TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Huku Arusha baadhi ya maeneo ya vibandani morombo hamna umeme tangu jana mchana na wala hata taarifa hamtoi tujue tatizo ni nini na tujue tunajihami vipi 😡
 
Chang'ombe, temeke mtaa wa mabembeani line mojawapo haina umeme tokea jana
 
Nyumba hii imejegwa huku nyaya za umeme zimepita chini ya paa, pamoja na jitihada za kutoa taarifa kwa Tanesco mara kadhaa kabla ya jengo hilo kupauliwa naa baada hakauna mfanyakazi wa Tanesco amefika hapo.

Nyumba ipo Dodoma Changombe juu, mnarani

IMG-20211230-WA0024.jpg
 
View attachment 2062698
Tafadhali onesha namba ya simu kwa wepesi wa kufatilia taarifa hii
 
Changanyikeni Kisiwani njia ya kwenda Kanisa la AICT umeme haupo tangu jana usiku. Walituambia mafundi wanashughulikia lakini uliporufu ni nyumba chache tu ndio walipata umeme.

Leo saa 5 asubuhi ulirejea lakini ilipofika saa 9 alasiri ulikatika tena hadi sasa haujarejea.

Ibrahimu
0787377511
 
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi tafadhali
 
Tatizo la kwanza.
Msongola, Ilala.
Eneo: Yatima, Tank la Maji.
Tatizo: Umeme umekatika tangu jana muda wa saa 2 usiku mpaka sasa haujarudi. Ni nyumba chache tu ambazo zimeathirika ikiwa ni pamoja na kituo cha watoto yatima Msongola (Msongola Orphanage Centre).

Tatizo la Pili.
Huu ni ukumbusho wa mwisho, nisiposhughulikiwa nakuja kumuona meneja wa Gongolamboto, nisiposhughulikiwa naenda Mahakamani kutafuta haki yangu.

Mafundi wenu Tanesco wamepitisha waya wa umeme kwenye paa langu na ndani ya uzio wa makazi yangu na hivyo kuhatarisha maisha ya familia yangu.

Namshukuru meneja alituma mtu kwa jina Mahmoud kuja kufanya analysis ya tatizo na picha akapiga, lkn since that day, it's been more than two months hakuna hatua yoyote ya kuhamisha nguzo iliyochukuliwa.

Kesho ijumaa nakuja Tanesco gongolamboto kuonana na meneja, as the last attempt to amicably find a solution for this. Nitafika popote, kwenye hili.
 
Mkuu niangalizie hii ilitokea vp..wapangaji wanataka kunilipisha..hiyo 6000 ilikatwa kwa deni lipi?
IMG-20211231-WA0000.jpg
 
Mkuu niangalizie hii ilitokea vp..wapangaji wanataka kunilipisha..hiyo 6000 ilikatwa kwa deni lipi?View attachment 2063867
Tafadhali tambua kuwa haya ni makato ya kodi ya majengo kwa muda wa miezi sita yaani Tsh 1000 kwa mwezi, wapo waliokatwa mapema kuanzia mwezi wa nane wengine wameendela kukatwa kutokana na uhakiki unaoendelea.
 
Ok poa...itabidi niwalipe hiyo 6k yao
 
TANESCO
Pale Manzese kwenye Kona ya kuingia serikali za mtaa wa Mvuleni kuna transformer yenu inabutuka butuka mara kwa mara.
Hatari iliyopo ni kwamba chini yake kuna mchoma kuku na kioski Cha vilevi vya bei rahisi na watahadharisha kuna siku italeta maafa
Mnashindwa Nini kuiambia serikali ya mtaa iwaondoe ilihali mafundi wenu wakija kutengeneza wanawaomba walevi wawapishe kidogo halafu warejee?
 
Leo siku ya pili huku eneo la Mgeni nani Mbagala hatuna Umeme nyumba 5 tuu! tumepiga simu 0748 550 000 tunajibiwa mafundi wanafatilia tatizo letu.

Mpaka saa hizi toka jana hatujaona fundi wala dalili ya umeme kurudishwa. Kupitia jukwa hili tunaomba tatizo letu lipatiwe ufumbuzi usiku huu.
 
Leo siku ya pili huku eneo la Mgeni nani Mbagala hatuna Umeme nyumba 5 tuu! tumepiga simu 0748 550 000 tunajibiwa mafundi wanafatilia tatizo letu. Mpaka saa hizi toka jana hatujaona fundi wala dalili ya umeme kurudishwa. Kupitia jukwa hili tunaomba tatizo letu lipatiwe ufumbuzi usiku huu.
Tafadhali onesha namba ya simu na namba ya taarifa kwa wepesi wa kufanyia kazi taarifa zako
 
TANESCO
Pale Manzese kwenye Kona ya kuingia serikali za mtaa wa Mvuleni kuna transformer yenu inabutuka butuka mara kwa mara.
Hatari iliyopo ni kwamba chini yake kuna mchoma kuku na kioski Cha vilevi vya bei rahisi na watahadharisha kuna siku italeta maafa
Mnashindwa Nini kuiambia serikali ya mtaa iwaondoe ilihali mafundi wenu wakija kutengeneza wanawaomba walevi wawapishe kidogo halafu warejee?
Tafadhali onesha namba ya simu na namba ya taarifa kwa wepesi wa kufanyia kazi taarifa zak
 
Back
Top Bottom