Kwa wale wasiojua ni kwamba viapo vya utumishi wa umma vina kanuni na taratibu zake tena vina miiko yake.
Je, wateule wa Rais wakiwemo wakuu wa mikoa na wale wa wilaya walizingatia kanuni na miiko ya viapo vyao wakati wanaenda kuchukua fomu?
Je walijiuzulu uongozi na kuacha kazi?
Je, walifikiria hasara na usumbufu watakaouleta serikalini kwa kuondoka ghafla ofisini?
Je, Rais na amiri jeshi mkuu amewatuma kwenda kutumikia muhimili mwingine?.......Hili Rais Magufuli ameshalijibu kwamba hajamtuma mteule yoyote kugombea ubunge.
Basi, kiufupi kamati kuu ya CCM haitakuwa na kazi ngumu wakati wa kushughulika na majina ya hawa jamaa.
Maendeleo hayana vyama!