TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tatizo la Umeme Wilaya ya Mvomero
Katika siku hizi za karibuni kumekuwa na tatizo kubwa sana la kukatika kwa umeme Wilaya ya Mvomero.Sijui sehemu zingine,ni kero,ni kero, ni kero.Ni kama kuna mgao hivi, na kuna mtoto mdogo somewhere anayechezea switch.

Tukiuliza mamlaka husika ya Wilaya tunaambiwa sababu ni kwamba line ya Wilaya ya Mvomero ni ndefu sana na inapita kwenye mapori,kwa hiyo kufuatilia faults ni vigumu sana.Really?Sasa tutaendelea hivi mpaka lini?Frankly sababu hii does not hold water,na inaelekea kuna uzembe wa kiutendaji.

Tunachojiuliza ni kwambaa, hapo nyuma matatizo kama haya yalipotokea tuliambiwa ni uchakavu wa miundobinu,swala la urefu wa laini halikuwepo.Sasa line imerefuka ghafla?So tuamini this time around shida sio miundombinu shida ni urefu wa laini tu?

Lakini kama tatizo kweli ni urefu wa lainii,why now,tena usiku, mchana ni kama tatizo halipo hivi.Laini imerefuka ghafla?Anyway kama tatizo kweli ni urefu wa laini,igawanyeni sehemu mbili basi, ili iwe na Mameneja wawili,mmoja akae Mgeta na mmoja akae Turiani,ili tatizo la urefu wa laini liishe,kusiwe na visingizio vya kiuzembe.

Hata hivyo nimalizie kwa kusema kwa ukubwa wa Wilaya ya Mvomero,it is advisable to have two Nanagers.By the way you should have thought about this a long time ago.
 
Habari. Naomba kujua inakuwaje watu wanajenga majengo chini ya nyaya za umeme mkali bila kuchuliwa hatua zozote?

Nimeona haya maeneo mengi lakini lililonitisha nikuona mpaka shule nayo imejngwa chini ya nyaya za umeme wa msongo mkubwa. Hapo Dsm nimeona shule moja ya msingi pale Mbezi Msuguli inaitwa Gift Skillful imejengwa chini ya nyaya za umeme mkali kitu ambacho no hatari kwa usalama wa maisha ya binadamu na mali

Nimeona pia Iringa pale Luxury Bar opposite na ofisi kuu ya CCM wamejenga mpaka wakaijengea nguzo ya umeme ndani ya nyumba kiasi kwamba mafundi wa tanesco wakitaka kufanya matengezo wanalazimika kupanda juu ya mapaa ya nyumba. Je nyaya zikikatika au shot ikitokea itakuwaje?

Nimetoa visa hivyo vuwili lakini kuna maeneo mengine pia hali kama hizi zipo. Naomba wamiliki wasione kuwa nawachongea lengo langu ni kuepusha madhara. Tususubiri hadi madhara yatokee ndipo hatua zichukuliwe
 

Attachments

  • IMG-20240926-WA0212.jpg
    IMG-20240926-WA0212.jpg
    51.8 KB · Views: 14
  • IMG-20240926-WA0211.jpg
    IMG-20240926-WA0211.jpg
    39.9 KB · Views: 16
Tanesco turudishieni umeme huku kinondoni kata ya msisiri mnakazi ya kuzima na kuwasha mnaboa nyie watu
 
Ndio kusema tariff 4 ile ya kupata unit 75 kwa shilingi 9500 kwa mwezi imeshaondolewa au sielewi maana nimeunga umeme wa tsh 10500 ila nimepata units 25 badala ya units 75

Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Katika watu ninaowaombea dua baya katika dunia hii basi ni TANESCO halafu anafata Shetani. Nyie jamaa ni ndugu wa baba na mama mmoja.
Mkoa wa Songwe hasa Halmashauribya mji Tunduma huku umeme ukikaa nao hata dakika tano basi umshukuru Mungu na mizimu ya kwenu.
Kila sekunde mnakata umeme na kurejesha, umeme ukirudi useme uwashe tv yako hata haijamaliza kujiandika maandishi mnkata. Tunakaa dakika kumi tena mbele mnawasha, badaa ya dakika mnakata.
Na hii ninkuanzia asubuhi hadi kesho asubuhi, shida yenu ni nini haswa?
Siku hili shirika likifa Wallah nitachinja kuku banda zima kama kafara ya shukran.
 
