Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Mr Kavishe - Lwandai Secondary school. Huyu jamaa alikuwa ni Second Master. Usiombe akutie mikononi
 
Mwalimu Kishazi Mawenzi sec,
Head master Mr Lwamwasi Old Moshi Sec,
Old moshi Sekondari - Huwezi kuitaja hiyo shule ukamuacha Headmaster aliyejulikana kama - Mtui (Mr)
miaka ya 1990- Alibadilisha Shule ikawa inafaulisha kama special school. Nafikiri yule alikuwa mwanajeshi
Kusimamia nidhamu ya wanafunzi wa kiume zaidi ya 1200 wote wa bweni (o-level & A-level) sio mchezo
 
5. Mwalimu Mpande - Moshi Technical Secondary School. Huyu mwalimu kwenye umisetta alikuwa tishio. Ukileta zako ni kibano unakula.
Umenikumbusha mbali. Nilikuwa pale 1981 mpaka 1984. Mpande namkumbuka sana kwenye mchakamcha saa 11 asubuhi.

Waalimu wetu wa miaka ile- Michael Malale, headmaster; Kasenge, second master; Isack Malisa, academic master, Nzohi, maths, baadae secondmaster; Bhatia & Mikhailov, Engineering science; Mama Mayasa, chemistry, etc
 
Mwalimu Walter jina la utani aliitwa Kimbunga wakati nasoma shule ya sekondari KWIRO huyu mzee alikuwa ni mkorofi haswa bahati mbaya sana nimeajiriwa nikakutana naye tena halmashauri moja huko Singida alipewa cheo cha MTAALUMA wa sekondari aliendelea na tabia ile ile ya kunyanyasa watumishi hasa walimu ,kutokana na tabia mbovu alitimuliwa saizi yupo Singida mjini anatembeza mafaili .

Kimbunga alikuja kuchukua nafasi ya kandoro..

Kandoro nae alikua anatupelekesha na jorgin asubuh…
 
Mwalimu 'Macho kumchuzi' [emoji16]
Alikuwa akikuangalia ni kama alikuwa anaomboleza hivi. Macho yalikuwa yanatokatoka mchuzi!

Mwalimu 'Mabangi' [emoji16]
Alikuwa akikohoa, nikama alikuwa akihitaji mapafu yatoke nje! [emoji23]

Mwalimu 'Kishundu'
Huyu kishundu sasa ndio ilikuwa balaa, sisi tulikuwa tunapenda aandike tu ubaoni tutajisomea wenyewe! [emoji23]

Natunza ID zao, ila kama mmo humu, mnajua kabisa majina yenu. [emoji16]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]nimecheka sana, ila wanafunzi kwa kutungia walimu majina [emoji119]
 
Ahahahahah, Domician Mkama huyu huyu ninae mfahamu?
 
JJ Kaaya miaka hiyo Minaki High School ulikuwa moto wa kuotea mbali.
Alinitwanga mingumi sana siku moja
 
Mwalimu Barosha, a.k.a isithubutu kukutwa na bwana pepsi. Tabora Boys 😁😁😁😁, Mwalimu Moris Mirambi, a.k.a Momi Munanila Secondary School.(Burton Rulanitse) Nyongeza😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom