TBC: Mfanyakazi aliyesoma habari kuhusu Meli ya MV Mwanza amechukuliwa hatua

TBC: Mfanyakazi aliyesoma habari kuhusu Meli ya MV Mwanza amechukuliwa hatua

Tutajiwe jina ila tukikesha naye vijiweni tujue kweli hatua zimechukuliwa
 
Hatua za kinidhamu za nini? Huyo anatakiwa avalishwe bukta ya blue shati nyeupe kidumu na fagio aende kusoma jografia darasa la 5
 
Hawa ni wengi tu, mnashangaa watangazaji, nendeni mashuleni mkashangae walimu wanafundisha kwa kubabaisha wanafunzi masomo wasiyokuwa na weledi nayo. Unakuta mwalimu anafundisha somo fulani huku hajui mada nyingi zilizoko kwenye somo lake, anaishia kurukaruka tu mada. Ukimuuliza mambo madogo ya primary yahusuyo somo lake hajui unabaki kushangaa ualimu kaupataje ingawa ana cheti cha ualimu, labda alikwenda chuoni kujifunza mbinu tu za kufundishia ila inside topic hana back up
 
wamemuonya ripota ila cha kushangaza na mtoa nidhamu badala ya kuandika 12 February 2024 mmeandika 12 February 2023. Ina maana bado hamjavuka mwaka? Yani bado mko nyuma ya majira? Haya ni matokeo ya kukimbilia kuandika vitu haraka haraka mnakosa hata muda wa kuedit.

View attachment 2949130
Nchi yakupigana fix. Alimaanisha hivyo inamaana watu hawajamsikia? Hata hiyo taarifa inakichafua chombo.
 
Professionalism vs Uchawa hahahaha

Na watakosea sana mpaka watakapojitambua.

"Raisi TRUMP AMPONGEZA MAGUFULI" HAWA TBC HAWA😝😆😆😆😆😆😆

HATA MAGU MPENDA SIFA ALIJISHTUKIA
 
Mkisema yeye aliletewa script tu aisome ina maana hakuisoma kabla ya kwenda hewani? Haya, kama mwandishi alikosea yeye alishindwaje kuhariri? Au msomaji huruhusiwi kuhariri unasoma hichohicho usome hata kama unaona kimekosewa? Sasa kama naona imeandikwa rais wa uganda ni kagame nisome hivyohivyo bila kusoma ni museven huku najua ni sahihi? Waandishi wa habari wanapaswa kuwa well know/much know wa maswala mengi sawa na walimu. Kama hujui waone wataalam wa mambo hayo wakujaze ufahamu
 
Huu ni uonevu tu... Hapa walitakiwa wafunike kombe mwanaharamu apite
IMG_25670330_174912.JPG
 
Back
Top Bottom