Tunaomba namba yako ya simu mkuu
 
TAARIFA YA KUOMBA RADHI WATEJA WETU WA BAADHI YA MAENEO WANAOKOSA HUDUMA YA UMEME

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi Wateja wake wa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar Es Salaam wanaokosa huduma ya umeme leo Machi 4, 2018.

SABABU: Ni line zetu za 11kV U9 na line ya NOTDIC 2 kupata hitilafu.

Jitihada zinaendelea kufanyika kuhakikisha hali ya upatikanaji wa huduma ya umeme inarejea katika hali yake ya kawaida.

Tutaendelea kutoa taarifa zaidi.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.

Tafadhali usishike waya ulioanguka au uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:

Kwa mawasiliano

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii:

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Tanesco Yetu

IMETOLEWA NA:

OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

MACHI 04, 2018
 


Mnachelewa sana kutoa taarifa kama hizi sijui kwa nini. Masaa 10 yamepita watu hawana umeme mko kimya mpaka muulizwe?
 
Maeneo ya Bunju usalama barabara ya kwenda kanisa la Efatha bunju waya za umeme zimekatika jana usiku kutokana na upepo mkali wa jana usiku, mbaka muda huu Tanesco awajafika kuja kurudishia zile waya , Tumelala giza jana kijiji kizima cha Bunju mtaa wa kilungule chini Tanesco tafadharini sana ni kazi ya sekunde tu , lakini mnajivuta vuta hivi utafikiri trasforma imeungua.
 
Kuna kazi kidogo mkuu umeme utarejea soon
 
Mnasubirigi mechi kubwa ndo inaanza tu ndo mnakataga umeme..hamjui Ni maelfu ya watanzania tunakodolea macho..mnakata
 
Naomba muongozo wa namna ya kubadili matumizi ya umeme nyumbanibkutoka juu kwenda chini maana situmii umeme mwingi kwangu.
 
Umeme maeneo ya Msalato Bible Dodoma usiku wa kuamkia leo umeunguza vifaa majumbani bila shaka sababu ya high voltage. Tupatie maelekezo taratibu za kudai fidia.
 
Umeme maeneo ya Msalato Bible Dodoma usiku wa kuamkia leo umeunguza vifaa majumbani bila shaka sababu ya high voltage. Tupatie maelekezo taratibu za kudai fidia.
Fika ofisi ya endo lako mkuu utapatiwa fomu kisha uchunguzi utafanyika na kutoa taarifa ya nini kimesababisha au kimepelekea madhara hayo unayodai
 
Swali :
Mradi wa stieglers gorge ni kampuni gani imeshinda tenda?
 
Chanika maeneo ya Mvuti mtaunganisha lini umeme? Miundombinu yote tayari na watu wachache wameunganishiwa. Ni mradi wa REA.\

shukran
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…