TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tanesco,
Huku Uyui, Tabora ...Kata ya Goweko na Nsololo umeme umekatika toka juzi 18 saa tatu usiku hadi leo hakuna umeme. Umerudishwa masaa kama matano tu usiku wa kuamkia leo na sasa umekatwa tena.

Mbaya zaidi hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kwa wananchi.
Tunaomba msaada
 
Tanesco,
Huku Uyui, Tabora ...Kata ya Goweko na Nsololo umeme umekatika toka juzi 18 saa tatu usiku hadi leo hakuna umeme. Umerudishwa masaa kama matano tu usiku wa kuamkia leo na sasa umekatwa tena.
Mbaya zaidi hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kwa wananchi.
Tunaomba msaada
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Hivi mhandisi wenu wilaya ya kilombero mji mdogo ifakara hii huwa haoni au taarifa hana? Hizi nyaya pamoja kuwa na maganda ya plastic lakini bado ni hatari hasa kwa watoto.
20210720_082209.jpg
 
Kuna mpangaji wangu wa Duka aliweka umeme hadi meter kwa Gharama zake, Leo amewaleta mafundi kuundoa, Mpangaji kakorofishana na mkewe, hivyo anasema anatoa umeme wake Dukani. Je ni sahihi?

Umeme huu si ni mali ya Tanesco na alikiutoa si ni serikali itakayokosa mapato, maana mimi mwenyewe Nimekuwa nikilipa Bill, kutokana na frame iliyopo hapo jirani.
 
Kuna mpangaji wangu wa Duka aliweka umeme hadi meter kwa Gharama zake, Leo amewaleta mafundi kuundoa,Mpangaji kakorofishana na mkewe, hivyo anasema anatoa umeme wake Dukani. Je ni sahihi?. Umeme huu si ni mali ya Tanesco na alikiutoa si ni serikali itakayokosa mapato, maana mimi mwenyewe Nimekuwa nikilipa Bill, kutokana na frame iliyopo hapo jirani
Mteja haruhisiwi kufanya chochote kuanzia kwenye miga kwenda nje
 
Mita namba ni 24218159168
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
TANESCO kibaha mnafeli sana, surveyor amefika eneo langu, kapima kanambia nitatumiwa control no. Mpaka leo ananizungusha tu nikimuuliza anasema wanasubiri maelekezo nahisi ni hii 27, 000 inawavuruga.

Foleni inazidi kuwa kubwa hapa huduma si tutapata mwakani kweli.
Ni vyema mkawa na jibu la wazi kuhusu hili jambo kuliko kuleta siasa
 
Mimi naomba Tanesco mkoa wa Iringa wawasaidie wakazi walipo Igingilanyi uwanja wa ndege ambao walihamishwa upande wa pili wa barabara kuna nyumba nyingi zimejengwa lakini Tanesco Iringa hawajachangamka kuwawekea nguzo na huduma ya umeme.

Sasa hivi nyumba nyingi za kisasa zimejengwa upande ule lakini Tanesco ni kama hawaoni na wengine walikuwa na huduma hiyo kabla ya kuhamishwa lakini sasa wako gizani.

Idadi ya wanaotumia umeme pale Igingilanyi ni wachache sana na ni wale waliopo pembeni ya barabara kuelekea Dodoma lakini wengi waliopo pembeni hawana huduma.

Naomba Tanesco Iringa waende pale Igingilanyi wafanye survey ya nyumba zinazohitaji umeme na kuanza kusambaza nguzo ili wananchi wapate huduma na wao kuongeza kipato na wateja
 
Mimi naomba Tanesco mkoa wa Iringa wawasaidie wakazi walipo Igingilanyi uwanja wa ndege ambao walihamishwa upande wa pili wa barabara kuna nyumba nyingi zimejengwa lakini Tanesco Iringa hawajachangamka kuwawekea nguzo na huduma ya umeme. Sasa hivi nyumba nyingi za kisasa zimejengwa upande ule lakini Tanesco ni kama hawaoni na wengine walikuwa na huduma hiyo kabla ya kuhamishwa lakini sasa wako gizani. Idadi ya wanaotumia umeme pale Igingilanyi ni wachache sana na ni wale waliopo pembeni ya barabara kuelekea Dodoma lakini wengi waliopo pembeni hawana huduma. Naomba Tanesco Iringa waende pale Igingilanyi wafanye survey ya nyumba zinazohitaji umeme na kuanza kusambaza nguzo ili wananchi wapate huduma na wao kuongeza kipato na wateja
Ahsante tumepokea taarifa
 
Tanesco ni moja kati ya mashirika ya ovyo sana.. NIMEMALIZA
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
TANESCO Ule umeme tulio nunua kipindi kile ukawa ukiingiza huwingii mpaka leo mjaturejeshea munamaanagani 50,000/= kubwa sana
 
Fvck you guyz nilikuwa na appointment usiku huu hapa buza mmekata umeme mpaka saiv haujarudi appointment imevunjika

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom