Walifanyia wapi huo utafiti kubaini shule za bweni azisaidii watoto katika socialisation, na hilo jambo linawezekana through ‘nuclear family’ and local communities tu.
Ningeelewa wangesema labda usalama watoto wawapo huko mashuleni, ie shule zisizokuwa na waangalizi wa kutosha kama matrons, walimu wa zamu kuangalia usalama wao mpaka muda wa kulala, ulinzi wa ukuta, geti, walinzi kuhakikisha watoto awatoki nje ya shule au watu awaingii mipaka ya shule na mambo mengine ya msingi juu ya usalama wao.
Lakini kusema unafungia tu kwa sababu ya socialisation issues ni sababu zisizo na msingi. Watoto wengine wanapoishi hakuna shule nzuri zinazofaulisha, au zipo mbali, au maporini wana pishana na wanyama pori, au wazazi awapo nyumbani muda mwingi.
Kuna sababu luluki wazazi wanapeleka watoto shule za boarding, mfano mimi nimesoma boarding kuanzia la kwanza moja ya sababu nyumba ilikuwa na mitoto kibao kupunguza headache wazazi wakaona waturushe boarding wapate muda wa kupumua.
Busara ni kuweka vigezo vikali vya ulinzi ili kuweka watoto wadogo bweni, lakini sio kuzuia kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu.