Tony Blair kaja kumwona Mama Samia? Nina Masikitiko!

View attachment 1957586

Kati ya viongozi wa Uingereza waliowahi kunikatisha tamaa ni Tony Blair. Huyu alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kati ya mwaka 1997 mpaka 2007.

Wakati akipata Uwaziri Mkuu, ndiye alikuwa kiongozi kijana kuliko wote kwa miaka 185 ya historia ya Uingereza, na alikuwa na miaka 44 tu.

Na alikuwa kiongozi wa chama cha Labour, chama ambacho nami nikiwa Uingereza nilikipigia kura nikiwa huko. Kwa ujumla vijana nchini Uingereza walimkubali sana.

Tony Blair aliongoza vizuri hadi baada ya 9/11 Marekani ilipopigwa World Trade Centre, New York.
Katika hasira na mchecheto wa kulipiza kisasi, Uingereza na Marekani ilibidi waunde maadui, maana hawakujua nani amewapiga.

Adui mmoja aliyesingiziwa ni Saddam Hussein wa Iraq. Huyu akatengenezewa uongo wa kutisha, ati ana silaha za kutisha zinazoweza kupiga hadi New York ndani ya dakika 45?

Na kwamba silaha hizo hazikai sehemu moja zinazungushwa zungushwa ndani ya Iraq ili zisifahamike ziko wapi.

Tony Blair alikuwa mstari wa mbele kupiga kelele kuwa Saddam ana Weapons of Mass Destruction!
Kilichotushangaza wengi ni kuona uongo wa dhahiri ukipigiwa upatu, na tukajiuliza hivi kuna silaha mbaya na hatari kuliko za Nuclear ambazo wakubwa hawa wanazo?

Pamoja na mapingamixi toka mataifa mengi, Marekani na Uingereza walipitisha Azimio Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa, kuwa Saddam apigwe.

Saddam akapingwa na kuuwawa.
Pamoja nao wakauwawa wananchi wengi, wanawake na watoto.
Iraq haikuwahi kuwa salama tena.

Mwisho wa siku ikaja dhihirika kuwa hapakuwa na silaha zozote za maangamizi Iraq.
Waliouwawa waliuwawa bure.

Wale waaarabu walioipiga WTC-World Trade Centre, ikaja gundulika walitoka Saudia. Tony Blair na wenzake waligwaya kwa aibu!

Sasa huyu T Blair aliyesababisha vifo vya watu mamilioni wasio na hatia, yupo hapa kwetu, Ikulu.
Sijafurahia sana kiongozi mwenye mikono ya damu kuwa mgeni wa Mama Samia.

Sijawahi kuona nchi za Ulaya na Marekani wakimwalika Mugabe(Zimbabwe), Idi Amin(Uganda) au Mengiste Haile Mariam (Ethiopia) huko kwao.

Mwana JF, mpe neno!

Tony Blair ni wakala wa makampuni makubwa ya ukwasi huko Ulaya, yeye kazi yake ni kulobby hawa viongozi wa nchi zetu kukubali kufanya shughuli za kibiashara au kisiasa kwa faida ya hayo makampuni, kwa jina lingine Tony Blair ni tu wa connection (tenderpreneur) na analipwa pesa nyingi . Anatumia nafasi ya kuwahi kuwa waziri mkuu wa Uingereza kuwa kinara wa kurubuni viongozi wengi wa nchi masikini ,ndio kazi yake na nchi nyingi ambazo bwana huyu amejifanya kuwa mshauri au kuzishauri zote zimekuwa katika matatizo makubwa ya kiuchumi na kiusalama. Cha kujiuliza kwanini huyu mheshimiwa sana ghafla bin vuu kawa rafiki wa Tanzania na safari haziiishi? mbona wakati wa mwendazake tulikuwa hatumuoni? ni kipi cha zaidi ambacho sasa tunakiona bwana huyu anacho na kageuka lulu, kwa muda mfupi kaja mara mbili hizi ndio safari tunazozijua je anakuja kufanya nini yeye sio mfanyabiashara, je mbona safari zake yeye ni kukutana tu na wakuu wa nchi si bara hata Zanzibar , huko Zanzibar tunamuona akiwa anakula upepo kwenye bustani ya ikulu iliyo juu ya jengo la ikulu. Hawa wasiwe watu wa kutuamulia mustakabali wa nchi yetu, ni matapeli tu, hawana la maana zaidi ya 10% na hiyo ndio kazi ya huyu tapeli Blair.
 
Huyu ni kati ya Economic Hitmen wanaijificha kwenye kichaka cha diplomasia.

