Tony Blair kaja kumwona Mama Samia? Nina Masikitiko!

Tony Blair kaja kumwona Mama Samia? Nina Masikitiko!

Usilolijua ni sawa na usiku wa giza: Tonny Blair ni waziri mkuu aliependwa sana Uingereza baada ya Winston Churchil, hayo ya Saddam yasome tu kwenye magazeti, ila Axis Of Evil Saddam alikua yupo top of all. Hata viongozi wa uingereza waliokua wakivipinga vita vya Iraq wengi wao weshafutika kwenye hii dunia..
 
Usitake kudanganya.
Blair aliokolewa na mahakama baada ya Tume ya Uchunguzi kuhusu vita ya Iraq kubaini kuwa altumia ulaghai na uongo kuingiza nchi yake vitani.
 
View attachment 1957586

Kati ya viongozi wa Uingereza waliowahi kunikatisha tamaa ni Tony Blair. Huyu alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kati ya mwaka 1997 mpaka 2007.

Wakati akipata Uwaziri Mkuu, ndiye alikuwa kiongozi kijana kuliko wote kwa miaka 185 ya historia ya Uingereza, na alikuwa na miaka 44 tu.

Na alikuwa kiongozi wa chama cha Labour, chama ambacho nami nikiwa Uingereza nilikipigia kura nikiwa huko. Kwa ujumla vijana nchini Uingereza walimkubali sana.

Tony Blair aliongoza vizuri hadi baada ya 9/11 Marekani ilipopigwa World Trade Centre, New York.
Katika hasira na mchecheto wa kulipiza kisasi, Uingereza na Marekani ilibidi waunde maadui, maana hawakujua nani amewapiga.

Adui mmoja aliyesingiziwa ni Saddam Hussein wa Iraq. Huyu akatengenezewa uongo wa kutisha, ati ana silaha za kutisha zinazoweza kupiga hadi New York ndani ya dakika 45?

Na kwamba silaha hizo hazikai sehemu moja zinazungushwa zungushwa ndani ya Iraq ili zisifahamike ziko wapi.

Tony Blair alikuwa mstari wa mbele kupiga kelele kuwa Saddam ana Weapons of Mass Destruction!
Kilichotushangaza wengi ni kuona uongo wa dhahiri ukipigiwa upatu, na tukajiuliza hivi kuna silaha mbaya na hatari kuliko za Nuclear ambazo wakubwa hawa wanazo?

Pamoja na mapingamixi toka mataifa mengi, Marekani na Uingereza walipitisha Azimio Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa, kuwa Saddam apigwe.

Saddam akapingwa na kuuwawa.
Pamoja nao wakauwawa wananchi wengi, wanawake na watoto.
Iraq haikuwahi kuwa salama tena.

Mwisho wa siku ikaja dhihirika kuwa hapakuwa na silaha zozote za maangamizi Iraq.
Waliouwawa waliuwawa bure.

Wale waaarabu walioipiga WTC-World Trade Centre, ikaja gundulika walitoka Saudia. Tony Blair na wenzake waligwaya kwa aibu!

Sasa huyu T Blair aliyesababisha vifo vya watu mamilioni wasio na hatia, yupo hapa kwetu, Ikulu.
Sijafurahia sana kiongozi mwenye mikono ya damu kuwa mgeni wa Mama Samia.

Sijawahi kuona nchi za Ulaya na Marekani wakimwalika Mugabe(Zimbabwe), Idi Amin(Uganda) au Mengiste Haile Mariam (Ethiopia) huko kwao.

Mwana JF, mpe neno!

Ni kama vile unamchagulia rafiki Mama Samia. Japo unazo hoja za kizalendo.
 
Usitake kudanganya.
Blair aliokolewa na mahakama baada ya Tume ya Uchunguzi kuhusu vita ya Iraq kubaini kuwa altumia ulaghai na uongo kuingiza nchi yake vitani.
Siasa tu hizo, hivi unafikiria waingereza wanaweza kufanya upumbavu kama huo??? ingekua hawampendi kihivyo, sasa mbona kila issue inayotokea duniani uwa lazima wamhoji kuona anasemaje...usilolijua ni kama usiku wa giza!!!kalaghabaho.
 
huyo mama yenu ana elimu kiasi gani (IQ) hata aweze kufanya mazungumzo na mtu smart kama Tony Blair?
 
