Nilifikiri suala la Tanesco ni maeneo flani tu kumbe lila pembe ya nchi hii shida ni zilezile. Leo nipo Wilaya ya Songea, hatuna umeme toka jana majira ya saa 2 hivi ni karibu kata kama mbili hivi, ukipiga Emergency wanakuambia mafundi wapo wanafuatilia ila sema hii mvua inawasumbua.
Hivi mimi nataka niulize hii ni kwa sababu ya technology duni au uzembe wa watu tu? Inawezekanaje watu wakae na giza karibu masaa 24 kwa sababu tu ya uzembe wa mtu au watu wachache? Tanesco jirekebishe jamani hamuoni kwamba ni kero kubwa kulaumiwa kila kona?