Tony Blair kaja kumwona Mama Samia? Nina Masikitiko!

Mkuu siyo rahisi Pasco kuthibitasha posti yake maana, yeye ni mtu wa local politics.
Hizi za kimataifa inaelekea ximempita kwa mbali.
Busara ilikuwa kuelewa msingi wa mada yenyewe.
Blair ni nuksi, kila anachoshika ni kawama, ana mikono iliyojaa damu za watu waliouwawa kwa hila huko Iraq.
 
Kama ulimpigia Kura ulifanya vizuri
 
Huyo SSH wako aliyekuwa makamu wa jitu lile lililouwa wengi unafikiri mikono yake haijachafuka damu? Unawezaje kumtenganisha na jitu wakati alishasema mwenyewe kwamba yeye na jitu ni kitu kimoja?! Wauaji huwa wanatembeleana.
 
Iraq na Tanzania ni cases mbili tofauti kabisa! Tatizo baadhi ya Watanzania wanapenda "Mboka ya makambo". Tuache maneno mengi. Tumuache Rais aongoze. Rais ni taasisi. Msiichukulie nchi yetu kirahisi. Historia ya Tanzania kimataifa ilikwisha jenga na Mwalimu Nyerere. Nchi hii ina heshima kubwa duniani.
 
Madame amezidi ukarimu sijui huo ukarimu mkubwa hivi unatokea wapi.
 
Anatembelea koloni lake kuangalia namna ya kulirudisha kabla wachina hawajalibeba kwa bei chee kupitia bandari ya bagamoyo
 
UNGETUAMBIA HAPA KWETU KAJA KUFANYA NINI NDIO INGETUSAIDIA HAYA MENGINE NI FITNA TU AMBAZO HAZINA MSAADA KWA NCHI YETU
 
Mambo ya Sadam na Tzn vinahusianaje? Kama ana pesa za kuwekeza aje hadithi zingine hazina maana kwetu.
 
Mkuu usiwe na wasi wasi, baada ya Blair kuonana na Samia ujue next Samia ataalikwa kupiga picha na Biden na Johnson then wawakonge CHADEMA mchezo kwisha.

Huku nyuma agenda za kufisadi nchi zitaendelea kwa kasi kwa kisingizio Mama Anakubalika hadi USA na UK.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…