TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kuna taarifa imetumwa kwamba kumetokea hitilafu ktk Grid ya Taifa iliyopelekea umeme kukatika muda wa saa moja na dakika mbili leo asubuhi na tatizo hilo linashughulikiwa sasa wewe unayeongea sana mara CCM imefanya hivi,kwani hao walio nje ya CCM si na wao walikuwa CCM na bado matatizo haya ya umeme tulikuwa nayo. Kipindi Lowassa akiwa Waziri Mkuu alisema ataleta umeme kutoka Indonesia sijui ulikuwa ni umeme wa kuchota na ndoo lkn hatukuuona hd anatimuliwa madarakani kwa ufisadi wa RICHMOND. Sumaye huyo mlonaye ndo ziro kabisa kakaa kwenye kiti cha Uwaziri Mkuu miaka kumi kuliko Mawaziri Wakuu wote tangu Tanganyika ipate Uhuru lkn hatukuona la maana alilofanya sasa leo hii ndo ataweza kutatua matatizo ya umeme? Tujadili matatizo ni kwa namna gani tuyaondoe lkn ukiongelea chama mimi japo si mwana CCM lkn naona hakuna chama mbadala wa kuiongoza Serikali bali nawaona walioko huko upande wa pili ni makanjanja tu..!!!
matatizo hayaishi!?..kalemani alisema wiki mbili..wiki mbili zimepita linakuja tatizo lingine
 
Waziri muongo alisema kukatika umeme itakuwa historia . CCM imechokwa nchi nzima.sijuwi hawa wanaokichagua hiki chama wanatumia tochi au vibatari?
 
JPM bado amezungukwa na watu wasiowajibika,wanaojificha nyuma ya mgongo wa chama
Huu unafiki wa kuwalaumu washauri na wanaomzunguka mtekelezaji mkuu ndio umetufikisha hapa. Nchi hii miaka yote ni watu waliowazunguka viongozi ndiyo wenye matatizo lakini hao watu wameteuliwa na hao hao viongozi.
 
MAHANJU
Hili la umeme sio siri, linakera kwa kweli.Na kwa nini wasitoe taarifa kama kuna mgao,jambo ambalo liko wazi?The problem ni kwamba wanavyozidi kukaa kimya, ndivyo wananchi wanavyozidi kukereka.Ni afadhali wakawa wawazi.

Mimi sijui watendaji wa TANESCO wanafanya hivyo kwa interest ya nani.Utendaji wa aina hii umeambukiza mpaka vitengo vingine,huduma ikiwa haipatikani,watu wanakaa kimya, wananchi hawapewi taarifa, wanabaki wana-speculate.Huu sio utendaji mzuri hata kidogo.Watanzania ni lazima tubadilike.

Na hivi zile mbwembwe za Waziri Kalemani za kumuondoa Mtendaji Mkuu wa Kidatu ziliishia wapi,mbona hatuoni matunda?
 
Nimesikia BBC World Service umeme umekatika nchi nzima Tanzania.

Hapa Kazi Tu.
 
Binafsi nilipo hakuna umeme na jana usiku ulisumbua mseneo ni temeke_yombo
Coment upo au haupp
 
Chama hakina Mungu bali kina yule aliye 'kinyume na Mungu' mnatarajia nini!. Chama kimejaa siasa za chuki, wizi, uonevu, majungu, hila, ufisadi, gilba, uongo, damu nk.
 
Back
Top Bottom