Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Kama tumemuamini tumuache Rais atekeleza majukumu yake. Maneno mengi hayana faida wala hayana msaada kwa taifa tuwaache wazee walio juu wazungumze naye kama kuna ukweli. Tunaongea sana mpaka tunaharibu.
Mkuu kumbuka rais aliapa kulinda katiba yetu kwa kinywa chake..
 
Uko sawa mkuu, katiba haijavunjwa ni msimamo wake ndiyo umemponza.
Katiba imevunjwa waziwazi, katiba inasema lazima awe ametimiza miaka 60.Assad ana miaka 58.kwa kufuata katiba rais alipaswa kumwondoa 2024 kama angeona hafai.
 
Umeeleza vizuri mwishoni umejichanganya, rais wetu amevunja katiba waziwazi.Assad alipaswa kustaafu 2024 kama rais asingetaka kumuongezea miaka mitano ya ziada iliyowekwa Na katiba, Na hiyo ya nyongeza anapaswa kumuongezea MTU asiyezidi 65 years.
 

Paskali huyu Mussa Assad hajastaafu bali amemaliza mkataba wake wa Miaka mitano!!! Akipenda anaweza kurudi UDSM akafundishe ndio astaafie huko!!
 
Paskali huyu Mussa Assad hajastaafu bali amemalia mkataba wake wa Miaka mitano!!! Akipenda anaweza kurudi UDSM akafundishe ndio astaafie huko!!
Huo mkataba alipaswa kumaliza 2024, sababu kuu kwa sasa ana miaka 58 katiba hairuhusu yeye kuondolewa kwa vile umri Wa kustaafu bado, kinachofanya ifike 2024 ni kwa vile katiba inatamka fixed terms of 5 years.baada ya hapo rais angeweza muongezea miaka mitano mingine angependa.
 

Hapana kuna kipengela hujakisoma vizuri; anaweza kuteuliwa kipindi chapili iwapo mamlaka ya uteuzi itaona inafaa!!!
 
Umeeleza vizuri mwishoni umejichanganya, rais wetu amevunja katiba waziwazi.Assad alipaswa kustaafu 2024 kama rais asingetaka kumuongezea miaka mitano ya ziada iliyowekwa Na katiba, Na hiyo ya nyongeza anapaswa kumuongezea MTU asiyezidi 65 years.
Naomba unukuu maneno ya katiba yanayoonesha rais kavunja katiba.

Katiba inasema CAG hawezi kuongezewa muda baada ya kutumikia serikali kipindi cha pili.

Mwisho wa utumishi wake kama CAG ni miaka 10.

Baada ya miaka 10 hatakiwi kuongezewa muda tena kwenda kipindi cha tatu.

Katiba haijasema CAG akitumikia kipindi cha kwanza cha miaka mitano, ni lazima aongezewe mkataba kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Hivyo rais, ana haki ya kutoongeza muda wa CAG baada ya kipindi cha kwanza cha miaka mitano, kwa sababu yoyote au bila sababu.

Bila ya kuvunja katiba.

Na kama unafikiri kuna sehemu katiba imevunjwa, weka hiyo sehemu hapa tuichambue.

Mimi sipendi uongozi wa Magufuli. Sipendi kwa mfano ATCL ilivyoenda kisiasa na CAG akakatazwa kukagua vitabu vya kihasibu. Assad alikuwa CAG mwenye msimamo, na inaonekana anaondolewa kwa sababu ya msimamo wake.

Lakini, katika hili la Assad kuondolewa, hakuna sehemu ambapo katiba imevunjwa.

Sipendi utawala wa Magufuli kwa sababu unavunja katiba mara nyingi.

Marufuku ya mikutano ya siasa ni kuvunjwa kwa katiba. Magufuli kavunja katiba hapo. Let's call him out on that.

Lakini hii habari ya Assad kuondolewa hakuna sehemu katiba imevunjwa.

Kama unafikiri kuna sehemu katiba imevunjwa, tujadili katiba imesemaje neno kwa neno.
 
Paskali huyu Mussa Assad hajastaafu bali amemalia mkataba wake wa Miaka mitano!!! Akipenda anaweza kurudi UDSM akafundishe ndio astaafie huko!!
Zile posts 5 za juu za executives, CDF, Director wa TISS, Director wa PCCB, IGP na CAG, baada ya utumishi wa ngazi, haruhusiwi kuhudumu kwenye executive position yoyote.
P
 
Mkuu soma historia ya Ma CAG waliopita, hakuna miaka kumi tu? Kwa mfano aliyepita ameongoza muda gani? Vipi yule Wa kwanza.pia kuna umri Wa kustaafu kuanzia miaka 60, kumbuka Assad ana miaka 58.Hawezi staafu maana bado umri huo...Wa kustaafu.
 
CAG mpya amefinyangwa, ametayarishwa na kujazwa yale ya yule atakayo just to be complete accord with him regardless to the brunders that will be committed.
Napata mashaka na ule utumbuaji uliofanyikaga TRA mpaka mtu akapelekwa kuwa katibu tawala and all over the suddenly leo ni CAG!
 
Katiba imevunjwa waziwazi, katiba inasema lazima awe ametimiza miaka 60.Assad ana miaka 58.kwa kufuata katiba rais alipaswa kumwondoa 2024 kama angeona hafai.
Lakini sikamaliza mkataba wake wa miaka mitano? Kwahiyo apewe mkataba wa miaka miwili kinyume Cha katiba? Kwa kumwangalia tu hiki kibabu so Kona miaka sabini kweli? Wengine mwishowe tutawapima dna
 
Wengine wanasema miaka 5 huku wengine mpaka atimize miaka. Nyie jamaa kwakweli mnawapotosha wa tz. Bora nitafute Jembe nikalime naona sielewielewi kama kunde au maharage.
 

Tatizo hamjui sheria kusoma hakuna sheria iliyo vunjwa hapa acheni ushabiki.
 
Wengine wanasema miaka 5 huku wengine mpaka atimize miaka. Nyie jamaa kwakweli mnawapotosha wa tz. Bora nitafute Jembe nikalime naona sielewielewi kama kunde au maharage.

Kama huelewi si ubakie kuabudu katiba binafsi toka chato na kolomije
 
Yale makosa ya TRA yalijifuta!?
 
Haheshimu wazee kabisa. Wakisema anawaambia wanawashwa washwa. Wakilalamika hata kwa njia ya waraka inakuwa taabu, anadukua mpk maongezi yao ya simu
Aliwahi hata kutaka kuwabambikia kesi za uhujumu uchumi akaogopa watamsomea Albadiri akaacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…