Uchaguzi 2020 Tamaa za Wateule wa Rais kutia nia Ubunge zitawaponza wengi. Ushahidi huu hapa wa Rais Magufuli na Humphrey Polepole

Uchaguzi 2020 Tamaa za Wateule wa Rais kutia nia Ubunge zitawaponza wengi. Ushahidi huu hapa wa Rais Magufuli na Humphrey Polepole

kauli za wanasiasa zinabadilika badilika ndani ya 24hrs.polepole kabla ya kuwa katibu mwenezi CCM alikua anatoa shit nyingi na mapungufu mengi yaliyomo ndani ya serikali ya CCM.lkn kwa sasa sio yule tena.
 
Ndugu wana JamiiForums, kumetokea hali ya wakuu wa Mikoa na Wilaya kuacha nafasi zao walizoteuliwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli na kukimbilia Ubunge.

Licha ya Rais John Pombe Magufuli kuwataka wateule wake kuridhika lakini tumeona wenyewe wateule wake wamepuuza agizo lake.

Sababu kubwa ninayoiona mimi ni tofauti ya mshahara wa wakuu wa Mikoa na Wilaya ukilinganisha na wabunge.

Ili kufanya wakuu wa Mikoa na Wilaya kuacha kukimbilia Ubunge nashauri waongezewe mishahara yao kwa kuwa kazi wanazozifanya ni kubwa kuliko hata za Mbunge.

Naomba maoni yako
 
Kwanini usishauri wabunge wapunguze mishahara ilingane na Wakuu wa Wilaya.
 
Unaonaje wabunge mishahara na marupurupu ipunguzwe ili wajitokeze wenye nia ya kutumikia wananchi na si kufuata maslahi binafsi?
 
Ndugu wana JamiiForums, kumetokea hali ya wakuu wa Mikoa na Wilaya kuacha nafasi zao walizoteuliwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli na kukimbilia Ubunge.

Licha ya Rais John Pombe Magufuli kuwataka wateule wake kuridhika lakini tumeona wenyewe wateule wake wamepuuza agizo lake.

Sababu kubwa ninayoiona mimi ni tofauti ya mshahara wa wakuu wa Mikoa na Wilaya ukilinganisha na wabunge.

Ili kufanya wakuu wa Mikoa na Wilaya kuacha kukimbilia Ubunge nashauri waongezewe mishahara yao kwa kuwa kazi wanazozifanya ni kubwa kuliko hata za Mbunge.

Naomba maoni yako
Afterall kwa nini mbunge alipwe mshahara wakati si mwajiriwa, mbunge anastahili kulipwa posho tu za kuhudhuria vikao kama ilivyo kwa madiwani, hiyo mishahara wanayolipwa na serikali inatolewa kama rushwa...na hata hicho kiinua mgongo cha mamilioni ya pesa hawastahili kulipwa..na kimsingi inatakiwa kuwa kazi ya kujitolea na hata kama ni kuchangiwa wanatakiwa kuchangiwa na wanajimbo wanakowakilisha.
 
Pamoja na tetesi zilizozagaa, nimeshangazwa sana na Makonda kuchukua fomu ya kuwania Ubunge Kigamboni.

Mh Magufuli kaoonyaaa weee lakini wapi, watu hawasikii wala hawaoni. Pengine ndio dempkrasia yenyewe, siujui!
Wanaona wakipata ubunge njia ni nyeupe kuelekea Uwaziri. Na mteuwaji uwaziri, jomba lao, Magufuli, yupo!

Lakini kuna clip Mh Magufuli ameonya, tena ameonya watu kuacha tamaa, kama Dr Mwananzila. Mwananzila alikuwa Mkuu wa Mkoa, akatupa virago akaenda kugombea ubunge kwao na akakosa.

Sasa Mwananzilani historia, sijui yuko wapi.

Magufuli baba endelea kuonya; Mtaka mawili moja au vyote humponyoka.
 
Wewe usieelewa hata JK kama katiba inaruhusu akihami ACT akagombea urais na akashinda itasemekana CCM imetolewa madarakani. Na kwa taarifa yako waliopo upinzani wote 90% walianzia CCM.

ama kweli nmeamini hatuna watu, wewe unabattle rangi ama una battle mindset ya muongozaji?? mnakwama wap upinzani nchi hii jaman! daah nachoka kuskia izi ngonjera za upinzani
 
Yaani watu hawajamwelewa kabisa Mh. Rais. Kila mmoja anataka ubunge target ni kuwa Waziri au Naibu Waziri, na mteuaji ni Mh. Rais, atawakata weee subiri, tamaa itawaponza.
 
KUNA FUNZO LOLOTE KWA SASA?

Aprili 2019 Rais Magufuli ktk moja ya vikao vya ndani ya chama cha CCM, amemlaumu Naibu Waziri wa zamani wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na aliyewahi kuwa pia RC Tabora ndugu Ludovick Mwananzila kwa kumwita mwenye tamaa nyingi sana

Mwananzila alishika nafasi ya unaibu waziri ktk awamu ya kwanza ya Kikwete na Mkuu wa Mkoa ktk awamu ya pili baada ya kukosa ubunge mwaka 2010

Rais Magufuli anamlaumu Mwananzila kwa kuwa baada ya kukosa ubunge 2010 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa lakini 2015 kwa tamaa zake alirudi tena jimboni kwake kuomba ubunge ilihali ana cheo kikubwa serikalini. Alifika mbali kwa kusema Mwananzila hafai hata kuwa Katibu Tarafa na ndiyo maana kampoteza kabisa

Je, kuna funzo kwa wateule wa Rais Magufuli?

View attachment 1508189
View attachment 1508190
Kweli hakuna haja ya kupiga ramli wacha muda uongee
 
Daaah cheo kilimpa kiburi sana huyu Jamaa,,, hivi sasa atajifunza kitu... Ila trust noBody
 
Back
Top Bottom