TFF na Bodi ya Ligi, inaeendelea kujidharirisha baada ya CRDB kuijibu Yanga SC kuwa pesa walishatoa
Dada acha wapigane tuone nani atavuja damu nyingi...
Kuna kitu kinasukwa hapa ..hii ishu pia imeshaingiliwa na siasa...Hawa wapumbavu háwajui kua si kila mtanzania anashadadia siasa , wengine wanapenda soka kwa ajili ya kujiburudisha ..Sasa timu zimeanza kutumika kuzima moto wa NRNE...baada ya muda Mpira utakosa msisimko sababu ya kuingiliwa na wanasiasa wapumbavu
Kabisaa kaka tukae tuangalie movie
 
Haya CRDB wamemwaga mboga Baada ya Ally kamwe kumwaga ugali

TFF na Bodi ya Ligi kuna changamoto Kubwa sana, haya njooni miwape majibu Yanga SC pesa mmepeleka wapi?

Pia soma > Ali Kamwe: Hatutacheza mchezo wa kombe la Shirikisho CRDB mpaka tulipwe pesa zetu za Msimu uliopita

---
TAARIFA KWA UMMA
​
Benki ya CRDB inapenda kutoa ufanunuzi wa madai yaliyotolewa na Msemaji wa Klabu ya Yanga katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika tarehe 09 Juni 2025 katika Makao Makuu ya klabu hiyo.
Katika mkutano huo, Msemaji wa Klabu hiyo alinukuliwa akitoa taarifa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kwetu kama Mdhamini Mkuu wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB kuwa Klabu ya Yanga haitocheza fainali za mashindano hayo msimu huu kama hawatolipwa fedha za ubingwa wa msimu uliopita.

Tungependa kuufahamisha umma na wadau wote wa soka kuwa Benki ya CRDB ni taasisi yenye kuzingatia weledi, kanuni na taratibu na kwa msingi huo tayari Benki ilikwisha tekeleza kikamilifu wajibu wake wa kifedha kwa TFF kama sehemu ya makubaliano ya udhamini wa mashindano haya. Malipo yote ya msimu uliopita yalifanyika kwa TFF kwa mujibu wa mkataba baina ya Benki ya CRDB na TFF.

Benki ya CRDB inatambua kuwa mbali na mchezo wa soka kuunganisha jamii yetu na kutoa burudani, lakini pia mchezo huu ni ajira kwa vijana wengi, hivyo dhamira yetu ni kuendelea kushirikiana na TFF, vilabu na wadau wengine katika kukuza mchezo huu kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Imetolewa na;
Idara ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma
Benki ya CRDB
Juni 10, 2025

Michezo tu
 
Yanga wameongeza barua nyingine kwa umma. Hapa nimechoka hili picha haliishi naona kuna mpambano na wa No reforms hakuna kupokea. Ngoja nikae kimya
Naona hapa kama Utoto tu. Baada ya barua ya TFF ilipaswa Watu wa finance Yanga wakutane na TFF kufanya reconciliation halafu itoke ripoti moja. Ukisoma between the line, unaona hata club yangu imejibu kiujumla jumla kuhusu kudaina na TFF.
 
Mimi ni Yanga pia. Hivi umeelewa majibu ya TFF mkuu? Uongozi wa timu yetu uliiandikia TFF kuwa deni likatwe kwenye malipo yao ya zawadi za ubingwa. Inamaana ilishakatwa kitambo. Ilikuwa ni jukumu la timu ya Yanga kwenda TFF kuhakiki makato yao ya deni mapema ili kama kuna kiasi kinabaki kichukuliwe na kama Yanga inadaiwa iendelee kujipanga namna ya kumaliza deni.
Umeona majibu ya Yanga khs hiyo taarifa ya tff.

Kuna mambo mengi hatuyajui, tuendelee kusoma pande zote huku tukiongeza na za kwetu
 
Naona hapa kama Utoto tu. Baada ya barua ya TFF ilipaswa Watu wa finance Yanga wakutane na TFF kufanya reconciliation halafu itoke ripoti moja. Ukisoma between the line, unaona hata club yangu imejibu kiujumla jumla kuhusu kudaina na TFF.
Kwanin unaona watu wa finance yanga ndo walipaswa kwenda tff kukokotoa salio?
Na sio tff walipaswa wawape Yanga salio lao baada ya kukata deni wanalosema?

Kata chako unipe haki yangu, siyo ukate chako halafu tena ubaki na haki yangu. Hiyo siyo sawa
 
Karia ni tapeli kama alivyokuwa Mbowe kwa chadema!! Anajifanya kufanya tupriject kiini macho ili watu wasiohoji mabilion anayopata...Caf, Fifa!. Afu kuna ya madundukwa yanakwambia mitano tena!!. Simba na ccm akili zao zinafanana tofauti ya ni jezi tu.😂
 
Nimecheka sanaaa...hasa ulivyojiuliza mwanzo kabisa kama ulijua wamekatwa...eti songesha... 😀
Ila inamaana wao Yanga mwaka mzima wamekaa kimya au hao tff hawasemi why hela haipo mpk leo?
Yanga haijakaa kimya. Wameiandikia TFF Septemba mwaka Jana na Aprili mwaka huu wamekumbushia.
TFf waliopti ku myuti.
 
Mimi ni Yanga pia. Hivi umeelewa majibu ya TFF mkuu? Uongozi wa timu yetu uliiandikia TFF kuwa deni likatwe kwenye malipo yao ya zawadi za ubingwa. Inamaana ilishakatwa kitambo. Ilikuwa ni jukumu la timu ya Yanga kwenda TFF kuhakiki makato yao ya deni mapema ili kama kuna kiasi kinabaki kichukuliwe na kama Yanga inadaiwa iendelee kujipanga namna ya kumaliza deni.
Kama Yanga anadaiwa kweli, kwani asingejibiwa kwenye barua zake za kudai na kukunbushia Zawadi ya Ubingwa wa FA CRDB ?
 
Mbwa ni mmoja tu mkuuu.
Usisahau SIMBA aliandika barua moja tuu.

Mpaka leo yanga ameandika barua karibia Dunia nzima
Kama barua ya NGADA SC ilipata majibu positive ulitaka waendelee kuandika nini?
MANZOKI mna vituko, hamjambo.
 
Ni ngumu kutaja kwa haraka kiwango cha pesa kinachodaiwa kwa kuwa mambo yametokea kwa haraka tangu tamko la Kamwe kisha CRDB. Ndio maana maana wameita team ya finance iripoti ofisini kuhakiki madai yao.

Hapa TFF nawapa heko kwa response ya haraka vinginevyo mambo yangekuwa hovyo
Yaani taasisi kubwa kama TFF hawana file wala documents za clubs zinazozidai hela mpaka wakae chini waanze kufanya mahesabu?
 
Mimi ni Yanga pia. Hivi umeelewa majibu ya TFF mkuu? Uongozi wa timu yetu uliiandikia TFF kuwa deni likatwe kwenye malipo yao ya zawadi za ubingwa. Inamaana ilishakatwa kitambo. Ilikuwa ni jukumu la timu ya Yanga kwenda TFF kuhakiki makato yao ya deni mapema ili kama kuna kiasi kinabaki kichukuliwe na kama Yanga inadaiwa iendelee kujipanga namna ya kumaliza deni.
Lete hiyo barua ya Yanga kuomba ikatwe madeni.
 
Back
Top Bottom