Imekuwa Desturi kwa kampuni ya Umeme
TANESCO Branch ya Bagamoyo kutoa huduma ya Umeme ambayo si ya uhakika. Umeme umekuwa ukikatika Mara kwa Mara na huchukua muda mrefu kurudi.
Hivyo, point yangu ya msingi hamuoni kwamba mnachangia kuwafanya wanachi wa Bagamoyo kuwa Masikini? Wananchi walio wengi Bagamoyo wanategea umeme katika uzalishaji ili kujipatia kipato waweze kuishi sasa mnapokata umeme kiholela hivyo pasipo kutoa taarifa mna maana gani?
Ndugu Meneja hakika haturidhishwi na uchapa kazi wako ni mbovu haiwezekani umeme ukatike kila siku kiasi hiki. Kama huwezi kazi kaa chonjo. Tunalipa kodi za frem tunalipia leseni kila mwezi hamuoni kama tunaumia? Mnataka tufunge maduka yetu turande mitaani ndiyo mfurahi. Hakika MNAKERA sana