TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kuna tatizo nyumbani kwangu MBAGALA NZASA KWA MWARABU MTAA WA ATALANTA H/NO 10 .

MITA NO 24210335501 imegoma kununua umeme leo ni siku ya Pili.

Walipita mafundi wa Tanesco kiasi miezi miwili imepita na kuahidi kuibadilisha lkn hawakubadilisha NAOMBA msaada.
 
Mita namba zinazoanzia 24210 zimesha expire haziwezi Tena kununua umeme wala kupokea token hivyo wasiliana na TANESCO Mahalia waje wakubadilishie mita
 
Mita namba zinazoanzia 24210 zimesha expire haziwezi Tena kununua umeme wala kupokea token hivyo wasiliana na TANESCO Mahalia waje wakubadilishie mita
Niko mkoani Morogoro nimemtuma mtu, amekwenda kutoa taarifa mara mbili na leo amekwenda tena. Wanapokea taarifa HAKUNA mrejesho.

Nb: waliwahi kupita pale na walimkuta binti yangu ambaye aliniunganisha nao wakanieleza wanataka kubadilisha hizo mita nikawapa ruhusa lkn waliondoka bila kubadilisha yapata kama miezi 3 sasa iliyopita.
 
Kubadilishiwa mita iliyopitwa na wakati inachukua muda gani? Baada ya kutoa taarifa.
 
three phase bei ya unit ni kubwa sana na kusababisha factor ya umeme kuwa na mchango mkubwa kwenye kukuza bei ya product
 
TANESCO mnafanya kazi nzuri na hongereni, lakini Kuna mambo yanashangaza kweli, Milani Morogoro, kata ya Mkundi, mtaa wa mawasiliano, mumeleta umeme, a couple of weeks, wateja wengi wamehitaji umeme, ajabu wamefikishiwa wachache tu kwa madai kwamba "NGUZO HAZIPO" yaani watu wa block Moja, wapo tayari kulipia huduma then Tanesco hauna NGUZO?

Inafikirisha sana kwamba, pamoja na miti mingiiii tuliyo nayo, bado tunakosa NGUZO???? Wakati huo huo, Kuna sera mpya 2024-2034 inataka watu tuache kupikia mkaa, ikiwa nishati ya umeme inashindwa kufikisha kwa wananchi kwa Wakati, naachaje kutumia mkaa?

Tumeomba umeme tangu 2022, ndo tumeletewa NGUZO Leo, na bado kati ya watu 130 tuliohitaji, eti wamefikishiwa huduma watu 24 tu, are we really serious???? TANESCO
 
Kuna shida ya umeme wakati wa mchana umeme unakuwa mdogo kiasi kwamba baadhi ya mashine zinashindwa kuwaka , hata fridge tu mchana hazipoozi zinashindwa kuwaka na tatizo hili limekuwa kubwa
 
Nyie kenge mna maana gani kutukatia umeme na joto hili la dar?
Hebu rejesheni umeme haraka kabla hatujalaumiana, shubaamit.
 
Tanesco tunawaomba mturudishie umeme huku kinondoni kata ya msisiri jamani joto ni kali mnooooooooo mnawezaje kutukatia umeme na joto hili
 
TANESCO mnafanya kazi nzuri na hongereni, lakini Kuna mambo yanashangaza kweli, Milani Morogoro, kata ya Mkundi, mtaa wa mawasiliano, mumeleta umeme, a couple of weeks, wateja wengi wamehitaji umeme, ajabu wamefikishiwa wachache tu kwa madai kwamba "NGUZO HAZIPO" yaani watu wa block Moja, wapo tayari kulipia huduma then Tanesco hauna NGUZO?

Inafikirisha sana kwamba, pamoja na miti mingiiii tuliyo nayo, bado tunakosa NGUZO???? Wakati huo huo, Kuna sera mpya 2024-2034 inataka watu tuache kupikia mkaa, ikiwa nishati ya umeme inashindwa kufikisha kwa wananchi kwa Wakati, naachaje kutumia mkaa?

Tumeomba umeme tangu 2022, ndo tumeletewa NGUZO Leo, na bado kati ya watu 130 tuliohitaji, eti wamefikishiwa huduma watu 24 tu, are we really serious???? TANESCO
Jibu hilo la nguzo hamna lipo kila sehemu na hii ndiyo chakula yao. Wape hela (rushwa), nguzo unapata siku hiyohiyo. Najua TANESCO mtakanusha ila naweza kuwathibitishia tuweke dau niwakamatishe za takukuru.
 
Ni kama miezi 4 hivi kila siku tanesco haipiti siku bila kukata umeme walau kwa masaa 2 shida ni nini?
 
Mbona unaandika kama unakimbizwa mkuu?

