Habari nilikua naomba kubadilishiwa matumizi nyumbani matumizi yangu niyachini lakini natumia gharama kubwa kulipia umeme.
Ukiangalia matumizi/flow ya umeme ni kama 200V au na zaidi kwa mda lakini napewa Unit chache na zinakatika kwa haraka.

Kwa matumizi ya kuwasha taa na kuchaji simu nalipa karibu 40elfu kwa mwezi. Nisaidieni kubadi matumizi ya Meter

Meter number yangu ni 37212843355
Naomba kubadilishiwa matumizi
 
Mzim
Nawasalimu kwa Jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania,kazi iendelee.

Dodoma ni makao makuu ya nchi ,ni aibu kama sehemu za mjini surveyer anapita kukagua,umeme hauweki mwezi mzima!Nawaomba ndgu zangu hii si sawa, mnakosa mapato pia hakuna ulazima.

Sehemu ya Kisasa surveyer kapita hadi sasa hakuna majibu ya lini tutawekewa umeme. Amka kazi iendelee.
 
Kwa kweli umeme kuunganishiwa kwa sasa unasumbua sana sana! Mimi nimelipia tarehe 03/6/21 mpaka leo naambiwa hakuna mita!

Sasa najiuliza kulikuwa na sababu gani mpaka ya kuniambia nikalipe wakati mita hakuna? Ni huku Kibamba,
Nimeuliza kwanini mita hakuna?

Wameniambia ni baada ya Waziri kutangaza kushusha gharama kwahiyo wahitaji wamekuwa wengi! Sasa mimi nimelipa tarehe 03/6/21 tsh 320900
hivi mnatoaje kisingizio cha kushuka kwa gharama?

Yaani hapa kwa sasa ni Rushwa ndio iliofanya waanze kuhudumiwa waliokuja kwa gharama ya tshs 27000/
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
TANESCO nimelipia toka tarehe 23.04.2021 mpaka leo majibu ambayo hayaeleweki tu...nililipa 27k REA mpaka leo mita hakuna Kigamboni...taarifa nilishakupa hapa hujawahi kutoa jibu lolote
 
Toka jana sina umeme nimetoa ripoti nikapewa namba 0146 nipo Kimara Stopova kwa kapinga.
 
TANESCO nimelipia toka tarehe 23.04.2021 mpaka leo majibu ambayo hayaeleweki tu...nililipa 27k REA mpaka leo mita hakuna Kigamboni...taarifa nilishakupa hapa hujawahi kutoa jibu lolote
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Mbona hamjibu?
 
Umeme nimefungiwa lakini kila nikitaka kulipa naambiwa meter namba haitambuliki.leo wiki ya pili sasa nashindwa kununua token. Kama hamtaki kuisajili meter mulionifungia, njooni mtoe haya majitu yenu, nisije nikayafanya kitu mbaya.
 
1.Mbona Leo Kigamboni hapa Kisiwani katika kata ya Vijibweni hakuna umeme? Hakuna sababu yoyote iliyotolewa kuhusiana na kutokuwepo kwa umeme. Umeme utarudi muda gani haijulikani.

2. Kwanini mnakata umeme kwa kujisikia bila hata taarifa? Mtaelimika lini? Hili ni tatizo la kukosa exposure. Safiri katika nchi za watu weupe huko jambo lolote au tatizo lolote must be notified. Ila kwenu nyie ni tofauti.
 
Nunua solar panels uachane na umeme wa kisiasa hutojuta bwashee
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

MKOA WA TEMEKE

TAARIFA YA KATIZO LA DHARURA-WILAYA YA KIGAMBONI

Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mkoa wa Temeke linawataarifu wateja wake wa wilaya ya Kigamboni kuwa kutakuwa na katizo la umeme la dharura kama ifuatavyo:-

Siku Ijumaa,02/07/2021(LEO)

MUDA Tutazima muda mfupi ujao, Saa 07:10 mchana na kazi itafanyika kwa dakika 20

SABABU Kufanya marekebisho ya dharura maeneo ya Mbutu Kichangani beach na kurejesha huduma ya umeme maeneo hayo.

Maeneo yatakayoathirika
Mwembemdogo, Cheka, Mbutu, Kimbiji, Pembe mnazi, Tundwi songani, baadhi ya maeneo ya Kibada Millungu, Serikali ya mtaa, Kisarawe II, Vumilia ukooni, Dar fresh, Dar zoo, Tanzania ruider, Amigo, Tecco na Mwasonga

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika toa taarifa dawati la dharura wilaya ya Kigamboni kwa msaada zaidi:
0739113311 , 0739113366

Au kituo cha miito ya simu Makao Makuu:+255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti:
www.tanesco.co.tz

Barua pepe: dm.kigamboni@tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii:

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook Kirjaudu sisään Facebookiin

Imetolewa na
Ofisi ya Uhusiano na
Huduma kwa Wateja
TANESCO Kigamboni
02/07/2021
 
Umeme nimefungiwa lakini kila nikitaka kulipa naambiwa meter namba haitambuliki.leo wiki ya pili sasa nashindwa kununua token. Kama hamtaki kuisajili meter mulionifungia, njooni mtoe haya majitu yenu, nisije nikayafanya kitu mbaya.
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya mita

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…