siku moja nilibeti nikaliwa laki 6 na 80 elfu kwa siku moja, na siku hiyo ndo mshahara ulikuwa umetoka na kabla sijanunua chakula ndani kodi ya chumba nadaiwa nikasema ngoja nibeti walau ifikike milion moja then ndiyo nifanye mahemezi, nilipe kodi na kufanya mengine madogo madogo, lakini kilichotokea nililiwa hiyo more than 600k bado sijaanza kulala njaa na kodi nadaiwa, nikarudi geto nikajifungia nikapiga magoti nikalia kwa uchungu nikasema "EE MUNGU NAOMBA PEPO LA KUBETI LINIPITE MBALI ".
Nikaingia you tube nikatafta clip ya pastor mmoja ili nitubu maana nikawa naona kusubiri jumapili kanisani ni mbali, nikaipata clip moja ya pastor anaitwa CHRISTOPHER MWAKASEGE akiwa anawaongoza watu toba na kuziungama dhambi zao, nikawa nawafatisha maneno alokuwa anayasema huku nikiwa nimepiga magoti kabisa geto,
Nikaapa kabisa sitorudia kubeti, lakini nilikaa siku 5 tu sijui shetani akatokea wapi nikauza redio na pesa yote nikabetia na ikaliwa kilichofata ilikuwa ni kupiga punyeto kupunguza machungu na msongo wa mawazo na ndiyo tabia yangu hadi leo, so natamani kabisa kutoka kwenye hiki kifungo lakini imefika muda roho yangu ndani inanambia kabisa kuwa siwezi tena kutoka, najikuta kama teja flani tu ivi