Tabata, Dar: Anayedaiwa kutaka kuiba bodaboda na kujeruhi ateswa kwa kukanyagwa na gari

Tabata, Dar: Anayedaiwa kutaka kuiba bodaboda na kujeruhi ateswa kwa kukanyagwa na gari

Sijaingalia hiyo video lakini wezi hawama huruma hata tena kama hawa wa bodaboda wameua Sana maana wanataka kuichukua mwenyewe hataki ataacha kumuua, jamani acheni wauawe maana hiyo kwao ni ajali kazini hajalishi kafaje
 
Wabongo ni watu makatili sana
Mambo ya kisiwa cha amani ni maneno tu


Sana ,yeye si kajiona mafia
Shupavu,
Sema pale sifa kujionesha mwamba
Anauza sura kabisa

Ova
Zamani tulikuwa wema na kisiwa cha utulivu kweli maana kila kitu tulisema na kushauriana tumuachie Mungu, Kwa sasa ni mwendo wa kulipiza, mwenye huruma hayajamfika
 
Habari wanajamvi,
Kuna hii Video nimekuta inatrend sana huko jamhuri ya Twitter leo hii na inasemekana hapo ni nchini kwetu Tanzania.

Sihitaji kuongelea wamefanya nini wala la kujichukulia sheria mkononi, lakini ni kiwango kikubwa sana cha unyama kilichofanywa na huyu mwenye Gari jeusi. Ni udhalilishaji mkubwa wa mwili wa mwanadamu na unapaswa kupigwa vita na kuchukuliwa hatua mara moja.

Huyu raia mwenye gari nyeusi ni "Psychopath" kabisa na anachokifanya ni zaidi ya mwananchi mwenye hasira kali.
Inabidi upigwe ban wewe, unaleta umbea bila video ili iweje?
 
Sijaiona video lakini naweweseka. Sipati picha aliefanya hilo tukio yupo na hali gani
 
Mbaya sana hii!!
Sheria mkononi haifai.
Njoo Dodoma maeneo ya Chamwino, Chinangali na Chang'ombe tembea kuanzia saa tatu na nusu usiku ukinusurika leta mrejesho haijalishi ni me au ke lazima wakunajisi halafu wameathirika, pili wanakuibia na mwisho wanakutoa uhai, ukinusurika kuuawa la Kwanza na la pili ni lazima, ni lazima (Kwa msisitizo) je hao ukiwakamata utawapa chai wanywe waondoke?
 
Mwizi anastahili kila aina ya adhabu...hilo halina ubishi.
 
Zamani tulikuwa wema na kisiwa cha utulivu kweli maana kila kitu tulisema na kushauriana tumuachie Mungu, Kwa sasa ni mwendo wa kulipiza, mwenye huruma hayajamfika
Zamani lini hiyo
Wezi wamekuwa wakiuwawa wakivishwa
Mataili kitambo tu

Nani kwanza kakuambia tz ni kisiwa cha amani
Bongo hakuna amani sema kuna utulivu tu!
Hakuna watu mafia wenye roho katili kama wabngo
Kwenye matukio inajidhihirishaga

Ova
 
Nimeangalia haitishi kabisa.
Ila aliyefanya hivyo akalale ndani au afungwe iwe fundisho
 
Yaani nyie mnaotetea hao wezi endeleeni labda hayajawakuta na ningekuwa mm nahisi ningemnyofoa hiyo mikono na miguu ninahasila nao sana..

Nakumbuka mwaka jana niliibiwa pesa zangu kama 2.5 million pamoja na laptop yangu na ubaya zaidi hiyo hela nilikua nahitaji kumlipia baba mkwe wangu kwenye matibabu kesho yake asubuhi kiukweli nilikwama kuipata hela nyingine kwa wakati mpka yule baba akafariki (R.i.p to him) na sahv binafsi nikimkamata mwizi yaani nampa maji ya betri tu akajifie mbele
 
Aliyerecord ni mkuda sana... kahakikisha dereva anaonekana live ili akamatwe huku yeye anafurahia huyo anayedhaniwa Mwizi akanyagwe kanyagwe...

Anakuchekea huku anakung'ong'a
Haya maviswahili ya ajabux2 mnayatoa wapi? Kung'ong'a ndio nini?
 
Mbona jamaa anampapasa..anamaliza mafuta bure..uyo wangemchoma moto tu...
Wezi wa pikipiki wao huua ili kupata pikpik
Kuna jamaa mmoja mitaa ya homu alikuwa dereva bajaji hao wahuni wakamkodi wakaenda kumuulia vichakani huko na kutelrkeza mwili huko na kuondoka na bajaji yake!

Ndio alikuwa tegemeo kwa mke wake na watoto,! Sasa hivi ukiwaona mke na watoto wanavyohangaika unabaki kuwahurumia.

Imagine dada wa watu hata miaka 40 bado ila tayari ni mjane kwa ajili ya wajinga kama hao!
 
Back
Top Bottom