Kumbe mitaa yafanana.Huku Mbezi beach washakata tayari!!
Jana usiku pia walikata kuanzia saa 12 jioni hadi kwenye saa saba usiku.
Leo hii wamekata mapema...saa nne kasoro tu!
Eff them.
.....Tanesco veeeepeee mnaogopa kutumbuliwa upele? tafuteni uongo wa kutuambia basi mbona wenzenu TRA wanadanganya kwenye mapato kila mwezi? Mnashindwa kutuambia sie wajinga kuwa nyenyere wameingia kwenye electric dynamo ndiyo maana kuna mgawo wa umeme?
......Kumbe mitaa yafanana.
Jana mbezi beach hapa niishipo umekatika saa 1 asubuhi, ukarudi saa 3.
Saa 2 usiku ukakatika.... Sijui hata ulirudi saa ngapi....
Leo kariakoo umekatika saa 4 hadi Sasa bila bila..
Shirika la kipumbafu sana kuwahi tokea duniani....yaani ni biashara ambayo Wateja wapo tayari kwa huduma , lakini supplier anashindwa kutosheleza demand.SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
*TAARIFA YA KUANZA KUREJEA KWA UMEME *
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake kuwa umeme umeanza kurejea katika Mikoa ya Dodoma, Iringa na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Tanga.
Jitihada zinaendelea kuhakikisha huduma ya umeme inarejea katika maeneo yote nchini.
Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.
Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka
Kwa mawasiliano zaidi
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.facebook/tanescoyetultd
twitter.com/
Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
01/12/2017
Alijisemea Prof Muhongo, tusubiri baada ya muda tutamkumbuka. Wale wanaokumbuka vibanda vya simu za mkononi ukipita posta na baadhi ya maeneo mengi ya miji midogo na makao makuu ya wilaya utavikuta vingi vimeinama kwa uchakavu. Mark my words, kwa kauli ya Muhongo, ipo siku nguzo za umeme zitageuka kuwa "tuliwahi kuwa na umeme miaka ya 2017". Wakati huo tunawahadithia wajukuu zetu amabo kwa wakati huo kibatari ni kawaida. Haiwezekani udanganye watu umejenga viwanda 3006 huku ukiwa una power shading ya aina hii. shame!Wakuu huu mgao wa umeme wa siri siri japo unaonekana kwa macho.. Nasema wa siri kwasababu huana maelezo ili watu tujipange kwa kununua ma generator.. Kwa mfano huku mbeya umeme ni kawaida kukatika sa mbili hasubuhi na kurudi sa tano usiku.
Ikumbukwe umeme kwa hii miaka ni muhimu sana kwa shughuli za viwanda vyetu vidogo vidogo kama saloon, welding n.k
Swali nnalo jiuliza ni nani wa kutumbuliwa kwa huu uzembe wa mgao wa umeme usio na kifani? Maana kama kutumbua kwenye sector ya umeme tumetumbua sanaaa hivi sahivi ni zamu ya nani!?
Na anayejua sababu ya umeme kukatika na huu mgao wa kutisha ni ipi?
nchi ya viwonder
TENA INAONGOZWA NA TUNDU LISSU WA CHADEMAHujuma kwa ponda mali
Umesomeka Mura,... Sasa kichuri hakijaaribika mura??Musoma mpaka sasa umeme hakuna muraa