Tanzania kuchoma tena vifaranga kutoka Kenya?

Ni Hivii:-

Wakenya wana dharau sana, wanaleta vifaranga vyao vya Kenchic lakini wewe ukipeleka bidhaa yoyote kwao labda Tanchic, Kilacha n.k hawanunui

Hata baada ya Magufuli kukataa maziwa ya Brookside, Tanga fresh wakaanza kuzalisha products za kutosha

Sasa wanamwona kama Mama Samia Suluhu ni Mdhaifu dhaifu wanaingiza bidhaa bila kufuata taratibu, bila ruhusa

Wakenya wanatuonaga kama sisi wajinga wajinga flani hivi. Wakomeshwe waache dharau

Sasahivi wataanza kufurika kutafuta ajira huku wakati kule kwao Wabongo hawaajiriwi at all.
 
Huu ufala ukome
 
Wewe unajua wanayotufanyia Watanzania?

Jamaa wanafikiri mama atakuwa mtetemko tu, kwanini waingize vifaranga bila ruhusa?
 
Hivi nyie wabongo mkipeleka bidhaa zenu bila kulipia wakenya wao hufanya nini? Na swala la mahindi vipi!

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Hii itakuwa ni mara ya pili Serikali ya Awamu ya Tano inafanya ukatili wa kutisha dhidi ya wanyama, kweli Wizara ya Mifugo haina wataalam wa kushauri namna ya kuokoa maisha ya vifaranga kwa kuvitaifisha na kuviuza kwa wateja wa aliye viingiza nchini? Vifaranga aina hiyo vinafugwa ndani bila kutoka nje kuzagaa ovyo kwa hiyo ni rahisi kuvifuatilia na kucheki afya zao mara kuwa mara mpaka watakapochinjwa kupunguza utapiamulo uliokithiri. Kuna tofauti gani kati ya vifaranga hivyo na wahamiaji haramu wanaokamatwa mara kwa mara na kupelekwa Mahakamani na kufungwa au kurudishwa kwao kwa gharama za Serikali yetu? Mikono ya Serikali hii imejaa damu, acheni waishi!
 
Zinateketezwagwa Ng'ombe sembuse Vifaranga?
Wacha kutuletea ujinga wako hapa, hakuna ng'ombe hai anateketezwa na moto bali ni nyama ya ng'ombe au mnyama yeyote aliyekufa mwenyewe au amechinjwa lakini nyama yake imegundulika haifai kuliwa na Binadamu. Machinjioni kila mnyama anayechinjwa kwa chakula nyama yake lazima ipimwe na mtaalamu ili kujua kama ni mzimà wa afya na salama kuliwa na Binadamu na ikikutwa haifai kabisa inatekelezwa au kama ugonjwa siyo mbaya sana inachemshwa hapohapo kwa usimamizi wa aliyepima.
 
Yaani huu ujinga unatokea TENA mara ya pili.
Kwanini UUE NAFSI ZISIZO NA HATIA?
 
Apigwe faini tu,aendelee na biashara yake.
Ni mambo ya ajabu kabisa wakaua hao kuku Then Wanafaidika nini?
Wakiongea na aliyewaleta wangeelewana tu na angewapa chao.
 
Vifaranga vimewafanya nyingi hadi wavichome, hiyo sheria ya kijinga ibadilishwe haraka.
 
Vifaranga hawana hatia, aadhibiwe mhusika, vifaranga wapimwe kujiridhisha kama wanafaa kuwepo nchini au warejeshwe walikotoka, kuna amri ya Mungu isemayo "usiue"
Vifaranga Vipime Afya. Kama ni wazima Wananchi wagawiwe bure au Wauziwe. Tuache ugomvi na Jirani kila Mwaka. Tunawakera Jirani zetu Kwa kuteketeza bidhaa toka Nchi Yao.
 
Akipigwa faini atarudia tena na tena. Dawa ni kumaliza kimtaji chake
 
Wengine hatuli hata nyama kwakuwa tunavaa uhusika, fikiria ng'ombe, mbuzi, kuku, kondoo wanavyohangaika mioyo wakiona wenzao wanachinjwa, au hata binadamu akichinjwa na gari
Unakula mbogamboga nazo viumbe vilivyokatwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…