TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tumeipokea mkuu uchunguzi utafanyika kuthibitisha kama aloyetuhumiwa ni mfanyakazi wetu au laa ikiwemo kupitia ushahidi wako.tumeipokea kwa ufatiliaji
Tunaomba jina uliloombea na namba yako ya simu hata kwa private message
 
Nimelipia umeme hii sasa inaenda mwezi wapili na nguzo ipo ndani ya mita 30 ila sijafungiwa mpaka leo na kuna mfanyakazi wenu anaomba rushwa ya ngono ili aweze kufunga umeme kwangu tena anamuomba mke wangu na ashajulishwa na haogopi na kasema kama anataka umeme amkubalie kwanza ndio umeme uingie yupo tanesco charambe na namba yake ya simu ni hii 0712949598 na nilimrekodi maongezi yake hivi ndio utaratibu mliojiwekea hamuweki umeme bila rushwa ya ngono sasa me jumatano au alhamisi naamkia ofisini kwenu ila mjue hilo
Mpendwa mteja shauri lako bado halijafanyiwa kazi kwa kuwa bado haujatupatia namba yako ya simu ili tuweze kupata ushahidi na kufuata taratibu
 
Ni jambo la kusikitisha sana kukatika kwa umeme ijapokuwa kwa hapa Kahama imekuwa kawaida si masika wala kiangazi,umeme unakatika sana wakati wa mchana.

Leo imenishangaza kwani si kawaida kukatika umeme wakati wa sikukuu!Ni kwa nini wanatufanyia hivi hawa Tanesco Kahama?

Kama ni ukarabati wa miundombinu mbona ni kila siku wanakarabati?
 
MFUMO WA KUTUPATIA TAARIFA/LALAMIKO

1.JINA.....................................

2.SIMU....................................

3.MKOA...................................

4.WILAYA................................

5.MTAA/KIJIJI/KATA.........

6.JINSI YA KUFIKA................

7.KITU/ALAMA/MTU MAARUFU.............................

8.NAMBA YA MITA................

9.TATIZO LAKO.....................

"TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO"
 
Maana yake nn pale ninapoingiza umeme wa luku ktk mita yangu then hauingii ila kila mara itatokea error 77.Mara kibao sana nikiingiza umeme lazima nijaribu zaidi ya mara 2 hadi 10.Tatizo ni nn? Network? Ama kuna kitu nakosea?
 
Wakaaji Wa Gongo La Mboto, Majohe, Pugu kajiungeni, chanika pamoja na Maeneo mengine ya Ukanda huo ambayo ipo wilaya ya ilala yana matatizo makubwa ya kukatiwa umeme karibu kila siku ya mungu bila taarifa yoyote.

Umeme hukatwa kwa Masaa yasiyopungua Nane kila siku. Huwa tunaona ajabu sana ikitokea siku moja umeme haujakatika. Wakati Dar hii hii wenzetu wanashangaa umeme ukikatika.

Mh Rais aangalie upande huu kuna jipu linahitaji alitumbue
 
Wakaaji Wa Gongo La Mboto, Majohe, Pugu kajiungeni, chanika pamoja na Maeneo mengine ya Ukanda huo ambayo ipo wilaya ya ilala yana matatizo makubwa ya kukatiwa umeme karibu kila siku ya mungu bila taarifa yoyote. Umeme hukatwa kwa Masaa yasiyopungua Nane kila siku. Huwa tunaona ajabu sana ikitokea siku moja umeme haujakatika. Wakati Dar hii hii wenzetu wanashangaa umeme ukikatika
Mh Rais aangalie upande huu kuna jipu linahitaji alitumbue
Ni kweli kamanda, yaani hawa TANESCO ni kata kata kila dakika
 
Mpaka muda huu bado ni giza tu,usalama upo shakani maana vibaka ni wengi sana maeneo ya pugu
 
Duh

Hata Mkulu ameshasema kuna wafanyakazi wake ambao hawataki kubadilika, dawa ndio hii kuyaandika wayasome.

Poleni
 
Wakaaji Wa Gongo La Mboto, Majohe, Pugu kajiungeni, chanika pamoja na Maeneo mengine ya Ukanda huo ambayo ipo wilaya ya ilala yana matatizo makubwa ya kukatiwa umeme karibu kila siku ya mungu bila taarifa yoyote. Umeme hukatwa kwa Masaa yasiyopungua Nane kila siku. Huwa tunaona ajabu sana ikitokea siku moja umeme haujakatika. Wakati Dar hii hii wenzetu wanashangaa umeme ukikatika
Mh Rais aangalie upande huu kuna jipu linahitaji alitumbue
MFUMO WA KUTUPATIA TAARIFA/LALAMIKO

1.JINA.....................................

2.SIMU....................................

3.MKOA...................................

4.WILAYA................................

5.MTAA/KIJIJI/KATA.........

6.JINSI YA KUFIKA................

7.KITU/ALAMA/MTU MAARUFU.............................

8.NAMBA YA MITA................

9.TATIZO LAKO.....................

"TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO"
 
Msaada namna ya kusahihisha jina lililokosewa wakati wa usajili wa mita. Mfano Kennedy ikawa Kenneth
 
Ombi langu ni maboresho kwenye teknolojia ya mita za luku.

Kwamba niweze kutumia simu yangu kujaza umeme moja kwa moja bila mimi kuinuka na kwenga nje kubonyeza vitufe.

Vile vile hata kumjazia mtu alie mbali mf. Mama yangu anaishi kibiti na mie nipo Songea, ninunue umeme huku huku kwenye simu yangu na nitume moja kwa moja kwenye mita ya mama pale Kibiti.

Yeye aone tu taa zinawaka bila yeye kuinuka na kwenda kujaza.

Wakati mwingine ni usiku na umeme umeisha, mita na yenyewe ipo nje na mama pale nyumbani hana vijana wa kumsaidia.

Ombi langu ni hilo yaani mama yeye awe anaona umeme upo tu muda wote bila kupanda kwenye stuli kujaza.
 
Back
Top Bottom