Siasa tu hizo, hivi unafikiria waingereza wanaweza kufanya upumbavu kama huo??? ingekua hawampendi kihivyo, sasa mbona kila issue inayotokea duniani uwa lazima wamhoji kuona anasemaje...usilolijua ni kama usiku wa giza!!!kalaghabaho.
Kalagabaho wewe unayeshabikia kama zuzu mtu aliyepelekwa hadi mahakamani kwa kuua kupitia madaraka!
 
Haina maana kuja kwake ni kuendeleza hayo unayosema. Bado pia tunashirikiana na matifa yaaliyoyupeleka urumwani

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
mahakama ya wapi wewe zuzu?? huyu mtu billionaire huoni kaja kutengeneza pesa zaidi kwa chief Hangaya. mahakamani yanapelekwa majuha tu tena weusi.
We lijitu la madongo kuinama taabu sana.
Kila mzungu unaye mwina unafikiri ana noti za kukupa.
Miafrika mingine ndivyo mulivyo, subjective mentality.
 
Nakumbuka kama si 2002 au 2003 kuna mkaguzi wa silaha za maangamizi alienda kukagua Iraq akaambulia patupu. Mwishowe tukasikia amejinyonga, sasa sijui alijinyonga kweli au walimfanyizia sijui.
Walimuuua anaitwa Dr kelly wakafanya ionekane kama suucide,blair siyo mtu mzuri
 
Walimuuua anaitwa Dr kelly wakafanya ionekane kama suucide,blair siyo mtu mzuri
Thanks!
Kuna mijitu ni mizuzu kabisa haiekewi kuwa huyu Blair ni mtu hatari.
Lazima Rais wetu atonywe hilo, siyo kila hela ni safi.
 
Nilipo umeme umekata ukirudi nitapandisha kitabu kuhusu huyu jamaa kipindi hicho pia nilikuwa uingereza kama wewe ,ila nilidhani kupiga kura inaishia kwa wabunge na ma councillors kwa sisi wa commonwealth anyway sikuwahi kupiga kura kwa miaka mitatu niliyoishi pale
 
Thanks!
Kuna mijitu ni mizuzu kabisa haiekewi kuwa huyu Blair ni mtu hatari.
Lazima Rais wetu atinywe hilo, siyo kila hela ni safi.
Nimeona dr lwaitama kule twitter anasema jamaa kaja kusuluhisha issue ya madini yaliyoshikiliwa na mr slim kwenye deal gone wrong na jamaa wa awamu iliyopita ,siyo maneno yangu kaangalie tweets za jana za azavery lwaitama
 
Huyo jamaa ni The Devils advocate!
 
Shida ya KAWAJA siku mkikosana wanakua bitter balaa na wanakugeuka kama hawakujuhi. Ukiona wanakuja kuna kitu wanataka lakini pia ni jambo jema kushirikiana nao. Lakini kushirikiana nao kwa akili sana na wala si kuwafokea fokea.
 
Washington, DC(CNN)The Federal Bureau of Investigation on Saturday released the first of what is expected to be several documents related to its investigation of the 9/11 terrorist attacks and suspected Saudi government support for the hijackers, following an executive order by President Joe Biden.

The newly declassified document, which is from 2016, provides details of the FBI's work to investigate the alleged logistical support that a Saudi consular official and a suspected Saudi intelligence agent in Los Angeles provided to at least two of the men who hijacked planes on September 11, 2001.
Marekani wamewastukia Saudia, lakini pesa inaongea.
 
Nakumbuka kama si 2002 au 2003 kuna mkaguzi wa silaha za maangamizi alienda kukagua Iraq akaambulia patupu. Mwishowe tukasikia amejinyonga, sasa sijui alijinyonga kweli au walimfanyizia sijui.
Kama sijakosea alikuwa anaitwa Hans Blinks
 
Back
Top Bottom