
View attachment 1252970
Yaani prof. Assad anavyochukiwa, hadi picha yake kwenye website (National Audit Office of Tanzania » The CAG) walishafuta kwenye orodha ya ma-CAG.

-Je, kafikisha miaka 60? (Mussa Juma ASSAD Born : 6 October 1961)
-Je, sheria ilibadilishwa lini kustaafishwa kabla ya miaka 60? (Mandatory retirement also known as enforced retirement or compulsory retirement)
-Je, anaumwa ama ametiwa hatiani na tume ya maadili?
-Je, Rais amefuata katiba inavyosema?

View attachment 1252957
View attachment 1252749
20191104_071838.png

Ibara ya 40..
20191104_071022.png

Hii ni reference kwa wale wabishi. Neno SHALL lipo kwa rais pia. Nimeweka ya kizungu na kiswahili mpate tafsiri wenyewe ya maneno SHALL BE ELIGIBLE.
Matukìo kama haya ndio yanaonyesha jinsi tulivyo na wanasheria wabovu. Hawajui hata kutafsiri sheria.
CAG muda wake umeisha leo.
 
Tumtakie CAG Mstaafu, Prof. Mussa Assad kustaafu kwema na amestaafu kwa heshima na kwa mujibu wa sheria na sio kwa hoja zozote za vitatange na vibirifitina, jina lake litaandikwa kwenye kile kitabu cha mashujaa wa kweli wa taifa wetu kwasababu ameacha Legacy.

Karibu CAG Mpya, Charles Kicheere, tunakutakia kazi njema.
Paskali
Vipi kuhusu picha yake kuondolewa kwenye tovuti rasmi ya serikali? Sawa hii?
 
Kasome vizuri sharia ya CAG
Atakaa madarakani kwa miaka mitano
Ni uamuzi wa ngazi ya uteuzi kumuongezea muhula au la
Assad atarudi kwenye ajira yake UDSM
Assad hajawahi kuwa na njaa. Very soon ataenda kufanya kazi IMF au WB. Kufanya kazi na majitu mbumbumbu ni sawa na kubeba gunia la misumari.
 
Back
Top Bottom