TANESCO mambo yamewashinda hawa yani mnashinda bila umeme na kulala giza na huna wa kumuuliza wala taarifa zozote wananchi hawapati, ukirudishwa umeme ndani ya dakika 10 umekatika mara 2.

Huduma gani hii TANESCO .?
 
Habar shirika mm ni mteja wenu nilitaka uduma ya kuhunganishiwa umeme nikafanya process zote na paliitaj nguzo pale kwang lkn nguzo wameleta wameiyacha chini kwa sasa wanawiki mbili toka waiyache cjaelewa shida nn toka mwez wa nane nimelipa kila kitu lkn akuna umeme na vitu vyangu vinazid kualibika napatikana mkoa wa dar es salaam wilaya ya temeke kata ya chamanzi kitongoj cha saku njia panda ndogo namb ya cm ambayo nimeombea maombi 0712284087
Namb yangu 0684878935
 
TANESCO TANESCO TANESCO nimewaita mara tatu, nyaya zenu zimeteremka chini kama mnavyoona kwenye video. Nimewapigia simu wiki mbili zimepita ila naona kimya hamjafika kurekebisha.
Location: Magomeni Tanga.
 
Tanesco

Habari.
Tunaomba mtafte njia mbadala ya kulinda miti yetu mti hukua kwa miaka 30 mpaka 30 nyie mnakuja siku moja mnakata miti njia nzima mnatuharibia sana angalieni njia nyingine hasa pitisheni umeme chini ya ardhi hata mambo ya nguzo ni ya kizamani.
 
Habarini jamani,mna changamoto moja,mita yangu ni mpya ndio mara ya kwanza naweka umeme ila haungii,nikiweka inaniandikia reject naomba utatuzi.Asante
 
salute.Tanesco mkoa wa Dar es salaam mnakata umeme bila taarifa Kuna mna mkatata na kurudisha mfululizo yaani ni kama mtoto anachezea switch kiukweli mnakela Kuna watu wanafanya biashara za samaki wabichi nyama saloon sasa mnavyokata na kurudisha toeni taarifa face book ni Bure kwann msiseme kesho tutakata sehem flani na kurudisha mda flani lkn utakuta umeme siku nzima hamna Kwa mfano Jana siku nzima umeme hamna na hakuna taarifa jamani mlioko huko TANESCO fanyeni kazi kama wasomi kama Kuna matengenezo toa taarifa page za Facebook ni Bure tu zinawafikia walengwa yaani mbaka DAWASA wanawashinda Kwa utendaji wa kazi maji yakikata mara moja taarifa unapata lakini TANESCO wanaweza kukata umeme siku hata mbili husikii taarifa yoyote mameneja wa Tanesco mjitafakari mnaendesha shirika kizamani nadhani Kuna haja ya kupata mshindani kutoka private company kiukweli mnaboa sana over.

TANESCO
 
Mimi nilinunua umeme wa shilingi 14,000 kwenye mita ya zamani namba 04167568379 nikapata unit 19 lakini mita ilikuwa inatakiwa kubadilishwa na hivyo umeme haukuingia. Nikabadilishiwa mita mpya namba 43524416005 nikaambiwa nijaze fomu kuomba nirudishiwe hizo unit. Mpaka leo ni miezi mitatu sijapata unit hizo. Naomba msaada wako, Tanesco Africana wanaboa sana ndugu.
 
