Nyie hii Mil 6 mnawezaje kusave aisee,
DSTV 110,000
Maji 100,000
Umeme 120,000
WiFi Nyumbani 70,000
Kifurushi cha simu mwezi 30,000
Kifurushi cha Bundle Camera za nyumbani - 20,000
Gari Full Tank Mbili/Mwezi 90Ltr*3800 = 400,000 (Hapa Bado Gari ya Mjerumani Haijacharuka)
Mshahara Dada wa Kazi 120,000 (Kama una Mlinzi pia mhesabie)
Wife Allowance 250,000
Wazazi na Msichana wao wa kazi 600,000
Mahitaji ya kula nyumbani 1,200,000
Kula yako mihangaikoni 300,000
Kodi 600,000
Subtotal -- 3,920,000
Kuna hizi gharama hapa chini kama unazo pia zinahitajika kupigiwa hesabu,
Beer Na Wana *************
Ada *************
Nauli za Wategemezi *************
Mchepuko. *************
Ufalme wa Mbinguni *************
Na katika nchi yangu huyu mtu anaiingiza hii mil 6 unakuta naye katika uwekezaji wake anatakiwa kulipa mishahara ya watu 3-5 kwa mwezi.
Bado kadhalika kadhaa, kuosha/service gari, viparcel vya nyumbani, , familia haijataka kwenda Fun City, Nauli za wakina Juniors kwenda shule , babu hajang'atwa na mbwa huko kijijini nk
Wakuu, tutafute hela, savings zangu zimetokana na nje ya earnings ya mil 6 kwa mwezi, peke yake haitoshi.