Umelipa TSh 6,000 kwa ajili ya LUKU, No. ya kampuni: 001002, kumbukumbu ya malipo:54205135483. Muamala: 25472915640. Salio jipya ni TSh 96. Jumla ya Makato TSh 100. (Ada TSh 0, Tozo TSh 0), VAT TSh 15. 25/01/22 21:11.
 
Tatizo ni nini Tafadhali?
 
Tunaona wastani wa matumizi yako kwa mwezi ni uleule miezi yote hivyo hakuna tatizo vinginevyo umuite fundi aliyesajiliwa kukagua muliundombinu yako ya umeme

Mkuu umesema wastani wa matumizi ya umeme uko sawa ila Mimi hapa mwenyewe nimenunua umeme wa 5000 juzi hiyo units 14 ukaisha asubuhi yake na ulivyoisha Jioni yake tena nikanunua Tena umeme wa units 11 na ndo nilioujaza ila kuamkia asubuhi Leo hii umeme umekata maana kile kiluku kidogo Cha kujazia umeme kinaonesha zero units Sasa kwann wastani wa matumizi uwe sawa ndani ya siku mbili tutumie umeme wa units 25?

Na fundi wa Tanesco tuliyempigia simu kasema shida ni MITA kubwa inabidi tuibadilishe na kuibadilisha unalipia Ela afu process zinafanyika mwezi mzima ndo anakuja kuifunga Sasa sijajua.
 
Pata elimu

Tafadhali tambua kuwa mita haili umeme bali ni matumizu ya mteja, kiasi cha matumizi ya mteja kinategemea
1.Vifaa vyake

2.Tabia za utumiaji

3.Ubora wa wiring yake

4.kutivuja kwa umeme haswa wiring iliyochakaa

Hivyo unaweza kufanya majaribio kwa kuzima kila kitu hata saa moja kisha kuangalia kama mita itaendelea kuhesabu matumizi
 
Okay hili la kuzima main switch baada ya lisaa limoja nimefanya majaribio tayari na hamna umeme uliopotea ila nikiwasha umeme ndo unaenda kwa Kasi ya ajabu
 
Okay hili la kuzima main switch baada ya lisaa limoja nimefanya majaribio tayari na hamna umeme uliopotea ila nikiwasha umeme ndo unaenda kwa Kasi ya ajabu
Wewe ni mwenzangu, tatizo letu ni moja, na nimefanya yote hayo. Umeme unakimbia kama Juma Ikangaaa.
 
Tafadhali tujulishe tatizo ni nini? Wilaya na namba ya simu kwa hatua zaidi

huwa natumia SimBanking kununua umeme
tangu ninunue umeme hadi Leo sijawahi kuupata na hela ilikatwa!

Nilinunua mara mbili kimakosa (Tsh 9,000 x 2)
ya kwanza nilipewa tokens
Ila ya pili hazijawahi kufika:
Tangu Tarehe 31 August, 2021
saa 3 usiku

Namba za Mita:
43000245977

Details zingine nimekutumia Inbox
 
Tafadhali pokea umeme wako ulionunua tarehe 31/01/2022

" 1775-9675-4469-0654-1852"

&

=" 5766-3194-0509-6091-5788"

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Tanesco Arusha- Njiro mtatuunguzia printer jamani.. unawaka unazima kwa muda mchache.
 
Okay hili la kuzima main switch baada ya lisaa limoja nimefanya majaribio tayari na hamna umeme uliopotea ila nikiwasha umeme ndo unaenda kwa Kasi ya ajabu
Tafadhali muite fundi wako wa umeme aangalie tatizo ndani ya nyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…