Toxic Concotion
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 5,760
- 20,837
TANESCO mnakera hasa kata utatuzi ama kuwekea uzito matatizo ya wananchi. Maana halisi ya kuwa na hotline number ni kuweza kufikiwa kwa haraka pale panapokuwa na tatizo. Jana Tabata segerea umeme ulikuwa unakatawa na kurudishwa kila mara.
Mara ya mwisho kurudi nyumba yangu tu ndo ilikosa umeme na hii ni kutokana na kutoka cheche kwenye nyaya zenu zinazoingia kwenye mita. Hii ilikuwa saa kumi na mbili jioni. Baada ya kupiga hotline yenu ya eneo la Tabata (0715 768 589) wakanipa reference number (014 7) ya tatizo langu kuahidi mafundi watakuja.
Mpaka saa 3 kimya nikawapigia tena lakini napo ahadi ile ile. Kufika leo asubuhi umeme umerudi kwa nguvu kupelekea kuunguza fridge. Kuwapigia tena huyo mpokeaji anaongea kama anaelazimishwa n hatilii uzito tatizo lilipo.
Hivi mnavyochukulia wateja si haki maana mwisho wa siku sisi ndio tunaifanya kampuni yenu ifanye kazi. Na mpaka dakika hii cheche bado zinatokaTANESCO