Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Afukuzwe tu maana hafai kabisa
 
Hii ni ishara tosha hata mikataba wanayo tusainia nchi za nje huwa tunapigwa yote, kama mkataba na kampuni za ndani zinawaingiza chaka na Je za mabeberu wataweza.

Pengo la kukosa upinzani bungeni ndo linatumiza zaidi sbb nileteeeni Gwajimaaaaa
Hatari sn
 
Usiweke maneno mengi leta takwimu za bei kwa nchi zinazotuzunguka,usilalamike tu
 
Hata huyu mpango hafai aisee na bado anasisitiza trillion mbili bila kuangalia Hali halisi yeye akiwa waziri wa fedha kaua uchumi aisee, kwani enzi za kikwete yeye alikuwa anafanyaje maana hawa wazee wa task force kutumia nguvu kwenye kukusanya Kodi bila mazingira halisi kumeua uchumi na maelfu ya biashara kufungwa
 
Uyu waziri Hamna kitu kabisa.alichoongea na kinachotokea tofauti kabisa.aje atuambie kwanini amutudanganya.
Ni bora angewaacha watuibie.
 
Hongera Mimi nilikuwa natumia Airtel ya chuo wamefuta hyo Sasa gb 1 elfu tatu loh, awamu ya wanyonge si mchezo hela hamna ila kila kitu kinapandishwa juu
Ndio kulimia meno kwenyewe huku.

Lakini wamasemaga katika nchi zote za EAC tz pekee ndio yenye bei rahisi za vifurushi
 

Ndiyo maana Mola akatuepusha nae tu.
 
Mwendazake mwenyewe hayupo duniani katuachia msala sisi aisee, hawa viingozi wawe wanafikiria na sisi raia aisee
 
Rest in peace night bando halotel wameondoa aiseee zile muvi sijui Nita download vipi ?!
 
Watapoona mapato kutoka makampuni ya simu yameshuka, waturudi kurekebisha hizi bei bila kuombwa ingawa watatumia kisingizio cha serikali sikivu.
Nalijua hilo,ila mpaka ifikie hatua hiyo baadhi ya vijana watakuwa wamejua nafasi yao katika jamii.
 
Naomba huu uzi uwe maalumu kwa ajili ya kuhamasisha kila mdau na kila mwenye mapenzi mema kususia huu uharamia wa ndugulile na waliomtuma.

Sisi ndio walaji wa vifurushi. Tunaweza kuamua kununua, kususa au kuacha.

Sisi ndio tunaoshikilia roho ya haya makampuni uchwara yanayoendeshwa kihuni na kienyeji kwa siasa za kubangaiza bangaiza.

Tukiamua kususia haya makampuni kwa wiki japo mbili tu, wanaweza kupata hasara isiyoweza kulipika wala kurudishwa.

Natoa wito kwa kila mmoja, kwa mitandao yote ya kijamii na kwa vyombo vyote vya habari kuhamasisha kususia haya makampuni kwa muda endelevu mpaka pale watakapotambua thamani ya kuwa na nidhamu ya biashara.

Hii kampeni ya kususia haya makampuni ifanywe kwa nguvu zote kila kona ya nchi hii kwa muda endelevu usiojulikana ukomo wake.

Sisi ndio walaji. Wasitubabaishe.

Lazima tuelezane ukweli kwamba, wewe ndugulile ni mtu mwovu.

Unapenyeza mikakati miovu na conspiracy za kuzima sauti za watu kupitia mgongo wa mitandao.

Hatuwezi kuwa watumwa wa conspiracies. We are free people in a free country.

Tuwajibishane.
 
Si mnakataa kwamba nyie siyo wanyonge sasa mwalalamika!!
 
Ni ngumu kususa!

Lakini si mnasema SERIKALI ipo kusaidia wananchi wake!

Mitano tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…