Kwanini usiweke eneo unaloishi at least kata au Wilaya ili usaidike haraka?
 
Kero : TANESCO. Nimenunua umeme tarehe 30/11/2024 Jumamosi, nikaipata unit 73.7 kabla ya kuziweka nilikuwa na units 345. badala ya kuongezeka na kufika 418.7 zilikuwa 117.6. Nilipiga simu huduma kwa wateja nikaambiwa litashughulikiwa, baada ya muda mfupi ilikuja meseji kuniarifu kuwa tatizo limeisha, kuangalia remote bado units zilikuwa hazijarudi. Niliendelea kufuatilia 01/12/2024 Jumapili nikapewa risiti na.7595249 na kuambiwa kuwa nitapigiwa na mafundi wa Mkoa wangu wa Geita. Tangu Tarehe 30/11/2024 Hadi leo 2/12/2024 ninapoandika hawajanitafuta na shida bado IPO palepale. Leo Jumatatu asubuhi nimepiga simu nimepewa ahadi zilezile. Nimeendelea kufuatilia nikapewa risiti 7613810 lakini bado sijafikiwa na fundi wala kupiga simu. Hili tatizo lilijitokeza mwezi Jana vilevile nilipoweka umeme. lakini baada ya kuripoti walilishughulikia juu kwa juu likaisha units zikarudi. Ninaitwa DIDAS JOSEPH, nipo Mkoa wa Geita, Wilaya ya Geita, Mji Mdogo Katoro, Kata Ludete, karibu na Ofisi ya Mwenyekiti wa Kitongoji Kaldonia. simu 0673364534. Naomba nirudishiwe units zangu shida iishe
 
Labda itakuwa wanafanya jitihada za kuzuia zile megawatts 2115 za Bwawa la Nyerere zisije zikaingilia ghafla bin vuu ule mfumo wa zamani, halafu ikaongeza msongo wa umeme utakaopelekea kuzidi nguvu na kuharibu vyombo vya umeme majumbani, maofisini na viwandani, bila kusahau treni yetu mpya ya SGR?
 
Tunataka kujua kitu pale jumba bovuuuu

"TANESCO hataki kusema ukweli kuwa analipwa mshahara mkubwa Serikalini na Malupulupu manono kila saa na siku nzima" - Muda wote ni Kazi ya TANESCO tu
Au tuanze kwenye hizo kazi za TANESCO anahitaji watu wa aina/tabia gani kufanya nae kazi sana sana!?
👑 Upole au Ukali
👑 Ukarimu au Ukatili
👑 Muoga au Jasiri
👑Wanaocheka au Wanaonuna
👑 Wenye Ndugu au Wasio na Ndugu
👑Wenye Fedha au Masikini
👑WafanyaBiashara au Wafanyakazi
👑 Uvivu au Uchapakazi
👑 Kufuata utaratibu uliopo au Kufuata utaratibu utakaokuja
👑Wafugaji au Wakulima
👑Wanaopenda Dini au Wapagani
👑Wanaopenda Starehe au Wasiopenda Starehe
👑Wabunifu au Wasio wabunifu
👑Wasomi au wasiosoma
Hivyo yaani
Yesu ulipigwa sijui walilidhika na ukweli uliowapa

images (3).jpeg
 
Qhsante TANESCO leo, nimepata huduma ya Mita mpya baada ya ile ya zamani kuondolewa katika mfumo.

Nimew3kewa UNIT 10. naomba maelekezo maana kila nikijaribu kununua umeme kwa sasa HAUKUBALI.
 
Umeme huku kwetu Toangoma TEMEKE Dar Es Salaam Umekatika Usiku wa SAA 10 Arfajiri ya Leo 4/12/2024
na Mpaka Muda Huu SAA 11.50 Haujarudi.
Shida Nini? Wakati mna jinadi Umeme Unazalishwa wa Kutosha Mpaka upo wa Ziada? Au Hamtakosa Sababu? Najua Mtasema Miundombinu?
 
Nyie kenge mna maana gani kutukatia umeme na joto hili la dar?
Hebu rejesheni umeme haraka kabla hatujalaumiana, shubaamit.
Natamani niungane na wewe, ila wao wameshika mpini viziwi na bubu wa shida zetu
 
Qhsante TANESCO leo, nimepata huduma ya Mita mpya baada ya ile ya zamani kuondolewa katika mfumo.

Nimew3kewa UNIT 10. naomba maelekezo maana kila nikijaribu kununua umeme kwa sasa HAUKUBALI.
Weka umeme kama wa 30,000 au 20000 maana hizo unit 10 umekopeshwa so jnatakiwa ulipe then uongeze zaidi
 
Back
Top Bottom