TFF na Bodi ya Ligi, inaeendelea kujidharirisha baada ya CRDB kuijibu Yanga SC kuwa pesa walishatoa
Ukikaa kwenye kitengo cha pesa au kusimamia taasisi inayopokea pesa toka taasisi nyingine huwezi maliza salama ama sivyo ujitoe mapema. Sep blater haikumuacha salama. Pesa inamuingiza matatizoni yeyote
Sure ni kweli unachoongea...
Taasisi hasa za kanisa na mpira zina fedha nyingi...huko kuchafuka nje nje...
 
Ahahha si unajua Karia hawezi kukubali kirahisi so mengi yataenda kutokea soon...
Ila awe makini kweli
Na anaruka viunzi kwa jeuri balaa. Ila hapa wale aliowashinda kwenye uchaguzi wanarudi kumshambulia kwa kasi. Hapa ndio utaelewa kwani mara nyingi earthquake inapita kwenye area of weakness
 
Hapa sasa tayari binafsi naanza kupata picha kwa nini Yanga wanajeuri ya kusema hawachezi dabi.

Kweli kabisa mpaka sasa dabi haitachezwa. Haitachezwa kwa sababu kuna watu wakubwa sana wapo nyuma ya Yanga kuhakikisha Wallace Karia hatoboi labda kwa sababu amezidisha makandokando anakula peke yake.

Na hata Kamwe kusema hawachezi fainali ya CRDB ni mwendelezo wa kuibua hoja kwamba huko TFF wanakula zaidi ya urefu wa kamba, pamejaa rushwa.

Hivi jamani, kuna kipindi ambacho TFF imewahi kuwa na udhamini mnono na pesa nyingi kama awamu ya Karia? Iweje apewe pesa na CRDB halafu asiziwasilishe Yanga? Mana yake wanakula sana hao watu. Safari hii hatoboi!
Halafu kama vile hajielewi vizuri, mtu una makandokando halafu bado tena unaongea shobo kwa Yanga. Kulikuwa na sababu gani ya kutoa kauli kama zile kwa Yanga pale uwanja wa ndege
 
Na anaruka viunzi kwa jeuri balaa. Ila hapa wale aliowashinda kwenye uchaguzi wanarudi kumshambulia kwa kasi. Hapa ndio utaelewa kwani mara nyingi earthquake inapita kwenye area of weakness
Nakwambia yajayo yanasikitisha sio tuu TFF mpk timu zetu
 
Mshaanza kucheza mdundo wa Yanga sasa,na mbado
Mdundo mdundiko??
Hakuna cha mdundo wa uto..hapo tunawaangalia tuu mtakavyofikishana FIFA mpira ufungiwe...
Ile kauli ya Aly Komwe kuwa kuna kiongozi wa juu kapiga simu geti lisifunguliwe...mtaijua soon
 
Bado hajasema,wengi mlikuwa mnailaumu Yanga bila kujua nini kipo nyuma ya pazia juu ya uozo wa TFF na Bodi yake.
Hat timu yako ina uozo...kwa sbb why wavumilie wasilipwe hela zao? Ukiona hivyo wana kitu walikua wanakipata kwa hao tff sasa wameona labda mwakani hawatakua favoured ndo wameamua kumwaga mboga ili wote wakose
 
Haya CRDB wamemwaga mboga Baada ya Ally kamwe kumwaga ugali

TFF na Bodi ya Ligi kuna changamoto Kubwa sana, haya njooni miwape majibu Yanga SC pesa mmepeleka wapi?

Pia soma > Ali Kamwe: Hatutacheza mchezo wa kombe la Shirikisho CRDB mpaka tulipwe pesa zetu za Msimu uliopita

---
TAARIFA KWA UMMA
​
Benki ya CRDB inapenda kutoa ufanunuzi wa madai yaliyotolewa na Msemaji wa Klabu ya Yanga katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika tarehe 09 Juni 2025 katika Makao Makuu ya klabu hiyo.
Katika mkutano huo, Msemaji wa Klabu hiyo alinukuliwa akitoa taarifa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kwetu kama Mdhamini Mkuu wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB kuwa Klabu ya Yanga haitocheza fainali za mashindano hayo msimu huu kama hawatolipwa fedha za ubingwa wa msimu uliopita.

Tungependa kuufahamisha umma na wadau wote wa soka kuwa Benki ya CRDB ni taasisi yenye kuzingatia weledi, kanuni na taratibu na kwa msingi huo tayari Benki ilikwisha tekeleza kikamilifu wajibu wake wa kifedha kwa TFF kama sehemu ya makubaliano ya udhamini wa mashindano haya. Malipo yote ya msimu uliopita yalifanyika kwa TFF kwa mujibu wa mkataba baina ya Benki ya CRDB na TFF.

Benki ya CRDB inatambua kuwa mbali na mchezo wa soka kuunganisha jamii yetu na kutoa burudani, lakini pia mchezo huu ni ajira kwa vijana wengi, hivyo dhamira yetu ni kuendelea kushirikiana na TFF, vilabu na wadau wengine katika kukuza mchezo huu kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Imetolewa na;
Idara ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma
Benki ya CRDB
Juni 10, 2025

TFF Wana kesi ya kujibu
 
Screenshot_2025-06-10-14-47-42-683_org.mozilla.firefox.jpg
 
Back
Top Bottom