Wanatumika kuwalainisha viongozi wetu kama Hangaya na wengine kuruhusu mikataba ya kinyonyaji kwa njia mbali mbali.
Mkuu tangulia kwa Mangi Lounge agiza chochote roho inapenda! Huyu tapeli hakuwahi kutia pua yake hapa wakati wa mwendazake.
 
View attachment 1957586

Kati ya viongozi wa Uingereza waliowahi kunikatisha tamaa ni Tony Blair. Huyu alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kati ya mwaka 1997 mpaka 2007.

Wakati akipata Uwaziri Mkuu, ndiye alikuwa kiongozi kijana kuliko wote kwa miaka 185 ya historia ya Uingereza, na alikuwa na miaka 44 tu.

Na alikuwa kiongozi wa chama cha Labour, chama ambacho nami nikiwa Uingereza nilikipigia kura nikiwa huko. Kwa ujumla vijana nchini Uingereza walimkubali sana.

Tony Blair aliongoza vizuri hadi baada ya 9/11 Marekani ilipopigwa World Trade Centre, New York.
Katika hasira na mchecheto wa kulipiza kisasi, Uingereza na Marekani ilibidi waunde maadui, maana hawakujua nani amewapiga.

Adui mmoja aliyesingiziwa ni Saddam Hussein wa Iraq. Huyu akatengenezewa uongo wa kutisha, ati ana silaha za kutisha zinazoweza kupiga hadi New York ndani ya dakika 45?

Na kwamba silaha hizo hazikai sehemu moja zinazungushwa zungushwa ndani ya Iraq ili zisifahamike ziko wapi.

Tony Blair alikuwa mstari wa mbele kupiga kelele kuwa Saddam ana Weapons of Mass Destruction!
Kilichotushangaza wengi ni kuona uongo wa dhahiri ukipigiwa upatu, na tukajiuliza hivi kuna silaha mbaya na hatari kuliko za Nuclear ambazo wakubwa hawa wanazo?

Pamoja na mapingamixi toka mataifa mengi, Marekani na Uingereza walipitisha Azimio Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa, kuwa Saddam apigwe.

Saddam akapingwa na kuuwawa.
Pamoja nao wakauwawa wananchi wengi, wanawake na watoto.
Iraq haikuwahi kuwa salama tena.

Mwisho wa siku ikaja dhihirika kuwa hapakuwa na silaha zozote za maangamizi Iraq.
Waliouwawa waliuwawa bure.

Wale waaarabu walioipiga WTC-World Trade Centre, ikaja gundulika walitoka Saudia. Tony Blair na wenzake waligwaya kwa aibu!

Sasa huyu T Blair aliyesababisha vifo vya watu mamilioni wasio na hatia, yupo hapa kwetu, Ikulu.
Sijafurahia sana kiongozi mwenye mikono ya damu kuwa mgeni wa Mama Samia.

Sijawahi kuona nchi za Ulaya na Marekani wakimwalika Mugabe(Zimbabwe), Idi Amin(Uganda) au Mengiste Haile Mariam (Ethiopia) huko kwao.

Mwana JF, mpe neno!

Ni kweli hata mimi nina historia ya kuishi huko kama wewe. Tony Blair alitegemewa kuiwakilisha Uingereza na Ulaya nzima katika uhusiano wake wa pekee na Marekani kwa kuonesha ukomavu wa muda mrefu wa Uingereza katika masuala ya uhusiano yeye akaingiza ushabiki ambao gharama yake ya maisha ya watu imekuwa kubwa na kuhitimishwa kwa matatizo lukuki ya hali ya Mashariki ya Kati. Halafu haoni aibu! Aidha, uhusiano wake na Tanzania ulikuwa na Mheshimiwa Rais Mkapa, aliyemteua kushirikiana naye kwenye Tume ya Afrika iliyokuwa inajihusisha na namna ya kuikwamua Afrika katika matatizo yake ya maendeleo. Hii ilikuwa kabla ya vita kuanza Mashariki ya Kati. Walitoa mapendekezo mazuri tu hayakiwa na ulevi wa aina yo yote.Hapa katikati hakuwa na mahusiano ya wazi na viongozi wetu wakuu. Kwa sasa Blair anashughulika na maslahi yake binafsi. Kujihusisha kwake na Rais wetu mpendwa mapema hivi hakuwezi kumwacha kimya Mtanzania ye yote mwenye huo uzalendo ambao tumezoea kuusemea bila fikra za kina na maelezo ya kutosha kwa vizazi vijavyo!
 
Nakumbuka kama si 2002 au 2003 kuna mkaguzi wa silaha za maangamizi alienda kukagua Iraq akaambulia patupu. Mwishowe tukasikia amejinyonga, sasa sijui alijinyonga kweli au walimfanyizia sijui.
Politics haitaki ligi mkuu,ukisikia wengi wameenda huku na wewe unaenda,ukijifanya kukomaa sana,unapeperushwa.Fuatilia sana wale waliojifanya kukomaa sana wameishia wapi...
 
