Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tunaomba namba yako ya simujamani tunahitaji kujua na majibu ya private sidhani kama ni sahihi kwa jambo la umma jibu humhumu
TANESCO MNAZINGUA NDANDA KUNA NYAYA ZA UMEME zimelala juu ya miti tena jirani na nyumba zina mwaka sasa taarifa mnazo lakin kimyaaa mpaka afe mtu ndio mlidhike sio.
Tatizo limerekebishwa na huduma imerejeaSHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA KUTOKEA HITILAFU KITUO CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME KUNDUCHI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa imetokea hitilafu katika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kunduchi majira ya Saa 8:34 Mchana.
JITIHADA ZILIZOFANYIKA
Mafundi wamefanya jitihada za kurejesha umeme katika hali ya kawaida na majira ya Saa 9:03 Alasiri hitilafu ilirekebishwa na Wateja kupata umeme isipokuwa wanaopata kupitia njia ya umeme ya TG3 na TG5.
MAENEO YANAYOKOSA UMEME NI:
Kunduchi, Mtongani, Uninio, Boko, Bahari Beach, Bunju, Madale, Wazo na Mbweni.
Tafadhali usiguse waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo:
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100
Tovuti: www.tanesco.co.tz
Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu
Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
23 Agosti 2017
TANESCO "Tunayaangaza maisha"
Hapana, Namaanisha nyaya na nguzo za umeme zimetapakaa kama uchafu karikati ya Miji.
Wapo ambao washalizwa na miamala waliorushiwa pesa IPO
Majina yao ya kitambulisho yanafanana na ya tigopesa
Sent using Jamii Forums mobile app
Tanesco wakupe units za bure??[emoji24][emoji24]kwa tanesco hilo sahau mkuu. ukienda kununua umeme mara ya kwanza hakikisha una elfu kama ishirini hivi hapo watakata deni la unit 50 na utapata unit zingine kama 6 hivi[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]TANESCO hivi mteja wenu mpya akiunganishiwa umeme anapewa unit 50 za kwanza, je hizi unit 50 ni ofa au ni deni na kama ni deni linalipwaje? Je umeme wa mwanzo ukiisha ili mteja aweze kununua au kuongeza unit anatakiwa afanyeje?
Habari mkuu!
Tanesco.mbona bado kimyaaa kuhusu swala miliosema mnafuatilia.SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA KUKOSEKANA UMEME MKOA WA TEMEKE HUSUSAN ENEO LA MBAGALA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke linaomba radhi kwa Wateja wake kutokana na kukosekana kwa umeme kutokana na hitilafu kwenye laini ya kurasini mbagala
Mafundi wako kazini ili kurekebisha hitilafu Hiyo.
Maeneo yanayoathirika ni mbagala na baadhi ya maeneo ya yombo
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano na huduma kwa Wateja
TANESCO -Temeke
16 August, 2017
TANESCO "Tunayaangaza maisha"