TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
GARI LAGONGA NGUZO WILAYA YA ROMBO.

Shirika Umeme Tanzania (TANESCO) linawajulisha Wananchi wake wa Wilaya ya Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro kuwa kuna gari limegonga nguzo na kupelekea baadhi ya maeneo kukosa umeme leo tarehe 2 Julai 2017 eneo la Tarakea

MAENEO YANAYOATHIRIKA:-
Tarakea yote, Usseri, Longido na Kamwanga

HATUA ZILIZOCHUKULIWA
Wataalamu wa Shirika wapo eneo la tukio kuhakikisha huduma inarejea mapema iwezekanavyo.

WITO
Shirika linatoa wito kwa wateja wake kote Nchini kulinda miundombinu ikiwemo kutoa taarifa vituo vya Polisi, Ofisi za Serikali, Ofisi za TANESCO kote Nchini ili kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa.

Imetolewa na :
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
2 Julai 2017
daf8ac77c537b807e049b72d59b301e1.jpg
ea8de11e7317fc7892a7dcbc43c21c05.jpg
 
ENEO LA OYSTERBAY HATUNA UMEME KWA ZAIDI YA MASAA 10 HADI NINAPO ANDIKA MADA HII TATIZO NINI?MWENYE TAARIFA TUJUZANE WAJAMENI
NATANGULIZA SHUKRAN
 
Aiseeee!!!!
Nimeshagaa na kusikitika sana
Huwa nasimuliwa huko oysterbay ndo pakishua, leo umeme umekatika?
Kweli BONGO BAHATI MBAYA
 
Umeme sio asili yetu WATANZANIA (usiutegemee sana), jaribu kutumia nishati MBADALA.
 
*TANZANIA ELECTRIC SUPPLY COMPANY LIMITED*

*POWER INTERRUPTION NOTICE IN COAST REGION*

The Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) regrets to inform its esteemed customers in Coast Region that power supply will be interrupted as follows: -

*DATE:* On Wednesday 12nd July, 2017.

*TIME:* From 09:00 Hrs to 17:00Hrs.

*REASON:* To allow contractor M/S CYLE Engineering Solution to make Foundation
works for relocation of 33Kv Bus Coupler Circuit Breaker at Chalinze
substation for new Twyford ceramic factory feeder located Pingo area.

*AFFECTED AREAS:*
Ngerengere Line: Magwila, Mikoroshini, Nelo, Msolwa, Mdaula, Matuli, Ubena Zomozi, Bwawani, Gwata, Ngerengere, Kidugalo, Kinonko, Sangasanga, Kizuka.

Lugoba Line: Bwilingu, Bunga, Chalinze mzee, Msoga, Mboga, Lugoba, Kinzagu, Mazizi, Msata, Masuguru, Mwetemo, Bago, Kiwangwa, Kihangaiko, Wami, Mandela, Miono, Lupungwi, Makole, Kimange, Mbwewe, Changarikwa.

Please do not touch or approach broken conductor, inform TANESCO through No. 0232402386/0658560404/0787600794 or Call Centre 0768985100

Any inconveniences are highly regretted.

Issued by:
Eng. Martin Madulu
*REGIONAL MANAGER - COAST*
 
TANESCO huduma zenu kwa maeneo ya Kipunguni B ni duni mno.

Baada ya kukatika umeme jana (tukio linalojirudia mara kwa mara) uliporudi nyumba zote zilipata umeme isipokuwa ya kwangu, meta inawaka lakini umeme hauwaki. baada ya kwenda ofisini zenu za Magereza, wamekataa kata kata kunipa reference number kwa ahadi ya kuwa watakuja tu. kwa uwelewa wangu mdogo it is within my rights to get a reference number ya complain yangu lakini ushirikiano ulikuwa mdogo sana na mpaka dakika hii hakuna yeyote aliyekwenda.
Kwa kumbukumbu tu, tatizo kama hili liliwahi kutokea na nilipewa namba tu ambayo baada ya kuweka kwenye mita yangu ikafunguka.

Ila leo nahisi natengenezewa mazingira ya kupigwa pesa kutokana na ushirikiano duni niliopewa.

kama itakuwa na msaada wowote kwenu, hii ndio meter number yangu 54130476911. Namba yangu ya simu ni 0784 416 504, Kipunguni B kata ya Kivule karibu na Kipako Maburini.

Narudia tena mna haja ya kubwa ya kutazama ofisini zenu za Magereza, huduma duni sana.
 
TANESCO huduma zenu kwa maeneo ya Kipunguni B ni duni mno. Baada ya kukatika umeme jana (tukio linalojirudia mara kwa mara) uliporudi nyumba zote zilipata umeme isipokuwa ya kwangu, meta inawaka lakini umeme hauwaki. baada ya kwenda ofisini zenu za Magereza, wamekataa kata kata kunipa reference number kwa ahadi ya kuwa watakuja tu. kwa uwelewa wangu mdogo it is within my rights to get a reference number ya complain yangu lakini ushirikiano ulikuwa mdogo sana na mpaka dakika hii hakuna yeyote aliyekwenda.
Kwa kumbukumbu tu, tatizo kama hili liliwahi kutokea na nilipewa namba tu ambayo baada ya kuweka kwenye mita yangu ikafunguka. Ila leo nahisi natengenezewa mazingira ya kupigwa pesa kutokana na ushirikiano duni niliopewa.
kama itakuwa na msaada wowote kwenu, hii ndio meter number yangu 54130476911. Namba yangu ya simu ni 0784 416 504, Kipunguni B kata ya Kivule karibu na Kipako Maburini.
Narudia tena mna haja ya kubwa ya kutazama ofisini zenu za Magereza, huduma duni sana.
Tumeipokea mpendwa mteja kama ambavyo tumeonge tutaifanyia kazi
 
Shirika la Umeme Tanzania - (Tanzania Electric Supply Company Limited - TANESCO), Tunaomba mtupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri kupitia huu uzi nasi tutawajibu.

