Themagufulianz
JF-Expert Member
- Apr 15, 2017
- 4,548
- 1,988
Kwa akili yako enzi za mwendazake, ukwepaji kodi ulikuwa hakuna? Hayo madudu ya bandari alikuwa hayupo?! Ni suala la muda tu huyu mama akiamua kweli afunue kote mlikokuwa mmefunikwa mtamuona huyo meko kumbe alikuwa hata zaidi ya JK!! Hizo ndege kila siku alikuwa anawaambia ni ma faida tu??
Msitake kupotosha maana ya "kuuwa Walipa Kodi".
Huyo Muagizaji hakujua hatua anazopaswa kufuata au alifanya kusudi, au alihonga?.
Yeye kama alijaribu zali basi avune alichopanda,
acha ushamba dogo!!Wacha kutuletea ujinga wako hapa, hakuna ng'ombe hai anateketezwa na moto bali ni nyama ya ng'ombe au mnyama yeyote aliyekufa mwenyewe au amechinjwa lakini nyama yake imegundulika haifai kuliwa na Binadamu. Machinjioni kila mnyama anayechinjwa kwa chakula nyama yake lazima ipimwe na mtaalamu ili kujua kama ni mzimà wa afya na salama kuliwa na Binadamu na ikikutwa haifai kabisa inatekelezwa au kama ugonjwa siyo mbaya sana inachemshwa hapohapo kwa usimamizi wa aliyepima.
Hapo sawa umetoa suluhisho jema na sio kuvichoma motoTuwe wakweli na wawazi je huyu aliyeingiza hao vifaranga nchini hajui kwamba kuna mambo ya kufuata kabla ya kuviingiza au anaipima serikali? Ningekuwa Mimi ningemuamuru arudishe alipo watoa halafu sheria inachukua mkondo wake
Mkuu wanavyofanya wanawapa sumu kwanza kabla ya kuteketezwa kwa motoHaki za wanyama ziko wapi.
Ha ha ha,kafa sasa.mkomeKama sheria inasema hivyo wavichome tu ili liwefundisho kwa hao wanaingiza vifaranga bila kibali.
Roho mbaya ni dalili ya umaskiniSheria ifate mkondo wake, hii mambo ya double standards katika kutoa adhabu haitakiwi.
Hata yeye alipokuwa anafanya hilo alijua kuwa anaweza kukamatwa mchezo ukaisha. Ila still alibeti na mkeka ushalost! Sheria zinavunjwa na watu wanaozijua kabisa ila tamaa ndio huponza watu. Afanyiwe anachostahili.
Haina tofauti sana na tunaobeti kwenye michezo kama mpira, basket n.k tunaelewa kama kuna kula na kuliwa so tunakuwaga Neutral.
Kama sheria inasema hivyo wavichome tu ili liwefundisho kwa hao wanaingiza vifaranga bila kibali.
Endeleeni kuvichoma,majibu watayapokea wafanyabiashara wa mahindi.Vifaranga kutoka nchini Kenya vyenye thamani ya Milioni 40 vimekamatwa na mamlaka ya serekali Tanzania bila ya kuwa na vibali halali. Kwa kujibu wa taarifa toka mamlaka husika Tanzania wamesema wataviteketezwa kwa mujibu wa sheria inavyotaka.
Japo vifaranga hivyo havijathibitika kuwa na magonjwa ila kwa kua vimeingia bila kibali vitachomwa moto.
Source; ITV
Gari inasambaza magonjwa kama kuku?huwa yanaumwa kideri au mdondo kama kuku?Mbona wakikamata magari hawayachomi moto wanataifusha?
Tunacoma milion 40 huku tukiendelea kutafuta walipa kodi wapya!
Hii ndio Tanzania. Kumbuka swala la yule mbwa aliyeitwa ImmigrationVifaranga hawana hatia, aadhibiwe mhusika, vifaranga wapimwe kujiridhisha kama wanafaa kuwepo nchini au warejeshwe walikotoka, kuna amri ya Mungu isemayo "usiue"
Mzimu wa Magufuli unatuandamaTaarifa ya Habari ya ITV ya leo imeonesha mfanyabiasha wa Ukonga aliyeingiza vifaranga vyenye thamani ya milioni 40 kutoka Kenya bila kufuata utaratibu.
Hatua zinazotakiwa kuchukuliwa kulingana na sheria ni kubinafsisha mali na kuteketeza vifaranga wote kwa mujibu wa sheria.
Je, kipi bora kumuita mfanyabiasha ukampiga faini pia akalipia gharama za kuhakiki usalama wa vifaranga(kwa afya ya binadamu) alafu umrudishie vifaranga? Au ukateketeza mtaji au fedha milioni 40?