Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Kuna siku mtakumbuka uzuri wa magufuli,hata kama hamtasema,magufuli alikuwa hataki ujinga,leo hii gharama za vifurushi vimepanda kuholela tu,angekuwepo magu,ndugulile ingekula kwake,
Kama huelewi kaa kimya mkuu. Huu mchongo ulibuniwa na kupangwa na jiwe siku nyingi nyuma, na tukajulishwa kuwa utekelezaji ni April 2021.

Wewe hukupokeaga msg kukutaarifu?
 
Kuna jamaa hapa kajichanganya kwenye kununua vifurushi kashangaa kapewa mb tu wakati simu yake Wala sio smartphone
Hivi vifurushi havijakaa kirafiki kabisa
Nilikuwa nateleza Sana na Univ Off Airtel sasahivi hakipo
 
Wakuu,

Kama kweli tunaamini katika uhuru wa mawazo kama haki ya kikatiba, na kama kweli tunaamini katika uwajibikaji wa viongozi, basi naomba huyu waziri Ndugulile asome ninayoandika kama jinsi yalivyo.

Wewe waziri Ndugulile, waziri mwenye dhamana kwa niaba ya serikali; una akili timamu!?

Nauliza swali? Unazo zilizotimia?

Hivi, zile mbwembwe zote za kujigamba na kujitutumua kwamba mtahakikisha vifurushi vinakuwa vya bei nafuu, ndio matokeo yake haya tunayoyaona hapa?

Yaani wewe waziri, unaweza kuwafanya watanzania milioni zaidi ya sitini kuwa ni wapumbavu na mbumbumbu?

Ukakimbia kwenda kujitungia kanuni haramu na za kitapeli ili kuhalalisha wizi?

Ulisikia wapi dunia ya leo, data zinakuwa ghali namna hii?

Katika nyakati za utandawazi ambapo maisha yote yanategemea digital devices, kwanini ufanye uhuni wa namna hii?

Sifahamu lengo ni nini? ama ni mbinu za kubinya watu wasipate access ya mtandao?

Ndugulile, nikueleze tu kwamba, maisha ya watanzania wengi hayazunguki kwenye muhimili wa siasa pekee.

Kama lengo ni kuwabinya watu kisiasa, basi hilo ni lengo mfu lisilo na uhalisia.

Mitandao ndio maisha yetu, ndio chakula chetu na kipato chetu. Tusivurugane.

Tunahitaji vifurushi vishuke bei. TAFADHALI
Kumlaumu waziri uhusika tunafanya makosa,unafikiri hayo maamuzi hayana baraka ya juu huko?

Kumbuka tupo awamu ya sita.
 
Kama huelewi kaa kimya mkuu. Huu mchongo ulibuniwa na kupangwa na jiwe siku nyingi nyuma, na tukajulishwa kuwa utekelezaji ni April 2021.

Wewe hukupokeaga msg kukutaarifu?
Hayati hayupo.

Aliyekuwepo sasa akuwepo mwanzo?

Tupo awamu ya sita usisahau kijana.
 
Tigo tanzania baba la maajabu Wanafatilia comment zenu taratibu
Kabla ajaangusha BOM la atomic hapo kesho kutwa mapema

Kwa mujibu wa chini ya kapeti
Wapo kwenye kikao cha dharura na VODA
kabla hawajaja na maajabu yao ya vifurushi FUNGA KAZI
Ambapo tutalia na kusaga meno
Nimeangalia voda weee, sioni kifurushi chochote chenye akili.
Bora kdg Airtel, ingawa siku hizi mtandao wao ni shida kusikilizana
 
Mimi nipo pamoja na makampuni, Susa peke yako. Ninaomba gharama ziongezeke zaidi ya hapa. Humu mitandaoni Kuna wajinga wengi Sana
Sema hivi watanzania wengi wajinga
Na ndio CCM wanapenda hivyo.
Miaka mingi CCM walitaka watu wajue kusoma na kuandika.
Mpaka Nyerere anatoka madarakani University moja wanafunzi 2000.waliatamba eti tunaongoza kusoma na kuandika afrika bila ujuzi wowote.
Makampuni yameweka Kodi waliyoongezewa ungana na Ndungulile.
Mungu aitwe mungu anatupenda
Mengi yangetuandama.
 
Hii ndio ilikuwa sera ya Magufuli katika akuhakikisha mitandao ya kijamii watu washindwe kuitumia, maana alishasema anatamani malaika washuke wafungie mitandao.
Utakuwa na chuki binafsi na hayati, mheshimiwa ametangulia mbele ya haki.

Naomba tuzingatie na tusisahau tupo kwenye awamu ya sita.
 
