TUJIKUMBUSHE: Timu Maarufu za Ndondo kutoka mitaa yetu

Kijiweni FC. uyole moja..

Ikaja ikahusishwa kuuzwa na tajiri mmoja wa mashine za mpunga. Wachezaji waka anzisha timu yao.. ZARAGOZA..

humu walikuwepo miamba kama

1.Siasa- Golie, hapa manula akasome
2. Zaka panga mawe
3. Fabian
4. Tiasi
5. Rai
6. Muso
7. Dimini
8. Oden pamwannya
9. Ahazi - mwamba alienda kukipiga hadi zanzibar
10. Mtumba - Ezekiel saa mbili.. Alikipiga hadi tukuyu stars
 
Unaijua MUKU bro. Sijui kama siku hizi zipo hizo.
 
Unaijua MUKU bro. Sijui kama siku hizi zipo hizo.
Muku wanadai mtu anachanjiwa kuna ishu kama za kimila ua kishirikina maana hawa ni watu wapole ila wanakuwa na nguvu za ajabu wengi wanakuwa na alama kama za chale na hawali baadhi ya vyakula kama bamia ila ni zamani sana ....Hivi ndo ninavyojua na wengi wanakuwa na majini ya kupandisha ila ni wapole sana ..

yupo mmoja niliskia alipambana na mamba ziwa la mabawa pale .
 
Nilikuwa nachat na jamaa mmoja inbox akaniambia anamjua huyo David Izengo na jamaa akakiri kabisa kama Ingekuwa sasa angechezea Man U. Kulikuwa na vipaji sana kwenye Ndondo ila nyakati zilikuwa za giza. Kuna watu walikuwa na uwezo hata kuliko wachezaji wakubwa wa sasa ila nyakati hazikuwa sahihi kwetu. Kuna jamaa nilikuwa nasoma naye kuna siku nilijiunga kwenye group la Whatsapp la Sekondary nilipojitambulisha akasema "Jamaa wa Mpira wewe hata ligi kuu ya EPL ungecheza ila basi tu" hao akina Manura, Chama, Mayere n.k wanabebwa na majira na nyakati tu ila kuna watu walikuwa zaidi yao.
 
Kimsingi wale wanakuwa na Majini sio kawaida.
 
Kimsingi wale wanakuwa na Majini sio kawaida.
Ile siku jamaa anapiga kuamulia ilikuwa kasheshe ila mpaka kapigana kachokozwa sana maana alikuwa hataki kupigana mpaka mamaake alikuja ...Wakaenda nae ndani kwao kaitwa shekhe kumsomea kama masaa matatu mbele ndo katulia na alifungiwa ndani kavunjavunja vitu kibao.

Ila ile MUKU naona kama inahusiana na mambo ya kishirikina hivi au unaonaje?
 
Sawa sawa mkuu lile lilikuwa chama, Na zamaani palikuwa na timu ya kuitwa wonder boys kama utaikumbuka.
Maana ni zamani sana sitokua naikumbuka ila ukitaja eneo nitaikumbuka,ile ligi nadhani ilikua ya mwisho au ya pili kutoka mwisho kwenye ule uwanja

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Oscar Fussi alikuwa na kipaji sana lakini ligi kuu hakucheza kipindi yupo kwenye fomu nilikuwa namuona kwenye mechi uwanja wa Tandale na pale Stendi
Ni kweli mkuu! Vipaji vingi vimepotelea pale tukuyu tatizo ya exposure. Last time nimeenda 2kuyu pale uwanja wa ccm pamekua Stendi ya magari, kule tandale bado wanacheza mpira lakina hakuna mzuka km zamani
 
Os
Ni kweli mkuu! Vipaji vingi vimepotelea pale tukuyu tatizo ya exposure. Last time nimeenda 2kuyu pale uwanja wa ccm pamekua Stendi ya magari, kule tandale bado wanacheza mpira lakina hakuna mzuka km zamani
Oscar miaka ya 2005 akiwa kwenye fomu alifanya majaribio Tanzania Prisons lakini hakucheza ligi kuu
 
Mbili chali f.c

Ujiji mwananyamala hii.....
Kipunje alikuwa anchezesha mpira na panga ktk kanzu[emoji23]
 
1. Mwakandambwa Fc - Kipawa
2. Palestina Fc- Mzambarauni
3.Black wizards - Goms
4.Goms nature - Goma
 
Maana ni zamani sana sitokua naikumbuka ila ukitaja eneo nitaikumbuka,ile ligi nadhani ilikua ya mwisho au ya pili kutoka mwisho kwenye ule uwanja

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
Wakati hata sekondari ya kambanwa haijajengwa, uwanja ulikuwepo pale ilipojengwa ile ghorofa.Timu ilikuwa ya pascal ambae ni padri mtoto wa mama bahati.
 
Kabisa ndugu, mm nimekulia magomeni kagera, viwanja km shoka, kifa, barafu, garden, quinea, gombelo, kinesi vyote nimevuruga ilikuwa ubabe kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…