DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mimi nipo kwenye hii kada ya ujenzi, kwahiyo nitakachokujibu naomba uniamini. Ukijenga jengo refu kama hilo bila kibali, kinachotakiwa kufanyika ni kulivunja kwanza, halafu ndio uanze kutoa hayo maelezo ya michoro nk.

Au laaa, utoe rushwa ya kueleweka, yaani rushwa kubwa. Maana watu wanaweza kufa hapo.

Nimemaliza na sitaki maswali.

kwa hiyo hujui kama kuna namna ya kukagua ametumia viwango gani vya ujenzi kulinganisha na michoro, iwapo ataibuka na michoro na vibali

kama hakuna jinsi ya kujua amejengaje basi majengo makubwa yanapaswa kukaguliwa hatua kwa hatua wakati wa ujenzi, mfano kukagua ususi wa vyuma kabla ya kumwaga zege

na pia bango liko wapi ? wahandisi wa manispaa nao wamezembea kutoliona jengo linajengwa mpaka ghorofa ya nne bila bango. Wajumbe na wenyeviti wa mitaa wana uwezo wa kushtukia na kuripoti Wasomali haramu kwenye maeneo yao within 3 days of arrival, lakini Mkurugenzi wa Halmashauri haoni jengo la floor nne lisilo na bango ! Vicarious negligence ya serikali inahusika.
 
Hakuna Cha unafiki,mbona mnalalamikia Ufisadi then fisadi unamtetea tena ,Huwa mnalalamikia nini Sasa?
Unajua kuna kitu kinaitwa 'uhuru wa mawazo/fikra'.
Usiforce kila mtu awe na mtazamo sawa na wako.

Ungepata wewe fursa usingejenga? Acha kuhubiri pepo ikiwa mwenyewe huna hakika ya matendo yako.
 
View attachment 2630959View attachment 2630960


Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia (pichani), maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.

Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.

Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.

Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.

Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.

Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.

Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.
unaweza kukuta hii post ni ya fundi mwenyewe. anyway Boni kazingua. Komesha rushwa
 
Moderator futeni huu uzi
1. Hakuna udhibitisho kama jengo liko chini ya kiwango
2. Hakuna udhibitisho kama mmiliki halali ni yeye.

Jamiifroum isiwe chaka la kuaribiana CV za watu yaani hii kama ni chuki na mtu ni sawa na kuchukua picha yake na jengo linalosemekana lake than nichonganishe hii sio haki kabisa, heshimuni maisha ya watu na kazi zawatu. kama mtu unauhakika na hili kwann usipeleke sehemu husika wadeal nae. Ukipaste hilo jina kwenye Google utaiona hiyo picha iko linkedin sio sawa imechukuliwa ikapastiwa hapa.
 
Wizi wizi wizi
Ndio maana kila mtu anataka kazi Tra sasa

Sasa kila mtanzania atataka akafanye kazi Tra,wanaweka pesa mpk kwenye makabati ya nguo nyumbani

Wengi wao watumishi wa Tra wanachezea sana pesa na wanawake
 
Unajua kuna kitu kinaitwa 'uhuru wa mawazo/fikra'.
Usiforce kila mtu awe na mtazamo sawa na wako.

Ungepata wewe fursa usingejenga? Acha kuhubiri pepo ikiwa mwenyewe huna hakika ya matendo yako.
Binadamu huwa tuna unafiki wa kuona jambo ovu ikiwa analifanya mwingine tukifanya wenyewe tunatafuta kila jina zuri kuhalalisha uovu yetu.

Hapa mijitu imeshupaza shingo kusema jamaa ni mla rushwa ila wangepata wao nafasi hizo hizo wangeita fursa na kufanya yao.
 
Moderstor futeni huu uzi
1. Hakuna udhibitisho kama jengo liko chini ya kiwango
2. Hakuna udhibitisho kama mmiliki halali ni yeye.

Jamiifroum isiwe chaka la kuaribiana CV za watu yaani hii kama na chuki na mtu ni sawa na kuchukua picha yake na jengo linalosemekana lake than nichonganishe hii sio haki kabisa, heshimuni maisha ya watu na kazi zawatu. kama mtu unauhakika na hili kwann usipeleke sehemu husika wadeal nae. Ukipaste hilo jina kwenye Google utaiona hiyo picha iko linkedin sio sawa imechukuliwa ikapastiwa hapa.
Ukute mmoja wa hao moderators ndio kaandika huu uzi baada ya kuona wivu jirani yake kujenga gorofa halafu unatarajia uzi ufutwe.

Huu uzi ingekuwa nchi za ulaya ni rahisi sana mtu kufungua kesi ya defamation na kupata pesa nyingi.

Alioandika uzi hana ithibati yeyote aliyoweka juu ya madai yake zaidi ya picha ya jengo na picha ya huyo aliemtaja.
 
Hawa washenzi ndio wanabambikia watu kodi za bilioni 30 kwenye kontena za vitenge mbwa hawa.., aeleze pesa katoa wapi mbwa huyo!
Hawa washenzi watumishi wa Tra ukiwakuta wanavojidai wana pesa,siku hizi hela wakichukua hawapeleki benki wanaweka nyumbani kwenye makabati ya nguo.


Hizo ni rushwa wanazochukua kwa wafanyabiashara kila siku

kwa hali hii watz lazima wakwepe kulipa kodi.
 
Unajua kuna kitu kinaitwa 'uhuru wa mawazo/fikra'.
Usiforce kila mtu awe na mtazamo sawa na wako.

Ungepata wewe fursa usingejenga? Acha kuhubiri pepo ikiwa mwenyewe huna hakika ya matendo yako.
Kelele mnazopigaga kuhusu Ufisadi Huwa mnamaanisha nini ikiwa Mafisadi mnawaona ni wajanja na mashujaa?
 
Wivu tu unakusumbua.
Ukiona ghorofa imesimama hadi hapo jua ana kibali tayari vinginevyo ungeshakuta Alama nyekundu.
Sio wivu hawa jamaa wanakula rushwa haswa,hukuona wafanyabiashara walivokua wanalia juzi

Kodi nyingi haziingii serikalini zinaliwa na watumishi wa Tra
 
Udaktari unakimbiliwa na vilaza mbona wengi tu,
Kuna watu kibao wamesoma PCB wakapiga division one Chuo wakaenda Kusoma B.Com, Tax Nk na ndio hao Wengi wao wako TRA
Kilaza utakatiza wapi kwenye medicine, labda hivyo vyuo mlivyoanzisha huko vichochoroni
 
Kelele mnazopigaga kuhusu Ufisadi Huwa mnamaanisha nini ikiwa Mafisadi mnawaona ni wajanja na mashujaa?
Watumishi wa Tra wanakula kodi zetu alafu wanatuona wengine wajinga

Kuna mmoja alikua anatambia watu kua atoke Tra aende kufanya kazi wapi.


Hawa wanachofanya ni wizi na kukadiria watu makodi ya ajabu ajabu ili mfanyabiashara ashindwe wamuite pembeni

Serikali iwaangalie hawa kwa makini sana,kodi za serikali nyingi mno zinaliwa na watumishi wa Tra
 
Wengi hapa watasema wivu na shutuma kibao

Ila ukweli wa mambo hatuwezi kupiga hatua kama nchi kwa hali hii ya wizi uliokithiri ndugu zangu, Kama jamaa na biashara zake hakuna anaemuonea wivu ila kama ndio Posho na mshahara wa TRA tusidanganyane.

nchi za wenzetu wana maisha sawa kawakua hakuna pesa ya ujanja ujanja.
 
Back
Top Bottom