TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TANESCO hivi huu mgao wa umeme siku za jumanne na jumatano kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 11 jioni huku Pugu Kajiungeni mitaa ya Mpakani ni kwa sababu gani ?
 
Tatueni tatizo la ununuaji LUKU kwa mawakala, mrudishe mtindo wa zamani kwani sasa mawakala nao wanatutoza hela yao ya kutuuzia.
 
Japo mods nimesikitika uzi wangu kuungwa na huu mimi ilikuwa ni maombi yangu kwa MH Rais sio taarifa kwa Tanesco maana kama ni taarifa tumepiga sana namba yao lakini hili swala ni MH Rais ndiye mkombozi aliyebaki kwetu sisi tunaenda na sera ya Tanzania ya viwanda
 
Habari wanabodi.

Naandika uzi huu nikijua fika Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli si mwanachama wa mtandao huu lakini naimani atauona au kuambiwa na watu wake.

Mh Rais tunakumbuka kuwa hapo awali Tanesco walitengeneza mgao feki ili baadhi ya wakuu wapige pesa ni wewe peels ndiye uliyelifichua hili na kusitisha mgao.

Mh Rais napenda kukufahamisha kuwa mgao ule Tanesco wameurudisha tena kwa siri. Mkuu mgao huu una athari kubwa hasa kwa sisi ambao tunatekeleza sera yako ya HAPA KAZI TU tukitumia VIWANDA vidogo ili tuifikishe nchi yetu katika uchumi wa Kati.

Mh Rais kinachoendelea Tanesco kwa sasa ni kuhujumu juhudi zako katika kuleta maendeleo ndani ya nchi yetu.

Huku kwetu Ilala (tabata) umeme unakatwa mchana kutwa unarudishwa jioni hauishii hapo usiku unakuwa unakatwa na kurudishwa muda mwingine unarudi kwa nguvu mfano hai ni jana usiku 23/10/2018 majira ya saa tano umeme ulionhezwa nguvu hali hii itasababisha short na uharibifu wa mitambo na vifaa vyetu vya umeme.
Mh Rais ikiwa ni majuzi tu katika moja na speeches ulisema umeme wetu una gharama kubwa sio rafiki kwa wenye viwanda. Sasa wanakata kabisa tutumie majenereta Je mkuu hawa watu wana lengo la kujenga au kuharibu.

Mh Rais katika hili swala ni wewe pekee wa kuwa mkombozi wetu kama ulivyofanya kipindi kile cha mgao nchi nzima au Tanesco waweke wazi sababu za mgao huu lakini vinginevyo kuna hujuma ndani ya Shirika la Umeme.

Nimatumaini yangu kuwa hii itakufikia Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Habari za sahizi mpendwa mteja wetu
Tunakuomba radhi sana wewe pamoja na wateja wetu kwa hayo uliyosema.tunaomba utujulishe ni eneo gani haswa na namba yako ya simi tafadhali
 
Japo mods nimesikitika uzi wangu kuungwa na huu mimi ilikuwa ni maombi yangu kwa MH Rais sio taarifa kwa Tanesco maana kama ni taarifa tumepiga sana namba yao lakini hili swala ni MH Rais ndiye mkombozi aliyebaki kwetu sisi tunaenda na sera ya Tanzania ya viwanda
Tutakupatia mrejesho mpendwa mteja wetu
 
Habari za sahizi mpendwa mteja wetu
Tunakuomba radhi sana wewe pamoja na wateja wetu kwa hayo uliyosema.tunaomba utujulishe ni eneo gani haswa na namba yako ya simi tafadhali
*TAARIFA KUHUSU HALI YA UMEME ENEO LINALOLALAMIKIWA*

Ndugu wapendwa wateja wetu

Tunapenda kuwajulisha kuwa hakuna mgawo unaoendelea Ila kuna Uboreshaji wa upatikanaji wa umeme kwenye kituo chetu cha Kipawa.Kazi hii inahusisha uvutaji wa njia nyingine ya umeme ya Msongo wa 132kv kutoka ubungo kwenda kipawa.Zoezi hili lilianza tarehe 18/9/2018 na litaisha 7/11/2018.

Matangazo yaliyotolewa kwa wateja wetu.Tunajitahidi wakati mwingine kupata njia mbadala wakati mwingine ili wateja waweze kupata umeme wakati wa mchana ambapo inatulazimu kurejesha katika hali ya kawaida wakati wa usiku.

Tunawaomba radhi sana wapendwa wateja wetu kwani kazi hii imelenga kuboresha upatikanaji na ubora wa umeme.

*TANESCO*
 
Habari wakuu, Leo nimeshtuka sana Mara baada ya kununua umeme, units nilizopewa Leo ni tofauti kabisa na kipindi cha nyuma ,Bei ya umeme imepandA?
 
Hakuna badiliko lolote la bei mpendwa mteja wetu
 
Habari za sahizi mpendwa mteja wetu
Tunakuomba radhi sana wewe pamoja na wateja wetu kwa hayo uliyosema.tunaomba utujulishe ni eneo gani haswa na namba yako ya simi tafadhali

Ninaishi Tabata mawenzi kwakweli kama ni vifaa vimeungua na kila siku umeme lazima ukatwe [emoji17][emoji17]
 
Nasikitika kuona ubungo kibangu ambapo ni nyuma tuu ya offisi za tanesco ubungo kuona umeme unakatika kila siku.. Hii ni nyumba niliyo amia miez 4 sasa ..lakini nalazimika kuhama kabla ya mkataba kuisha kwasababu ya umeme kukata kata ovyo..

Mimi ni naendesha shughuli zangu kupitia youtube chanel na ndo inaniweka mjini. Kutokana na tatizo la umeme kukatika mara kwa mara..mnanifanya nishindwe kuripot matukio mda husika

Ajali ya MV NYERERE Sikutoa taarifa mda muhafaka kwaiyo mukanikosesha viwers

Kupatikana kwa mo pia umeme ulikatika nimekuja kupata taarifa saa 3 asubuhi baada ya umeme kurudi,,kumbe taarifa za za kupatikana zilianza kusambaa saa 8 usiku

Kukata kwenu umeme munanikosesha mambo mengi
Kesho ndio nahama rasmi hii sehemu
 
Mna shida gani? Mchana mmekata siku nzimu, sasa hivi npo mnakata. Mbona mnaoenda kukera? Kwanini msibinafsishe kama mmeshindwa kutoa huduma?
 
Ndugu mpendwa mteja ni matumaini yetu kuwa uliona hali ya hewa ilivyokuwa hata hivyo hatua stahili zimechukuliwa
 
Nasikitika kuona ubungo kibangu ambapo ni nyuma tuu ya offisi za tanesco ubungo kuona umeme unakatika kila siku.. Hii ni nyumba niliyo amia miez 4 sasa ..lakini nalazimika kuhama kabla ya mkataba kuisha kwasababu ya umeme kukata kata ovyo..

Mimi ni naendesha shughuli zangu kupitia youtube chanel na ndo inaniweka mjini. Kutokana na tatizo la umeme kukatika mara kwa mara..mnanifanya nishindwe kuripot matukio mda husika

Ajali ya MV NYERERE Sikutoa taarifa mda muhafaka kwaiyo mukanikosesha viwers

Kupatikana kwa mo pia umeme ulikatika nimekuja kupata taarifa saa 3 asubuhi baada ya umeme kurudi,,kumbe taarifa za za kupatikana zilianza kusambaa saa 8 usiku

Kukata kwenu umeme munanikosesha mambo mengi
Kesho ndio nahama rasmi hii sehemu
Pole sana umeme unaweza kukatika kwa sababu mbalimbali moja ikiwemo hali ya hewa kama ulivyoona upepo mkali ukivuma hivyo tunaomba radhi na uwe unatupatia taarifa mapema zaidi
 
Leo nilipita ofisini kwenu kurasini DSM kitengo cha procurement nimeonana na mdada mmoja akaniambia yupp field kutoka TIA DSM mid namfahamu ni MTU was TISS na kabla ya kuja hapo kwenu alikuwa bandari najua akimaliza kazi take mtatafutana hapo kama sisi kula bandari NASA haha charisma tu muwe makini
 
Back
Top Bottom