Tulikutana behind anonymous usernames, urafiki ukawa halisi, lakini leo hatujui walipo wala kama kuna siku tutasikia habari zao tenađź’”

Tulikutana behind anonymous usernames, urafiki ukawa halisi, lakini leo hatujui walipo wala kama kuna siku tutasikia habari zao tenađź’”

Wasalaam,

Maisha ni fumbo lisilo na majibu ya moja kwa moja, leo tunakutana na watu, tunajenga ukaribu wa mda mrefu, lakini kesho hatujui njia zetu zitatupeleka wapi. Wengine huwa sehemu ya maisha yetu kwa muda mfupi, lakini alama wanayoacha mioyoni mwetu hudumu kwa miaka.

Wakati mwingine, kinachouma zaidi si kupoteza mawasiliano na mtu, bali ni kutokujua kama yuko salama, anaendeleaje na maisha yake, au kama kuna siku mtapata nafasi ya kuzungumza tena.

Perhaps one day, you will log in hoping to find a familiar username, only to realize that someone who was once part of your daily conversations has become a distant memory, with no way of knowing where life has taken them.

Ndiyo maana ni muhimu kuthaminiana tunapopata nafasi. Maana nyuma ya kila username kuna binadamu mwenye hisia, changamoto na maisha yake binafsi.

Special shout-out kwa wale tuliokutana hapa JF, lakini urafiki wetu ukavuka mipaka ya jukwaa hili. Kwa wale ambao hadi leo tunawasiliana, tunakutana na kunapeana updates za maisha, tunashauriana na kuendeleza ujamaa wetu nje ya anonymous usernames.

Some friendships begin anonymously, but leave memories that last a lifetime.

Paula Paul


Wasalaam,

Mla bata

München, Deutschland 🇩🇪.
Bwana huyu yuko wapi?
 
Back
Top Bottom