Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Tanzania: Serikali yapiga marufuku watoto kukaa bweni (boarding) kuanzia darasa la nne kushuka chini

Tena hata hiyo kwa kibali maalum iondolewe.ndio maana tunapata ma graduate wa ajabuajabu kwa kutelekeza malezi ya watt na kutegemea waalim watulelee watoto.
Hata wanavyosema kuanzia std4 kushuka chini wasiruhusiwe kulala bweni,bado haitoshi. Inatakiwa wote kuanzia std7 kushuka chini. Bweni iwe kuanzia sekondari pekee. Hizi shule binafsi wanafanya haya kwa malengo ya kibiashara zaidi..
 
Walifanyia wapi huo utafiti kubaini shule za bweni azisaidii watoto katika socialisation, na hilo jambo linawezekana through ‘nuclear family’ and local communities tu.

Ningeelewa wangesema labda usalama watoto wawapo huko mashuleni, ie shule zisizokuwa na waangalizi wa kutosha kama matrons, walimu wa zamu kuangalia usalama wao mpaka muda wa kulala, ulinzi wa ukuta, geti, walinzi kuhakikisha watoto awatoki nje ya shule au watu awaingii mipaka ya shule na mambo mengine ya msingi juu ya usalama wao.

Lakini kusema unafungia tu kwa sababu ya socialisation issues ni sababu zisizo na msingi. Watoto wengine wanapoishi hakuna shule nzuri zinazofaulisha, au zipo mbali, au maporini wana pishana na wanyama pori, au wazazi awapo nyumbani muda mwingi.

Kuna sababu luluki wazazi wanapeleka watoto shule za boarding, mfano mimi nimesoma boarding kuanzia la kwanza moja ya sababu nyumba ilikuwa na mitoto kibao kupunguza headache wazazi wakaona waturushe boarding wapate muda wa kupumua.

Busara ni kuweka vigezo vikali vya ulinzi ili kuweka watoto wadogo bweni, lakini sio kuzuia kwa sababu zisizo na kichwa wala miguu.
 
Waraka huo ulitolewa na Kamishna wa Elimu wa wizara hiyo, Dk Lyabwene Mtahabwa kwa wadau wa elimu nchini unasema utekelezaji wa waraka huo unatakiwa kuanza Machi Mosi mwaka huu.

Amesema hairuhusiwi kutoa huduma ya bweni kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza isipokuwa kwa kibali maalum kitakachotolewa na Kamishna wa Elimu baada ya kupokea maombi kutoka mdau husika.
Dk Mtahabwa amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa mwongozo wa uanzishaji wa usajili wa shule uliotolewa na wizara Novemba 2020.

Amesema kwa upande mwingine malezi na makuzi ya mtoto yanategemea sana mchango mkubwa unaotolewa na familia kupitia wazazi/walezi wa watoto hao.

“Hata hivyo imebainika kuwa kuna baadhi ya shule zimekuwa zikipokea watotro wenye umri mdogo kuanzia darasa la awali hadi darasa la nne,”amesema.

Amesema huduma za bweni kwa wanafunzi wenye umri mdogo ikiwemo wale wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne huwanyima watoto fursa ya kushikamana na familia na jamii zao, kujenga maadili na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya familia na jamii zao.

Kwa upande wa makambi, Dk Mtahabwa amesema hairuhusiwi kwa shule yoyote ile kuwa na makambi ya kitaaluma.

Amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa Waraka wa Elimu namba 3 wa mwaka 2007 kuhusu kukataza kambi za masomo katika shule za msingi.

“Hata hivyo imethihirika kuwa makambi mengi yamebainika kuwa na mazingira hatarishi kimaadili, usalama na afya za wanafunzi kutokana na kuanzishwa bila kufuata taratibu rasmi za uanzishwaji wa bweni au makazi ya pamoja ya wanafunzi,”amesema.
 
Nliwahi kwenda visitation day ya mtoto wa mtu darasa la 5 ye alikua boarding..nkakutana na wengne kama miaka mitatu kiumri yani tufanye yupo baby class au middle class..halafu kawekwa boarding..nkashangaa!!

Ila naelewa ni changamoto za maisha na malezi tu.usiombee ukose mda wa kuwa free halafu una mtoto hana msaidizi
 
Hao watoto wanaosoma sekondari nao wanakuwa wadogo sana kiasi chakuwa rahisi kuharibiwa...

Inawezekana zipo shule zenye umakini lakini zilizonyingi umakini ni mdogo sana kwenye malezi ya hawa watoto.
Hivi hawa panya road ambao wengine wameishia tu darasa la pili ni Boarding Schools ndiyo zimewaharibu?
 
Hii ni hatua nzuri.

Huwa najiuliza hawa watoto wa siku hizi eti wanaambiwa darasa la 4 wakae boarding kwa masomo yapi hasa ambayo enzi zetu sie hatujasoma?

Mpaka mtu unajiuliza ni darasa la 4 tu au wanasomea PHD?

Wafute kabisa huo utaratibu,darasa la 4 ni watoto wadogo kabisa!
 
Nadhani Sheria ya mtoto kutokukaa boarding iingaliwe upya siku hizi watoto huanza shule mapema darasa la tano anaingia akiwa na miaka kumi au kumi kasoro ukimpeleka boarding bado ni mdogo sana kwa umri huo anatakiwa kuwa mikononi mwa wazazi,
 
Kama vipindi vitaanza muda uleule kwa madarasa yote basi tutegemee janga jingine hasa kwa watoto haohao wa day madarasa ya chini shule za private.

bodaboda.jpg
0595dce6a39c452cfc9a4da5f204d8608cbd2ffe.jpg
wazazi-pic.jpg
259844f1ae667cd8dceecf5a6e885aca8e0515c3.jpg
 
Nadhani Sheria ya mtoto kutokukaa boarding iingaliwe upya siku hizi watoto huanza shule mapema darasa la tano anaingia akiwa na miaka kumi au kumi kasoro ukimpeleka boarding bado Ni mdogo sn kwa umri huo anatakiwa kuwa mikononi mwa wazazi,
Kwani mzazi kalazimishwa kupeleka boarding au ni kiherehere chake?
 
Mi mwanangu primary sipeleki boarding hata Kama itakuwa bure sitathubutu,secondary Napo nitafikiria
Ni maamuzi yako binafsi na upo sahihi kabisa,lakini pia atakaepeleka mtoto wake boardimg pia yupo sahihi.
 
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekumbusha kuwa hairuhusiwi huduma ya bweni kutolewa kwa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza hadi la nne...
Tamko hili lina mantiki maridhawa.

Ni sahihi
 
Back
Top Bottom