TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Hii document ni valid!?

Ni kwanini watendaji wa Tanesco wilayan hawatekelezi hili tangu tarehe ya maelekezo?
 
Toka asubuhi hatuna umeme wakati jana tu mlitusumbua na ma luku yenu
 
Ni jambo la kushangaza sana! Ni kweli kabisa hayo maeneno yamejengeka lakini hakuna umeme. Unaenda vijijini, sehemu nyingine nyaya zinaenda hata umbali wa mita 400 bila kuwepo nyumba, lakini umeme upo. Mwanza nyumba kwenye hayo maeneno, zipo karibu karibu sana lakini umeme hakuna.

Watu walio mbali na Mwanza, wengi wanaamini marehemu aliipendelea Mwanza, lakini ukweli ni kwamba hakuna cha pekee. Barabara za lami ni za kuhesabu. Barabara ya njia moja ni moja tu ya kilometa 4, mitaani barabara nyingi mashimo matupu, umeme maeneo mengi ya pemebezoni mwa jiji, haujapelekwa.
Mkuu watu wanaamini hivyo kuwa Mwanza aliipendelea kutoka na matamshi yake: "Mwanza sita bomoa nyumba zao kwa sababu walinipigia KURA ila hao wa KIMARA/MBEZI nitabomoa bila fidia pamoja na kesi yso Mahakamani
 
Nikweli Bei ya kuingizia umeme mijini imeshuka Hadi 27000?
MKuu sio mjini tu, hata huko vijijini. Kama ulipitwa na awamu ya kwanza ya REA, basi bei ya TANESCO (300,000/- + ) INAKUHUSU.
Namhurumia na Mh. Waziri wa Nishati, japokuwa anachapa kazi kwelikweli.
 
TANESCO makao makuu,ninaendelea kuwapa taarifa za Kimara mwisho,na nadhani tatizo linakuwa kubwa maana jana nilitembelea maeneo hadi ya Kinondoni nikakuta nako hakuna umeme.

Jpili mlikata umeme. Jnne mlikata mara mbili. Jana mchana mlikata umeme. Usiku mmekata mara mbili na asubuhi saa 11 mmekata hadi muda huu wa saa mbili hamjarudisha.

Hebu angalia trend hii ya ukatikaji umeme Kimara mwisho halafu uniambie ni jambo gani utamueleza mteja akakuelewa.

Hebu vaeni viatu vyetu sisi watanzania tunaoishi Kimara halafu uniambie, miaka nenda miaka rudi ni kitu gani kinachokushinda TANESCO Kimara mwisho ambacho unakiweza maeneo mengine.

Kwanini umeme Dar es salaam hautulii kwa muda mrefu bila matatizo haya?Mnapata faida gani kukata umeme hovyo hovyo hivi tena kwa, miaka mingi now?
 
Leo ni tarehe 28/05/2021.
Kimara mwisho line ile ile ya dawasco nnayoizungumzia kila mara humu inaexperience jambo lile lile miezi nenda miezi rudi,miaka nenda miaka rudi.
TANESCO hebu angalia frequency ya hizi taarifa zangu za kila wiki humu uone tatizo la kukatika umeme mara kwa mara lilivyo kubwa Kimara mwisho.
Kwanini kwingineko mmeweza kutuliza umeme,Kimara panawashinda nini?!
Hapo juu it was last week i came here complaining ukanijibu hivyo.
Leo nimekuja tena nakueleza Kimara mwisho mlikata umeme asubuhi saa 12 mkarudisha saa 2.Saa hizi jioni hii mmekata tena.
Wewe unayeninibu embu angalia hii feequency ya report zangu za kila wiki humu uniambie ni kwanini Kimara hapaishi tatizo hili.
Mimi nimeamua kukusaidia.Ntaripoti kila mara umeme unavyokatika ili huko makao makuu mjue kinachoendelea Kimara mwisho.
Hizi taarifa zangu kuhusu Kimara mwisho.Kila wiki nakuja na taarifa kama hizi.Na bado tatizo linaendelea.

Hapa leo tarehe 10 June 2021.Hakuna umeme almost usiku mzima na asubuhi hii haupo.
 
Kwani kuna tatizo gani tena kwenye mfumo wa ununuaji umeme kwa njia ya simu?Mfano tigopesa,M-PESA n.k.Toka jana huduma haipatikani
 
Kwakweli kama mkazi wa Dar naamini hatujazoea kabisa hali hii ya kukatika umeme kila baada ya robo saa! Mbaya zaidi unakatika hovyo hovyo bila taarifa na mpaka sasa umeshaniunguzia friji yangu.

Kwakweli haya mambo mbona hatukuyaona enzi za utawala uliopita?

Je Tanesco wanahujumu nchi? Hali hii inakera sana! Mbaya hakuna yeyote anayechukuliwa hatua na wanaona ni sawa tu kwakuwa hakuna anayeweza kuwagusa! Nasema Tanesco tangu juzi sijaingiza hela kwa umeme wenu wa hovyo! Mbaya zaidi mmeniunguzia friji langu! Mlaaniwe!
 
Umeme umerudi saa tatu kamili,saa tatu na nusu umekatika tena.Kimara mwisho hii.Ntaendelea kuripoti hata kama ni mwaka mzima ntaandika hapa hadi hili tatizo la Kimara lishughulikiwe.
 
Kwakweli kama mkazi wa Dar naamini hatujazoea kabisa hali hii ya kukatika umeme kila baada ya robo saa! Mbaya zaidi unakatika hovyo hovyo bila taarifa na mpaka sasa umeshaniunguzia friji yangu.Kwakweli haya mambo mbona hatukuyaona enzi za utawala uliopita? Je Tanesco wanahujumu nchi? Hali hii inakera sana! Mbaya hakuna yeyote anayechu...
Daaaa Rais ajiuzulu ? Tukuchague wewe basi, ukikatika tena ukiwa wewe Rais tukufanyeje?
 
Kwakweli kama mkazi wa Dar naamini hatujazoea kabisa hali hii ya kukatika umeme kila baada ya robo saa! Mbaya zaidi unakatika hovyo hovyo bila taarifa na mpaka sasa umeshaniunguzia friji yangu...
Karibu Songwe. Umeme 24/7 elfu kumi unapata units 321.8
 
Kwakweli kama mkazi wa Dar naamini hatujazoea kabisa hali hii ya kukatika umeme kila baada ya robo saa! Mbaya zaidi unakatika hovyo hovyo bila taarifa na mpaka sasa umeshaniunguzia friji yangu...
Ajiuzuru sababu friji yako imeungua?
 
Back
Top Bottom