TBC: Mfanyakazi aliyesoma habari kuhusu Meli ya MV Mwanza amechukuliwa hatua

Wameanza kwa kumtetea kuwa alimaanisha blah blah kisha eti alichukuliwa hatua!

Ni UONGO.
 
Mtangaza habari katuabisha wanaume. Ilitakiwa alale ndani polisi na vyeti vichunguzwe. Katika hali ya kawaida meli inaendaje Sudani wajameni? Au alikuwa amekunywa? Madhara ya watu kupewa kazi bila kusomea ndio haya
 
Wongo mtupu. Ndio shida ya kuwa mtu mzima chawa, yani unasema kila kitu bila reasoning.
 
Huyo aliyetoa huu ufafanuzi hapo TBC naye achukuliwe hatua.

Hiyo mizigo ya Malawi au Zambia kwenye Mv Mwanza itakuwa inatokea wapi?

Hawa jamaa wa TBC wanatuonaje?
 
sasa kama kuutwaaaa watu wanawaza teuzi tu wanashukuru rais hadi mvua ikijinyeshea zake huko unategemea nini?
 
Huyo muandishi yupo sawa, c mnajua tena tupo kwenye kipindi cha kusifia hadi kupitiliza
 
Ameonewa, mbona yule waziri aliyesema Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zimbabwe hakuchukuliwa hatua zozote.
 
Inasemekana walimcheleweshea mshahara akaamua asome habari vibaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…