Tunawaomba mzingatie yafuatayo ili kurahisisha ufafanuzi na ufumbuzi wa tatizo au taarifa husika;

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Kw mawasiliano Kituo cha Miito ya Simu (+255) 22194400 or (+255) 768 985 100 Mitandao ya kijamii Tanescoyetu (@tanescoyetu) | Twitter Facebook: Tanesco Yetu

HAPA CHINI NI NAMBA ZA SIMU ZA MIKOA

Ofisi ya Mkoa wa Mbeya Simu ya Mkononi (+255) 757 529 380 ya Mezani (+255) 252 504 219

Ofisi ya Mkoa wa Ilala Simu ya Mkononi (+255) 784 768 586 ya Mezani (+255) 222 133 330

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) Simu ya Mkononi (+255) 715 271 461/ (+255) 784 271 461

Ofisi ya Mkoa wa Kinondoni Kaskazini (Mikocheni) Simu ya Mkononi (+255) 784 768 584 / (+255) 716 768 584 ya Mezani (+255) 222 700 367/ (+255) 222 701 602 / (+255) 222 774 098

Ofisi ya Mkoa wa Temeke Simu ya Mkononi (+255) 712 052720 / (+255) 758 880155 / (+255) 732 997361

Ofisi ya Mkoa wa Pwani Simu ya Mkononi (+255) 78 5122020 / (+255) 65 7108782ya Mezani (+255) 23 2 402 386

Ofisi ya Mkoa wa Arusha Simu ya Mkononi (+255) 75 8 174 343 Mezani (+255) 272 506 110

Ofisi ya Mkoa wa Tanga Simu ya Mkononi (+255) 658 122 412/ (+255) 687 677 667 Mezani (+255) 27 2 646 779

Ofisi ya Mkoa wa Kilimanjaro Simu ya Mkononi (+255) 765 397 925/ (+255) 682 771 310 Mezani (+255) 272 755 007/8

Ofisi ya Mkoa wa Manyara Simu ya Mkononi (+255) 689 795 599 / (+255) 75 9 534 130 Mezani (+255) 272 530 590

Ofisi ya Mkoa wa Mwanza Simu ya Mkononi (+255) 759 777 786 / (+255) 687 910 202 Mezani (+255) 282 501 060 / (+255) 282 500 090

Ofisi ya Mkoa wa Geita Simu ya Mkononi (+255) 744 085 696 Mezani (+255) 28 2520330

Ofisi ya Mkoa wa Kagera Simu ya Mkononi (+255) 78 5 787 898 / (+255) 75 3 120 701 Mezani (+255) 282 220 061

Ofisi ya Mkoa wa Mara Simu ya Mkononi (+255) 762 165 087 / (+255) 732 985 672

Ofisi ya Mkoa wa Simiyu Simu ya Mezani (+255) 282 700 180

Ofisi ya Mkoa wa Dodoma Simu ya Mkononi (+255) 782 161 643 Mezani (+255) 262 321 728

Ofisi ya Mkoa wa Morogoro Simu ya Mkononi (+255) 68 4889272 / (+255) 65 4829046 Mezani (+255) 232 613 501/2

Ofisi ya Mkoa wa Singida Simu ya Mkononi (+255) 71 4 477 445 / (+255) 732 960 924 / (+255) 689 373 757 Mezani (+255) 262 502 133

Ofisi ya Mkoa wa Tabora Simu ya Mkononi (+255) 786 558 510 / (+255) 763 162 868

Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga Simu ya Mkononi (+255) 754 521 070 Mezani (+255) 28 2762120

Ofisi ya Mkoa wa Kigoma Simu ya Mkononi (+255) 78 3720598 Mezani (+255) 28 2802668

Ofisi ya Mkoa wa Katavi Simu ya Mkononi (+255) 68 8345200

IMETOLEWA NA:- Ofisi ya Uhusiano

TANESCO Makao Makauu.

Vilevile pitia threads hizi kupata Maelezo ya ziada;


LUKU:Mfumo wenye Tija kwa Wateja na TANESCO

Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Zijue taratibu za kufuata ili kufungiwa umeme na TANESCO
 
jamani naomba kujua mwezi wa sita nimenunua umeme wa tsh.9500 nilipewa units 75 mwezi huu nimeshindwa kuelewa kabisa tarehe moja nimenunua pesa ileile tsh.9500 nikapewa units 26 naomba kuelewa tatizo ni nini niko Kagera Biharamulo
 
Back
Top Bottom