Taarifa yao imezingatia weledi. Huwezi weka kila details
 
Umezipenda au zimekuboa?
Nimebaini soka la Tz linasimamiwa na viongozi wapuuzi wasio na maono yeyote kuanzia clubs mpaka TFF. Sasa mimi siwezi kuendelea kufuatilia vitu vya kitoto toto.

Imagine Shirikisho la soka linatapeli club fedha. Lakini kuna sababu gani zawadi ya Yanga apokee TFF. Inatofauti gani na wale tuma kwa namba hii
 
Haya CRDB wamemwaga mboga Baada ya Ally kamwe kumwaga ugali

TFF na Bodi ya Ligi kuna changamoto Kubwa sana, haya njooni miwape majibu Yanga SC pesa mmepeleka wapi?!!!
Hapa sasa tayari binafsi naanza kupata picha kwa nini Yanga wanajeuri ya kusema hawachezi dabi.

Kweli kabisa mpaka sasa dabi haitachezwa. Haitachezwa kwa sababu kuna watu wakubwa sana wapo nyuma ya Yanga kuhakikisha Wallace Karia hatoboi labda kwa sababu amezidisha makandokando anakula peke yake.

Na hata Kamwe kusema hawachezi fainali ya CRDB ni mwendelezo wa kuibua hoja kwamba huko TFF wanakula zaidi ya urefu wa kamba, pamejaa rushwa.

Hivi jamani, kuna kipindi ambacho TFF imewahi kuwa na udhamini mnono na pesa nyingi kama awamu ya Karia? Iweje apewe pesa na CRDB halafu asiziwasilishe Yanga? Mana yake wanakula sana hao watu. Safari hii hatoboi!
 
Sasa watu ndo watajua kuwa pale tff ubabaishaji ni mwingi sana. Tuwaache Yanga wasimamie msimamo wao ili ubabaishaji upungue pale tff na bodi ya ligi
 
TTF hawataki kutoa fedha kwa washindi/mshindi wa msimu uliopita?

Mkataba wa udhamini wa 3.7 bilioni
 
Uhuni mwingi soka letu kivyetuvyetu, kanuni zipo hila hazifuati ni mwendo wa hekima na busara. Then leo linaibuka jingine hili la upigaji. Timu kubwa kama Yanga haijalipwa chake vipi hao wengine,marefa nao manake tuna walaumu ila hatujui nao watakuwa wanakopwa. Mpira wa bongo mgumu sana.
 
Mfikirie refa ambaye analipwa 300K, 500K au 1M halafu anaenda kuchezesha mechi ya Kengold dhidi ya Simba au Yanga. Waamuzi wakapigwa 10M halafu mabeki wakapigwa 2m kila mmoja unaona nini kinatokea?
 
Haya CRDB wamemwaga mboga Baada ya Ally kamwe kumwaga ugali

TFF na Bodi ya Ligi kuna changamoto Kubwa sana, haya njooni miwape majibu Yanga SC pesa mmepeleka wapi?!!!
Ripoti ya ukaguzi wa sieji wa tiefuefu na , Bodi ya ligi zipoje, sio za umma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…