Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Hii watu humu wanajua basi? Wabongo kusoma ni wavivu wanajua siasa pekee
 

Sawa kama kwenye mikeka si unasema kuna kula na kuliwa; sawa nae huyu bwana vifaraga took a chance lakini kakamatwa ,hivyo apewe adhabu ya faini lakini kuviharibu vifaraga kama ni vizima itakuwa hasara kwa nchi!!! Mpigeni faini alafu muacheni akuze vifaranga vyake alafu alipe kodi stahiki!!
 
Naona jamaa anarudi kwenye umaskini kama utani. Why asipigwe tu fine then aachiwe? Au viuzwe kwa nusu bei kwa wafugaji? Ila viliingiaje Dar na vimetoka Kenya?
 
Tuwe wakweli na wawazi je huyu aliyeingiza hao vifaranga nchini hajui kwamba kuna mambo ya kufuata kabla ya kuviingiza au anaipima serikali? Ningekuwa Mimi ningemuamuru arudishe alipo watoa halafu sheria inachukua mkondo wake
 
Jamani si watugaie kama samaki wa Magufuli. Wanachoma moto tena? Sasa huko ni kuadhibu viumbe wasio na hatia, sasa Kosa la vifaranga liko wapi hapo.?
 
Vimewakosea nini
 
Sheria ni msumeno kama katenda kosa na inajulikana wazi basi aadhibiwe kadri ya makosa asionewe wala kupendelewa...
 
Kama sheria inasema hivyo wavichome tu ili liwefundisho kwa hao wanaingiza vifaranga bila kibali.
Nadhani hao wanaoingiza vifaranga ndio wachomwe vifaranga hapo ni innocent creatures. Lakini pia sioni sababu kwa nini tuwachome na tusitaifishe wawekwe quarantine kama hawana magonjwa wauzwe kwa mnada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…