TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kama kuna kitu kinafanya tumkumbuke marehemu JPM ni tatizo kubwa ambalo lipo Tanesco, tatizo ni nini?
1. Baada ya waziri mpya kuteuliwa umeme unakatika kila wakati, wengine wanahisi huenda hii ni janja janja ya kutengeneza tatizo ili zabuni za umeme wa dharura zitolewe watu wapige dili, kwa kweli ndugu February ndoto zako za urais zisahau kabisa kwa utendaji huu, inatia hasira na uchungu, WHY? Iliwezekanaje miaka 6 sasa hivi ishindikane, au kuna hujuma?

2. Kubadili mfumo wa huduma kwa wateja nalo ni tatizo kubwa sana.

Shirika kubwa hivi kuwa na kitengo kimoja cha huduma kwa wateja nchi nzima ni kujidanganya, ukiIngatia utatuzi wa chngamoto unahitaji mafundi kwenda kwenye eneo husika na sio utatuzi remotely kama kampuninza simu au mabenki. Unapiga simu mtoa huduma hajui ni wapi huko unapopataja, apokee simu ya sikonge, apokee ya ndungu, apokee ya buhongwa, lazima achanganye madesa. Mfumo uliokuwepo wa kituo kuwa eneo husika ulikuwa mzuri na fanisi kwa wapata huduma kwanza wanajua maeneo na matatizo pia wanayafahamu na utatuzi wake ni rahisi. Kwa mfumo wa sasa kuapata tu hiyo fursa ya kuongea nao utapiga mara 5 au 6 na usubiri haswa....

Kwakweli tanesco mmetuweza, tunasikitika na kuumia, nawaza mkurugenzi mkuu na waziri hawaoni hizi kero au ndio watasema wapewe muda, mpaka lini???
Ufafanuzi

Tunapenda kukujulisha kuwa mfumo wa uendeshaji na utoaji wa huduma duniani unaelekeza taasisi/kampuni kuwa na njia sahihi za kupokea na kufanyia kazi taarifa za wateja kama ifuatavyo:

1.Upokeaji wa simu kwa kutumua mifumo ya kisasa ambapo simu zote zinaingia sehemu moja, mazungumzo yanarekodiwa, kazi inaingia kwenye mfumo na usimamizi wa utekelezaji wa kazi au taarifa za wateja kufanyiwa kazi kwa haraka zaidi

2.Simu zinazoingua hazipokelewi na mtu mmoja bali ni timu ya watu ambao wanatumia laini moja ya simu (0748550000) ambayo inapokelewa kupitia wapokeaji wengi kwa wakati mmoja

3.Tumeanzisha viunga maeneo mbalimbali ili kusohmgeza huduma karibu na wateja wetu. utakuwa shahidi unapoona magari au bajaji zikipitia kutoa huduma, lengo ni kusogeza huduma karibu na wananchi ambapo kila penye watu wengi timu yetu itakuwa hapo, kazi ikipokelewa inafikisha kwa timu husika kwa mfumo mara moja

Tunatambua wakati wa mabadiliko kutakuwa na changamoto za kimtazamo lakini sisi tunazipokea zote ili kuendelea kuboresha huduma

TANESCO,Tunayaangaza Maisha Yako
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Eti kwa haraka zaidi acheni uongo jipangeni upya na mkubali kusahihishwa watu tunalalama kufungiwa umeme mita tu miezi sita je wanaohitaji nguzo moja au mbili si wanalia na kusaga meno
 
Tafadhali onesha taarifa kamili tukupatia huduma au ufafanuzi, je uliandika namba gani ya simu, Wilaya? Na tatizo gani
 
Mbona mmetukatia umeme usiku huu jamani, Tabata mwananchi? Tunalalaje sasa na joto hili?
 
Leo mmeamua kuongeza umeme ili kutuunguzia vitu Mamaee zenuuuu
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Mbona mmetukatia umeme usiku huu jamani, Tabata mwananchi? Tunalalaje sasa na joto hili?
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Nipo mwanza rodi tabora kuna nguzo imegama kwa masika hii inaweza anguka na kuleta mazala no 0694484119
 
Nguzo kubwa zilizopo pembezoni mwa Barabara kwanini zisifungwe Mataa makubwa yamulike barabarani usiku? Umeme siupo wakutosha?
 
Nipo mwanza rodi tabora kuna nguzo imegama kwa masika hii inaweza anguka na kuleta mazala no 0694484119
Tunashukuru kwa taarifa tafadhali onyesha namba ya taarifa kwa wepesi wa kuifatilia nankuchukua hatua
 
Na kisarawe nako umeme shida.
Ndani ya saa moja unakatika mara nne. Ukiruri chumba cha jirani upo kwako haupo au nyumba moja upo nyingine haupo. Tatizo nini.
0762625515.
Tunashukuru kwa taarifa imepokelewa kwa hatua zaidi
 
Kuna tofauti gani kati ya huduma za T1 na T2, una utaratibu gani unatumika kumuhamisha mtu kutoka T1 kwenda T2 au T2 kwenda T1?
 
Back
Top Bottom