TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TANESCO mnakera hasa kata utatuzi ama kuwekea uzito matatizo ya wananchi. Maana halisi ya kuwa na hotline number ni kuweza kufikiwa kwa haraka pale panapokuwa na tatizo. Jana Tabata segerea umeme ulikuwa unakatawa na kurudishwa kila mara.

Mara ya mwisho kurudi nyumba yangu tu ndo ilikosa umeme na hii ni kutokana na kutoka cheche kwenye nyaya zenu zinazoingia kwenye mita. Hii ilikuwa saa kumi na mbili jioni. Baada ya kupiga hotline yenu ya eneo la Tabata (0715 768 589) wakanipa reference number (014 7) ya tatizo langu kuahidi mafundi watakuja.

Mpaka saa 3 kimya nikawapigia tena lakini napo ahadi ile ile. Kufika leo asubuhi umeme umerudi kwa nguvu kupelekea kuunguza fridge. Kuwapigia tena huyo mpokeaji anaongea kama anaelazimishwa n hatilii uzito tatizo lilipo.

Hivi mnavyochukulia wateja si haki maana mwisho wa siku sisi ndio tunaifanya kampuni yenu ifanye kazi. Na mpaka dakika hii cheche bado zinatokaTANESCO
 
Kuna meneja wilaya ya waziri mkuu ni kishoka hatari afu anapenda sana hela ukitaka kazi yako akufanyie fasta we mpe hela watu hawa mnashughulikaje nao
 
TANESCO mnakera hasa kata utatuzi ama kuwekea uzito matatizo ya wananchi. Maana halisi ya kuwa na hotline number ni kuweza kufikiwa kwa haraka pale panapokuwa na tatizo. Jana Tabata segerea umeme ulikuwa unakatawa na kurudishwa kila mara. Mara ya mwisho kurudi nyumba yangu tu ndo ilikosa umeme na hii ni kutokana na kutoka cheche kwenye nyaya zenu zinazoingia kwenye mita. Hii ilikuwa saa kumi na mbili jioni. Baada ya kupiga hotline yenu ya eneo la Tabata (0715 768 589) wakanipa reference number (014 7) ya tatizo langu kuahidi mafundi watakuja. Mpaka saa 3 kimya nikawapigia tena lakini napo ahadi ile ile. Kufika leo asubuhi umeme umerudi kwa nguvu kupelekea kuunguza fridge. Kuwapigia tena huyo mpokeaji anaongea kama anaelazimishwa n hatilii uzito tatizo lilipo. Hivi mnavyochukulia wateja si haki maana mwisho wa siku sisi ndio tunaifanya kampuni yenu ifanye kazi. Na mpaka dakika hii cheche bado zinatokaTANESCO
Tumelipokea na kama tulivyoongea tutalifanyia kazi mpendwa mteja
 
Kuna meneja wilaya ya waziri mkuu ni kishoka hatari afu anapenda sana hela ukitaka kazi yako akufanyie fasta we mpe hela watu hawa mnashughulikaje nao

Tunaomba taarifa hata kwa private message ya jina na wilaya na ushaidi wowote ule itakuwa siri
 
Tunashukuru sana hapa sasa tutapata mawasiliano kwa urahisi sana
 
Ndugu upo maeneo gani? Mtwara hii mbona huku kwingine safi labda kuna matengenezo. Au unaweza fika ofisi za tanesco upeleke malamiko.
 
Sioni msaada wenu hapa zaidi ya blabla tu
Maswali yangu yote sioni majibu
 
Naomba ufafanuzi hivi kwanini,umeme nanunua bei sawa na wanao tumia unit zaidi ya sabini kwa mwezi wakati mimi natumia unit takribani stini na mbili kwa mwezi. Wakati huohuo jirani yangu anapata unit nyingi akinunua kwa kiasi cha hela km ntakayonunua mimi, Naomba mnielimishe tafadhali
Kwenye thread yangu hii, nashukuru mliisoma na mliomba niwatumie meter namba niliwatumia lakini sijui kinachoendelea mt.No. 24217491554
 
Nilihitaji kufungiwa mita nyengine lakini mpaka sasa nazungushwa wakati nilipeleka maombi tokea mwaka jana mwezi wa pili pale Kurasini (mwaka sasa na zaidi ya miezi miwili) na mara nyingi nikienda naambiwa hawana mita na wana uhaba wa mita.

Tafadhali lifafanue hili maana mwenzangu aliomba badala yangu amepata (Sitaki kuamini kwamba alitoa rushwa)

TANESCO
 
Nilihitaji kufungiwa mita nyengine lakini mpaka sasa nazungushwa wakati nilipeleka maombi tokea mwaka jana mwezi wa pili pale Kurasini (mwaka sasa na zaidi ya miezi miwili) na mara nyingi nikienda naambiwa hawana mita na wana uhaba wa mita. Tafadhali lifafanue hili maana mwenzangu aliomba badala yangu amepata (Sitaki kuamini kwamba alitoa rushwa)

TANESCO
Tunaomba namba yako ya simu, Jina ulilolipia ili tuangalie kwenye taarifa zetu
 
Tunaomba namba yako ya simu, Jina ulilolipia ili tuangalie kwenye taarifa zetu
Taarifa zipo mara zote naenda pale wananiuliza hivyo wanacheki kisha wanasema nipo baada ya hapo ndio napewa majibu ya subiri utapigiwa simu.
 
TANESCO nawashukuruni mno nimeweza kufungiwa umeme tarehe 29/04/2017.


MUNGU awabariki muweze kusikia na kilio cha Watanzania wenzangu wengine ambao bado hamjayashughulikia matatizo yao.


Sasa nipo tariff (1).
 
TANESCO nawashukuruni mno nimeweza kufungiwa umeme tarehe 29/04/2017.


MUNGU awabariki muweze kusikia na kilio cha Watanzania wenzangu wengine ambao bado hamjayashughulikia matatizo yao.


Sasa nipo tariff (1).
Wateja wote wa mijini wanafungiwa wakiwa tarif 1 vaada ya miezi mitatu wakiwa na wastani wa matumizi ya unit 75 wanarudishwa tarif 4
 
Hii threed, nailaani kama ninavyowalaani Tanesco, maana swqli moja nimeuliza maractatu bila majibu!!!
Ukitoa taarifa zote ulizoombwa inatusaidia kukupata ufumbuzi mfano jina simu eneo mkoa na wilaya
 
Wateja wote wa mijini wanafungiwa wakiwa tarif 1 vaada ya miezi mitatu wakiwa na wastani wa matumizi ya unit 75 wanarudishwa tarif 4
Ahsante mkuu.


Tariff (1) na (4) zina tofauti gani na ni kwanini watarudishwa tariff (4)? Asante
 
Ahsante mkuu.


Tariff (1) na (4) zina tofauti gani na ni kwanini watarudishwa tariff (4)? Asante
Tarif 1 wanaotumia umeme chininya 75 unitd kwa mwezi na zaidinya hapo mpaka 7500 units ni tarif 1
 
Back
Top Bottom