TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TANESCO MNAZINGUA NDANDA KUNA NYAYA ZA UMEME zimelala juu ya miti tena jirani na nyumba zina mwaka sasa taarifa mnazo lakin kimyaaa mpaka afe mtu ndio mlidhike sio.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUTOKEA HITILAFU KITUO CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME KUNDUCHI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa imetokea hitilafu katika Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kunduchi majira ya Saa 8:34 Mchana.

JITIHADA ZILIZOFANYIKA

Mafundi wamefanya jitihada za kurejesha umeme katika hali ya kawaida na majira ya Saa 9:03 Alasiri hitilafu ilirekebishwa na Wateja kupata umeme isipokuwa wanaopata kupitia njia ya umeme ya TG3 na TG5.

MAENEO YANAYOKOSA UMEME NI:
Kunduchi, Mtongani, Uninio, Boko, Bahari Beach, Bunju, Madale, Wazo na Mbweni.

Tafadhali usiguse waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo:

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
23 Agosti 2017

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
Tatizo limerekebishwa na huduma imerejea

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA UMEME MKOA WA MOROGORO

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa MOROGORO kuwa kutakuwa na katizo la Umeme siku ya Alhamisi tarehe 24.8.2017

MUDA: Saa 2:00 asubuhi- Saa 11:00 jioni.
SABABU:- Mafundi wetu watakuwa wanafanya Matengenezo katika kituo cha kupokea na kupooza umeme kihansi

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:- Chita,Mngeta,Mpaka Mchombe Pamoja na KPL.



Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka .

Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo:

Dawati la dharura Mkoa wa Morogoro
0232613501/0232613502,0654829046/0684889272
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO -MOROGORO
23/08/2017

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Tanesco naona mnachoongea na kutuaminisha ni tofauti sana na hali halisi tuionayo,Nina jirani yangu maeneo ya Ilala sambusa alikuwa anachomelea geti kisha baada ya hapo Mita ya Luku ikazima,baada ya hapo umeme akawa hapati akatoa taarifa Tanesco kwa njia ya simu,kisha akapewa namba ya taarifa yani tb 2829 ilikuwa siku ya jumatatu ya tarehe 21/8/2017,lakini tangu siku iyo wakipigiwa simu wanadai kazi yako anayofundi anakuja lakini mpaka leo ijumaa bado hawajaja sijui mpaka hapo na nyie mtatusaidiaje,ni hayo tu
 
TANESCO hivi mteja wenu mpya akiunganishiwa umeme anapewa unit 50 za kwanza, je hizi unit 50 ni ofa au ni deni na kama ni deni linalipwaje? Je umeme wa mwanzo ukiisha ili mteja aweze kununua au kuongeza unit anatakiwa afanyeje?
 
TANESCO hivi mteja wenu mpya akiunganishiwa umeme anapewa unit 50 za kwanza, je hizi unit 50 ni ofa au ni deni na kama ni deni linalipwaje? Je umeme wa mwanzo ukiisha ili mteja aweze kununua au kuongeza unit anatakiwa afanyeje?
Tanesco wakupe units za bure??[emoji24][emoji24]kwa tanesco hilo sahau mkuu. ukienda kununua umeme mara ya kwanza hakikisha una elfu kama ishirini hivi hapo watakata deni la unit 50 na utapata unit zingine kama 6 hivi[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zimepungua mwaka jana mpendwa mteja kadri hali itakavyoruhusu

Sent using Jamii Forums mobile app
Habari mkuu!


Kwa wateja wapya waliokwisha unganishiwa umeme ni baada ya muda gani au units kiasi gani ziwe zimebaki ndio waende ofisi za TANESCO kwa ajili ya kulipia zile units 50 za mwanzo na kubadilishiwa tariff?

Mimi nimebakiwa na Units 16, je naweza kwenda kununua mwingine sasa hivi na kuhamishwa tariff wakati huohuo?maana matumizi yangu kwa mwezi ni chini ya Units 75. Asante
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUKOSEKANA UMEME MKOA WA TEMEKE HUSUSAN ENEO LA MBAGALA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke linaomba radhi kwa Wateja wake kutokana na kukosekana kwa umeme kutokana na hitilafu kwenye laini ya kurasini mbagala

Mafundi wako kazini ili kurekebisha hitilafu Hiyo.

Maeneo yanayoathirika ni mbagala na baadhi ya maeneo ya yombo

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano na huduma kwa Wateja
TANESCO -Temeke

16 August, 2017

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
Tanesco.mbona bado kimyaaa kuhusu swala miliosema mnafuatilia.
Umeme ktk kijiji ambacho wao huziona nguzo kama mapambo .Njooeni mtufungie trans4mer na cc.apa kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco hebu mtufikirie na watu wa huku Tunduru maana watu tumelipia muda mrefu sana lakini majibu kila siku 'hatuna nguzo wala waya' sasa hii inakuaje?