Baada ya Ku apply kwenye Nikonekt app nini kinafuata? Inachukua mda gani surveyor kufika saiti
 
Tanesco Tanzania hivi kweli nyie binaadamu ama majini mnamaana gani kutukatia umeme asubuhi hii kinondoni kata ya msisiri muda wa watu kujiandaa kwenda makazini turudishieni umeme tafadhalini
 
Leo ni siku ya tatu ilipofika saa 3 asubuhi TANESCO wamekata umeme bila taarifa yoyote !
Hali hii imetokea pia jana na juzi .Jana umeme ulirudi saa 2 usiku na majuzi umeme ulikatwa asubuhi ya saa 2 ukarudi karibu saa 4 usiku !
Swali: TANESCO kwa nini mnafanya hivi ?
Je bwawa la mwl.Nyerere la nini kama sasa ??
TANESCO MJITAFAKARI
 
TANESCO narudia tena, Walipeni hawa Ndugu Stahiki zao au mnataka kufanya Malipo Bwana akisha watwaa kama ilivyotokea pale sub-station kwa Baadhi ya waliokuwa wanadai na kama hamna Fedha ya kulipa waambieni Wananchi ukweli.

Maeneo yametengwa tangu 2018

Uthamini umefanyika 2021

Uhakiki umefanyika 2023

Disclosure mmefanya 2024 na Uongo juu kwamba Malipo ni Mwezi wa 8.

Yaani zaidi ya Miaka 6 mmewazuia watu kutumia ardhi Yao lakini Fedha ya Fidia hamtaki kulipa.

Hivi mngekuwa nyinyi na familia zetu mngefurahi?.

Wakati mnatwaa haya maeneo VIWANJA pale MSALATO vilikuwa vinauzwa 2,000,000= sasa hivi ni zaidi ya 12,000,000.

Walipeni wenzenu ili wakaanze Maisha upya siyo mnakaa ofisini ili kuwachonganisha Wananchi na Serikali Yao.

DETAILS
MKOA: DODOMA
WILAYA: DODOMA JIJI
KATA: MSALATO
MRADI: 220 KV RING CIRCUIT
MWENYE MRADI: TANESCO
Naomba niwakumbushe tena juu ya hili Jambo.
TANESCO narudia tena, Walipeni hawa Ndugu Stahiki zao au mnataka kufanya Malipo Bwana akisha watwaa kama ilivyotokea pale sub-station kwa Baadhi ya waliokuwa wanadai na kama hamna Fedha ya kulipa waambieni Wananchi ukweli.

Maeneo yametengwa tangu 2018

Uthamini umefanyika 2021

Uhakiki umefanyika 2023

Disclosure mmefanya 2024 na Uongo juu kwamba Malipo ni Mwezi wa 8.

Yaani zaidi ya Miaka 6 mmewazuia watu kutumia ardhi Yao lakini Fedha ya Fidia hamtaki kulipa.

Hivi mngekuwa nyinyi na familia zetu mngefurahi?.

Wakati mnatwaa haya maeneo VIWANJA pale MSALATO vilikuwa vinauzwa 2,000,000= sasa hivi ni zaidi ya 12,000,000.

Walipeni wenzenu ili wakaanze Maisha upya siyo mnakaa ofisini ili kuwachonganisha Wananchi na Serikali Yao.

DETAILS
MKOA: DODOMA
WILAYA: DODOMA JIJI
KATA: MSALATO
MRADI: 220 KV RING CIRCUIT
MWENYE MRADI: TANESCO
Naomba niwakumbushe tena TANESCO juu ya hili Jambo màana watu wanateseka sana.
Fanyeni uungwana kwa kuwalipa watu madai Yao ili wakasake maisha Mengine au kama hamna fungu la kulipa Rudisheni Ardhi kwa Wananchi ili ikatumike kwa Uzalishaji.

Hawa Wananchi mmewaumiza na kuiponda mioyo Yao vya kutosha sasa.

Semeni yatosha kwa kuwalipa Wananchi stahiki zao.
 
Back
Top Bottom