Uchaguzi 2020 Tamaa za Wateule wa Rais kutia nia Ubunge zitawaponza wengi. Ushahidi huu hapa wa Rais Magufuli na Humphrey Polepole

kauli za wanasiasa zinabadilika badilika ndani ya 24hrs.polepole kabla ya kuwa katibu mwenezi CCM alikua anatoa shit nyingi na mapungufu mengi yaliyomo ndani ya serikali ya CCM.lkn kwa sasa sio yule tena.
 
Ndugu wana JamiiForums, kumetokea hali ya wakuu wa Mikoa na Wilaya kuacha nafasi zao walizoteuliwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli na kukimbilia Ubunge.

Licha ya Rais John Pombe Magufuli kuwataka wateule wake kuridhika lakini tumeona wenyewe wateule wake wamepuuza agizo lake.

Sababu kubwa ninayoiona mimi ni tofauti ya mshahara wa wakuu wa Mikoa na Wilaya ukilinganisha na wabunge.

Ili kufanya wakuu wa Mikoa na Wilaya kuacha kukimbilia Ubunge nashauri waongezewe mishahara yao kwa kuwa kazi wanazozifanya ni kubwa kuliko hata za Mbunge.

Naomba maoni yako
 
Kwanini usishauri wabunge wapunguze mishahara ilingane na Wakuu wa Wilaya.
 
Unaonaje wabunge mishahara na marupurupu ipunguzwe ili wajitokeze wenye nia ya kutumikia wananchi na si kufuata maslahi binafsi?
 
Afterall kwa nini mbunge alipwe mshahara wakati si mwajiriwa, mbunge anastahili kulipwa posho tu za kuhudhuria vikao kama ilivyo kwa madiwani, hiyo mishahara wanayolipwa na serikali inatolewa kama rushwa...na hata hicho kiinua mgongo cha mamilioni ya pesa hawastahili kulipwa..na kimsingi inatakiwa kuwa kazi ya kujitolea na hata kama ni kuchangiwa wanatakiwa kuchangiwa na wanajimbo wanakowakilisha.
 
Your browser is not able to display this video.


Pamoja na tetesi zilizozagaa, nimeshangazwa sana na Makonda kuchukua fomu ya kuwania Ubunge Kigamboni.

Mh Magufuli kaoonyaaa weee lakini wapi, watu hawasikii wala hawaoni. Pengine ndio dempkrasia yenyewe, siujui!
Wanaona wakipata ubunge njia ni nyeupe kuelekea Uwaziri. Na mteuwaji uwaziri, jomba lao, Magufuli, yupo!

Lakini kuna clip Mh Magufuli ameonya, tena ameonya watu kuacha tamaa, kama Dr Mwananzila. Mwananzila alikuwa Mkuu wa Mkoa, akatupa virago akaenda kugombea ubunge kwao na akakosa.

Sasa Mwananzilani historia, sijui yuko wapi.

Magufuli baba endelea kuonya; Mtaka mawili moja au vyote humponyoka.
 
Wewe usieelewa hata JK kama katiba inaruhusu akihami ACT akagombea urais na akashinda itasemekana CCM imetolewa madarakani. Na kwa taarifa yako waliopo upinzani wote 90% walianzia CCM.

ama kweli nmeamini hatuna watu, wewe unabattle rangi ama una battle mindset ya muongozaji?? mnakwama wap upinzani nchi hii jaman! daah nachoka kuskia izi ngonjera za upinzani
 
Yaani watu hawajamwelewa kabisa Mh. Rais. Kila mmoja anataka ubunge target ni kuwa Waziri au Naibu Waziri, na mteuaji ni Mh. Rais, atawakata weee subiri, tamaa itawaponza.
 
Kweli hakuna haja ya kupiga ramli wacha muda uongee
 
Daaah cheo kilimpa kiburi sana huyu Jamaa,,, hivi sasa atajifunza kitu... Ila trust noBody
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…