Suala la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Vipengele kadhaa vya Kisheria

Upo sahihi kabisa!!!
 
Umeeleza maana ya "shall" kwa mujibu wa nini?! Mimi nimeeleza kwa mujibu wa sheria zetu, na nimeweka kifungu!
Sasa kama wewe umeeleza maana ya shall kwa mujibu wa sheria zetu, na mimi sijakataa maana ya shall uliyoieleza, tatizo liko wapi?

Nimekuuliza unaelewa objection yangu iko wapi, hujajibu.

Ni kwa sababu huelewi na hutaki kukubali kwamba huelewi au ni kwa sababu gani?

Unaelewa objection yangu?
 
Tatizo Raisi amefanya haya kwa Mihemko, Kudanganywa na Kujidanganga, Kushauriwa vibaya na Kujishauri vibaya na On top of that Kwa CHUKI binafsi.

Raisi amevunja Katiba ALIYOAPA kuilinda huku akimtaja MUNGU anayedai kumtanguliza mbele'
Ngoja tusibiri hayo madongo wakati wa uapishaji wa voda fasta!!
 
Nimejibu nilichokujibu kwa sababu umesema hilo neno SHALL tunalitafsiri vibaya... na mimi ndo nimekuambia neno SHALL limetafsiriwa na sheria zetu wenyewe! Kwahiyo kama kutafsiri vibaya, basi ni sheria zetu ndizo zimetafsiri vibaya na sio "..sisi"

Aidha, umesema:-
Ukiandika "shall be eligible for renewal" hapo ulazima unaongelewa kwenye eligibility. Eligibility ni potential ya kuwa CAG, si lazima aliye eligible kuwa CAG.
Hapo ingekuwa sio lazima, kwa mujibu wa sheria zetu wangeandika "may be be eligible for renewal" na sio "shall be eligible for renewal"

Msingi haupo kwenye neno ELIGIBLE bali kwenye neno SHALL. Lau kama wangeandika "may be eligible" hapo ingekuwa sio shuruti!!
 
Hawa wanadakia mambo ila IFRS amemaliza ubishi aliposema:


CC: Chige uache ubishi wa kitoto
 
Mkuu tunakushukuru saana kwa kutuchambulia na kutufafanulia kwa uhakika kabisa na kisheria.kuhusu kutenguliwa kwa CAG na Mamlaka aliyonayo CAG
Sasa ndio tunazidi kufahamu ukweli upo wapi

Tuliambiwa kuwa Prfs Musa Asaad ametenguliwa kwasbb ya umri wake umefika mwisho.pia tukaambiwa kuwa ana umri wa miaka 60.Hio ndio ni sababu kuu ya kutenguliwa
Kumbe Prfs Asaad ana miaka 58..!!!
Hii ni Aibu ya wazi kabisa na inaonesha dhahiri kuwa panachuki binafsi baina ya viongozi wa Nchi hii[emoji2211]
 
Mleta mada unahangaika na neno shall unasahau neno eligible !! Kuteuliwa Soo automatic kunategemea eligiblity pia .Chukulia CAG labda ni kibaka kwa hiyo.umuongezee muda tu kwa ku base neno shall !!!
Bila ku consider eligible?

Pili hata Kama angepewa ingeleta usumbufu usio na sababu.Katiba inasema umteue kwa miaka mitano na anatakiwa kustaafu akiwa na miaka 60 ina maana Raisi angempa U CAG angevunja Katiba sababu anampaje mtu miaka mitano anayejua kabisa miaka 60 anatakiwa kuondoka .Akimpa mitano kavvunja Katina kampa mtu ambaye hastahili sababu ya umri na katiba haisemi apewe u CAG kwa miaka miwili.Raisi angempa angekuwa kavunja katiba

Umri wa CAG Assad kuteuliwa kikatiba ulikuwa umefikia ukomo
 
Unaelewa eligible maana yake ni nini?

Unaelewa kinachoongelewa hapo ni nini?
 
Tatizo Raisi amefanya haya kwa Mihemko, Kudanganywa na Kujidanganga, Kushauriwa vibaya na Kujishauri vibaya na On top of that Kwa CHUKI binafsi.

Raisi amevunja Katiba ALIYOAPA kuilinda huku akimtaja MUNGU anayedai kumtanguliza mbele'
Haya ni matokeo ya kuwa na "weak legal institution" poor attoney general......
 
Ndio uelezee objection yako ilipo ili wengine tupate faida
 
Na wale mliokuwa mnatumia tafsiri ya Prof Shivji na kudai kwamba hapana ulazima huo, hatimae Prof ameona kosa lake na kusema:-
 
shall be eligible ikageuka kuwa must be eligible??

Na kama ni must hiyo miaka mi5 yanini?
si wangeunganisha tu bila eligible?
Mkuu mleta mada neno eligible kaliacha makusudi.Katiba inasema CAG apewe miaka mitano.Lakini lazima astaafu akiwa na miaka 60.profesa Assad Ana miaka 58 ukimpa mitano na huku unajua anastaafu na miaka 60 ina maana umempa mtu U CAG ambaye sio Eligible kwa umri.wake sababu atatumikia miaka Miwili tu na katiba haitoi mamlaka ya mteuzi kumpa miaka Miwili.Kikatiba profesa Asad kafikia ukikongwe wa kutoteulika Kama CAG sababu ya eligiblity ya umri

CAG Assad is disqualified by age as per professor Issa Shivji statement
 
Ndio uelezee objection yako ilipo ili wengine tupate faida
Mara ngapi?

Nimeeleza hapo juu kwamba kipengele cha shall be eligible kinaelezea term limits.

Kwamba CAG hatakiwi kuwa CAG baada ya terms mbili. Kama rais.

Sasa, kama habari ya "shall be eligible" inaelezea kwamba CAG hatakiwi kuendelea kuwa CAG baada ya terms mbili (term limits) kwa nini kipengele hicho kiwe relevant kwenye mjadala wa CAG kuondolewa baada ya first term yake kuisha?

Ni kama vile mtu anasema kwamba, kwa sababu mwisho wa urais ni vipindi viwili vya urais, basi rais asipigiwe kura katika uchaguzi wa rais baada ya miaka mitano kuisha.

Totally unrelated.
 
Sifahamu... eleza wewe kwa kuangalia muktadha huu na bila kukiuka vifundgu vya sheria zetu!!
Sasa kwa nini unashupalia vitu usivyoelewa?

Eligibility maana yake ni kuwa na sifa za nafasi, cheo, haki etc.

Mtu mwenye miaka zaidi ya 18 na mwenye akili timamu ana eligibility ya kupiga kura.

Lakini, hilo halimaanishi kila mwenye eligibility anapiga kura.

Wabunge wote wako eligible kuwa mawaziri.

Lakini, si wote wanateuliwa kuwa mawaziri.

Sasa kwa nini watu wanataka kufanya eligibility iwe inamfanya mtu automatically a hold office?

Wahasibu wote Watanzania wenye uzoefu wako eligible kuwa CAG. Lakini si wote wanaoteuliwa kuwa CAG.

Kwa nini watu wanatafsiri eligibility kama ni automatic appointment to office?
 

Ni kilaza tu amabaye hatakuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…