HOJA Tuliovaa Jeans, T-shirt, raba tumezuiwa kufanya usaili katika ajira ya TRC, hii ni sawa?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Kwani mavazi nadhifu ni suti tu? Huwezi kuvaa suluari na shati za kawaida na ukaonekana nadhifu?
 
Eeh hapo umegusa jambo la watu wengi mkuu, mimi nikienda usaili huwa najaribu kufuata mavazi yao ingawa wakati mwingine inakera, lakini ndio mfumo wetu hivi, unakuta wengine wanaweza kuwa na uwezo zaidi lakini wamezuiwa kwa sura.
Ni taifa la wajinga linalompima mtu kwenye suala la kitaaluma kwa muonekano. Ajabu air Tanzania ilipokatwa South Africa, wakili wao (serikali ya Tanzania) akawa ni mwenye rasta kichwani na hereni sikioni na wakashinda kesi๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜†, hawajifunzi tu?
 
Usiende kwenye usaili mana hata ukienda hutofanya huo usaili
Basi kuna siku mshikaji wangu alikuwa ananisimulia siku hizi ukinda huko kwenye usahili wa vitendo ukizingua unarekodiwa kabisa wakati wa vitendo! Usijekusema nilifanya vizuri nikakatwa au nimeonewa.
So hata hawa wadau wa tshirt na jinsi wangerekodiwa kabisa.
Ili kupunguza lawama za baadae...
Nimechekeka sana
 
Watu wa usaili wanatakiwa kuwa na viboko kwa ajili ya wapuuzi kama huyu mtoa mada
 
Vijana wa kitanzania wamekuwa kama manguruwe siku hizi. Sisi miaka ya 70 kabla ya kwenda kwenye interview
๐Ÿ”ธ Tulikuwa tunajiandaa nawonekano, tunatafuta na hata kuazima mavazi yatakauotupnyesha tupo smart na ya kiheshima

๐Ÿ”ธ Tulikuwa tunanuoa nywele kiheshima , KUEPUKA kupaka manukato , viatu tuna brash

๐Ÿ”ธ Tulikuwa tunafanya utafiti kwanza Kwa watu walioajiriwa kwenye kampuni hiyo kujua dressing code ikoje

๐Ÿ”ธ Tulipeleleza possible questions na mitego ambayo wabobezi wa interview wa zamani walikuwa wanatutega kupima nidhamu yetu, mfano anazuga amefonfosha kalamu makusudi? tulikuwa tunapeleleza namna ya kusalimia

๐Ÿ”น Lakini kizazi hiki Cha Nguruwe kinanda kutafuta maisha kina dred kichwani, visuruali havieleweki ni suruali au kaptula halafu kaweka kata k na Wala hakajali. Wa kike ndio balaa kabisa wanakwenda wamevalia kama changu
 
Aisee hiki kizazi cha sasa kweli shida,hivi wewe umeshindwa hata kujiongeza...interview inabeba mambo mengi ikiwemo muonekano wako.
Unapokaa kwenye kiti/meza ya interview kuna mikao yake siyo unajikalia tu kama upo kibanda umiza.
Pale huwa unaangaliwa macho yako,umekaaje,umevaaje,unaongeaje,unajibu vipi maswali lakini pia ndani ya interview kuna activities ndogo ndogo zinaweza kujitokeza....usishangae anaekufanyia interview anachomoa pakiti ya sigara anawasha anavuta huku anakuhoji kisha anachomoa tena sigara nyingine tena anakurushia na kiberiti na wewe uwashe...

Kuws makini kila hatua iinterview ni kifurushi cha wewe kupekuliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