Motorola Verizon Droid X8
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA(TANESCO)

TAARIFA YA KUTOKEA HITILAFU YA UMEME KWENYE MTAMBO WA UZALISHAJI MAJI WA RUVU CHINI-MKOA WA PWANI

Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) linawajulisha wateja wake kuwa mnamo tarehe 24/08/2017 majira ya saa 5:54 Usiku ilitokea hitilafu ya umeme kwenye transfoma inayohudumia mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu chini, Kutokana na hitilafu hiyo iliyotokea upande wa washirika wetu (DAWASCO) Shirika lilitoa wataalamu wake ili kuungana na wataalamu wa DAWASCO kutatua tatizo hilo.

MAENDELEA YA KAZI
Mpaka sasa wataalamu wamefikia hatua nzuri na shirika litaendelea kutoa taarifa kwa kila hatua itakayokuwa imefikiwa.

Kwa taarifa za huduma za TANESCO unaweza kuwasiliana na Dawati la dharura Mkoa wa Pwani 0232402386/0785122020

Kituo cha Miito ya Simu Makao Makuu
0768985100/0222194400

www.tanesco.co.tz

www.facebook/twitter.com/tanescoyetu



Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
26/08/2017

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

MATENGENEZO YA DHARURA KITUO CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME CHA KIPAWA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mikoa ya Ilala na Temeke kuwa kutakuwa na kazi ya matengenezo ya dharura katika Transfoma 90 MVA ya Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Kipawa siku ya Jumapili Agosti 27, 2017 kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 7:00 jioni hivyo kusababisha baadhi ya maeneo ya Mikoa hiyo kukosa Umeme.

MAENEO YATAKAYO ATHIRIKA:

Temeke , Chang'ombe, Sokota, Uwanja wa Taifa, Kigamboni, Viwanda vya Alaf, Camel Steel, Bakhresa, Steel Master, Vita Foam, DPI Simba, Sili Africa, Cello, TCC,Metal Product, Yeboyebo, Polisi Chang'ombe, Serengeti Breweries, Plasco, sign industry, Dar Coach

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika.

Toa taarifa kupitia namba zifuatazo:-

kituo cha miito ya simu Makao Makuu 2194400 au 0768 985100

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
Agosti 25, 2017

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Tanesco naomba mtujibu sie wakazi wa mabwepande SACCOS Viwanja vya Manispaa ya kinondoni BLOCK 14(Karibu na CHUO CHA KILIMO), Mlitutangazia mtaleta umeme wa REA February 2017 lakini mmeleta nguzo mkaacha katikati pasipo taarifa yeyote,hili swali ni General nilishatoa namba ya simu haujapiga,please jibu hapa hapa maana ni wakazi wote wa SACCOS hatuna umeme mmeweka nguzo tu tena umbali mrefu wa kama nguzo 7 hivi,mmefanya hivyo ili mtuchaji pesa?

Huo mradi wa REA ambao fedha mshapewa kwanini mmeuacha Kati? Kwanini msilete nguzo mpaka kwenye makazi ya Watu? Hapo si mnaweka mazingira ya RUSHWA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu nilikuwa nafanyanae biashara lakini sasa nimemuachia yeye aendelee, ila mwanzoni Mimi ndio nilifanya uandikishwaji pamoja na malipoyote kwaajili ya kupata luku, je anaweza kuendelea kutumia lukuhiyo kwa jinalangu.

Je kuna hasara yoyote nitakayopata kwa sababu hiyo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inasikitisha kuwa pale mnapotaka kutimiza matakwa yenu basi mko radhi kudanganya ili yenu yatimie. Siku ya Ijumaa walikuja watu wa Tanesco ofisini kwangu Pugu Road kwa madai ya kuwa wanabadili meter za zamani kuweka mpya.

Ni jambo jema na nilitoa ushirikiano. Eneo langu lina meter 3 zote za 3 phrase maana ni industrial area.

Niliuliza mara mbili mbili juu ya upatikanaji wa units baada ya kubadili na nikahakikishiwa na Mtu wa Tanesco (Jerome - 0712 830 930) kuwa Jumamosi nitaweza kununua units na Jumatatu nitaweza kuclaim units zangu (Kila meter ilikuwa na si chini ya units 2000).

Cha ajabu Jumamosi kwenda ofisi zote za Tanesco naambiwa hizo meter mpya hazipo kwenye system bado. Hii inamaanisha toka Jumamosi nalazimika kutumia Generator (si chini ya laki 6 kwa siku). Leo hii Jumatatu naambiwa yale yale kuwa siwezi kununua umeme maana sijasajiliwa.

Kosa langu ni kukubali kubadilishiwa meter ambapo kumepelekea kuingia gharama zaidi? Kwanini nidanganywe kuwa nitaweza kununua umeme siku ya pili tu ilhali si kweli? Je hizi gharama za uendashaji kwa kutumia generator kwa kosa ambalo si langu ni za haki?

Kuweni wa kweli kuzingatia na hali halisi ya kiuchumi. Mpaka dakika hii bado naendesha kazi kwa generator.
Number za meter mpya zilizobadilishwa ni
43153681812
43153688411
43153692736

Naushad
Royal Furnishers
0658427994
TANESCO
 
Back
Top Bottom