View attachment 1957586

Kati ya viongozi wa Uingereza waliowahi kunikatisha tamaa ni Tony Blair. Huyu alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kati ya mwaka 1997 mpaka 2007.

Wakati akipata Uwaziri Mkuu, ndiye alikuwa kiongozi kijana kuliko wote kwa miaka 185 ya historia ya Uingereza, na alikuwa na miaka 44 tu.

Na alikuwa kiongozi wa chama cha Labour, chama ambacho nami nikiwa Uingereza nilikipigia kura nikiwa huko. Kwa ujumla vijana nchini Uingereza walimkubali sana.

Tony Blair aliongoza vizuri hadi baada ya 9/11 Marekani ilipopigwa World Trade Centre, New York.
Katika hasira na mchecheto wa kulipiza kisasi, Uingereza na Marekani ilibidi waunde maadui, maana hawakujua nani amewapiga.

Adui mmoja aliyesingiziwa ni Saddam Hussein wa Iraq. Huyu akatengenezewa uongo wa kutisha, ati ana silaha za kutisha zinazoweza kupiga hadi New York ndani ya dakika 45?

Na kwamba silaha hizo hazikai sehemu moja zinazungushwa zungushwa ndani ya Iraq ili zisifahamike ziko wapi.

Tony Blair alikuwa mstari wa mbele kupiga kelele kuwa Saddam ana Weapons of Mass Destruction!
Kilichotushangaza wengi ni kuona uongo wa dhahiri ukipigiwa upatu, na tukajiuliza hivi kuna silaha mbaya na hatari kuliko za Nuclear ambazo wakubwa hawa wanazo?

Pamoja na mapingamixi toka mataifa mengi, Marekani na Uingereza walipitisha Azimio Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa, kuwa Saddam apigwe.

Saddam akapingwa na kuuwawa.
Pamoja nao wakauwawa wananchi wengi, wanawake na watoto.
Iraq haikuwahi kuwa salama tena.

Mwisho wa siku ikaja dhihirika kuwa hapakuwa na silaha zozote za maangamizi Iraq.
Waliouwawa waliuwawa bure.

Wale waaarabu walioipiga WTC-World Trade Centre, ikaja gundulika walitoka Saudia. Tony Blair na wenzake waligwaya kwa aibu!

Sasa huyu T Blair aliyesababisha vifo vya watu mamilioni wasio na hatia, yupo hapa kwetu, Ikulu.
Sijafurahia sana kiongozi mwenye mikono ya damu kuwa mgeni wa Mama Samia.

Sijawahi kuona nchi za Ulaya na Marekani wakimwalika Mugabe(Zimbabwe), Idi Amin(Uganda) au Mengiste Haile Mariam (Ethiopia) huko kwao.

Mwana JF, mpe neno!

Nafikiri kaja kumshauri afate uliberali wa magharibi kwenye uchumi badala ya kujali umma. Ndio unaona anawaweka maadui wa fikra za magufuli ili warudi kuiba uchumi wa tanzania 😂
 
Wakati wa Utawala wa Awamu ya kwanza ilikuwa ni vigumu sana kuona kiongozi kama Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair akiruhusiwa kuzuru Ikulu ama kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Huyu Tony Blair ni mhalifu wa kivita baada ya yeye na aliyekuwa Rais wa Marekani George Bush kudanganya dunia kwa kupitia baraza kuu la Umoja wa mataifa kuwa serikali ya Iraq ina silaha za maangamizi. Hii ilipelekea mamilioni ya raia wasiokuwa na hatia kuuwawa na majeshi ya kivamizi kutoka mataifa hayo makubwa.

Ni muhimu kwa Wizara ya Mambo za Nje ya Tanzania kuangalia upya sera za sasa kuhusu kuruhusu viongozi wanaoweza kukutana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haswa ukiaangalia rekodi zao za nyuma. Mwaka 1980 baada ya mapinduzi ya Liberia mauuaji makubwa yalifanyika chini ya kiongozi aliyeongoza mapinduzi hayo Samwel Doe.

Baada ya mapinduzi hayo kiongozi huyo alifanya ziara ambapo serikali ya Tanzania ilikataa kumpokea lakini baada ya Rais huyo kuomba sana Mwalimu Nyerere alikubali kukutana naye kwa saa moja tu bila kuwa na shamra shamra yeyote na kiongozi huyo alilaumiwa na Mwalimu Nyerere kwa vitendo vyake vya kikatili

Hivi hii ni msra pili kuja Tanzania kama sikosei alikuja tena wakati tunapokea chanjo corona kama sikosei
 
Back
Top Bottom