Wakuu,

Kama kweli tunaamini katika uhuru wa mawazo kama haki ya kikatiba, na kama kweli tunaamini katika uwajibikaji wa viongozi, basi naomba huyu waziri Ndugulile asome ninayoandika kama jinsi yalivyo.

Wewe waziri Ndugulile, waziri mwenye dhamana kwa niaba ya serikali; una akili timamu!?

Nauliza swali? Unazo zilizotimia?

Hivi, zile mbwembwe zote za kujigamba na kujitutumua kwamba mtahakikisha vifurushi vinakuwa vya bei nafuu, ndio matokeo yake haya tunayoyaona hapa?

Yaani wewe waziri, unaweza kuwafanya watanzania milioni zaidi ya sitini kuwa ni wapumbavu na mbumbumbu?

Ukakimbia kwenda kujitungia kanuni haramu na za kitapeli ili kuhalalisha wizi?

Ulisikia wapi dunia ya leo, data zinakuwa ghali namna hii?

Katika nyakati za utandawazi ambapo maisha yote yanategemea digital devices, kwanini ufanye uhuni wa namna hii?

Sifahamu lengo ni nini? ama ni mbinu za kubinya watu wasipate access ya mtandao?

Ndugulile, nikueleze tu kwamba, maisha ya watanzania wengi hayazunguki kwenye muhimili wa siasa pekee.

Kama lengo ni kuwabinya watu kisiasa, basi hilo ni lengo mfu lisilo na uhalisia.

Mitandao ndio maisha yetu, ndio chakula chetu na kipato chetu. Tusivurugane.

Tunahitaji vifurushi vishuke bei. TAFADHALI.
Usishangae wakipaza sauti kwenye media kwamba "Tanzania ndio ina vifurushi nafuu kuliko nchi zote duniani!!" Kana kwamba tunaishi kisiwani kusiko taarifa ama kujua habari za kwingine.
 
Wanaendesha wanavyotaka wao kwa sababu tumekuwa wavivu kupaza sauti physically tuna kalia kupaza sauti mitandaoni ambapo wanapita na kuzipuuza kama vile hawazioni.
Kama tusingelikuwa na unafikinafiki watumiaji wote wa simu tungeacha kuweka "vocha" alau siku moja tu kwa mpigo TUNGEELEWANA... Maana inaonesha wanahalalisha "uizi wa makampuni ya simu" Je kwanini wateja hawashirikishwi kutoa maoni yao kabla ya huu upuuzi wao
 
Salamu Ndugu Ali Alile.

Najua ipo mingi, ila Mzimu huu ukiuvumilia utakuumiza na kutuumiza Ndugu Ali Alile??

Mzimu wakumfurahisha Kiti,
Kiti alikua akiona nyumba ina kunguni anachoma nyumba nzima!! , haijalishi waliomo wataishi vip???

Sasa kiti hayupo tafadhali mizimu ya ajabu ajabu sharti ikataliwe.
Zimu ka hili lisilotaka watu waongee kwa picha na mapicha mtembeo, muonano mbashara jamani linatia HASARA.

Unatakiwa ajue kwenye maongezi kuna biashara, mapicha picha ndo mvuto wa biashara sasa kama anataka kuchoma nyumba Moto kwaajili ya kunguni, tunamshauri kunguni hao watahamia kibanda chake kabla ya nyumba kuteketea.

Mzimu huu alioutengeza kumfurahisha kiti ujiongezo mara moja kabla haujakurudia au anadhani Mzimu unavuka maji baharini??
Sisi ndugu zako wa Wanyo wa Ongeni!
 
Kama Zimbabwe yan ukinunua bando we kidume kwelikweli,mi nitoe jero ili nipate mb 150!???..si bora jero langu ninunue al kasusu??!!.kwa sababu mb 150 nafanyia nini..huyu ndungulile sijui alikuwa anawaza nini,au yeye bando anawekewaga na shemeji ake
 
Hii mitandao ya Simu hivi ni kweli inashindwa kutumia fulsa?.

Mmiliki mmoja wa hii mitandao akishusha bei za Bundle kidogo tu, ni wazi atateka idadi kubwa sana ya wateja.
 
Hii mitandao ya Simu hivi ni kweli inashindwa kutumia fulsa?.

Mmiliki mmoja wa hii mitandao akishusha bei za Bundle kidogo tu, ni wazi atateka idadi kubwa sana ya wateja.
unadhani kupandishwa huku wameamaua wenyewe hio ni Kodi, sa nani mwenye jeuri nani alipe Kodi kubwa kuliko anachoingiza??
 
Back
Top Bottom